agathaM
Member
- May 24, 2024
- 14
- 25
Biashara kitu kizuri sanaHabari wakuu:
Nafanya biashara ya duka la rejareja yapata miaka 6 sasa mafanikio makubwa nimeyapata kupitia hii biashara hakika sijutii kuingia katika hii biashara...
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Biashara kitu kizuri sanaHabari wakuu:
Nafanya biashara ya duka la rejareja yapata miaka 6 sasa mafanikio makubwa nimeyapata kupitia hii biashara hakika sijutii kuingia katika hii biashara...
Faida yake ni ndogo sana. Ni moja ya sababu zilizonifanya nikabadili biashara aisee. Biashara ya duka la takataka buana, wateja kumi wanakuachia faida ya elfu 5 wkt biashara kama ya nguo au urembo hiyo elfu 5 unaipata kwa mteja mmoja.Haya mafuta futa mengi sana kwenye ngazi,japo huwa yanapendezesha sana duka lakin faida yake huwa ni nzuri kweli
Chuma ulete ni matokeo ya kuibiwa na mfanyakazi wako ama kuingiza matumizi binafsi kwenye fedha za mauzo.Hakuna kitu kinaitwa chumaulete hata mimi ningenunua hilo jini nile maishaHii imani mimi sina
Fanya mil5 itapendeza sana mkuuHii biashara naidandia siku si nyingi.
Nanyemelea mwezi wa 12,, vimillion 3 vyangu nije nivibananishe huku, nimechoka masimango ya Mabossi.
Mtaji kiasi gani mkuu? Nina ki 2.5m nataka niingie huko,, sina cha kufanya graduate mimiNimeanza nayo mwaka huu,si haba natumai itaendelea kuwa nzuri hivi hivi
daaah mkuu hapa umetusaidia wengi sanaCha kwanza mpe uoga kuwa unaijua kazi yako vizuri, pia uwe na dadtari la kupokelea Mali dukani kwa mfumo wa
Aina ya bidhaa!
Kias
Bei ya kununulia
Bei ya kuuza
FAIDA
Ukitaka kujua umeibiwa au hujaibiwa
Jumlisha FAIDA zote
Toa matumizi yako yote
Toa pia akiba uliyosave
Kinachobaki kinatakiwa kionekane kama ongezeko kwenye mtaji
Hii ni RAHISI SANA
Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
asantePoleni na pilika za kutwa na hongeren pia kwa ibada
Mchango wangu ni mdogo sana Ila unaweza kukusaidia
1:kama unataka kufungua duka tafuta eneo lililochangamka lenye movement ya watu kwa nyakati zote za siku,
2: chunguza kwa makini waliokutangulia Wana udhaufu gani, Kisha usiwe na udhaufu kama wao
3 baada ya kufungua fanya haya
Fungua mapema, Sali/swali, ikabidhi kazi yako mikonon mwa mungu, uwe msafi, uwe na kauli nzuri kwa watu, panga bidhaa zako kwa mpangilio mzuri epuka mopo
Epuka mazoea mabaya na mabint, wake za watu
Kauli yako iwe ni moja shemeji, dada karibu
Jenga urafiki n watoto na wazee
Epuka anasa weka malengo
Funga kwa kuchelewa
UPATIKANAJI WA FAIDA
tafuta machimbo yenye bidhaa kwa Bei nzuri
Wastani wa FAIDA kwa kila bidhaa ni 25 %au Zaid
Nafaka, na vinginevyo
Kwa maana hiyo ukitoa FAIDA ya 15% tambua kuwa 10%umeiacha dukani kwa ajili ya kuendeleza kukuza mtaji
Pia Kuna bidhaa zenye FAIDA kubwa Zaid ya hiyo kutikana na chimbo ulilopata
JINSI YA KUTHIBITI KUIBIWA NA MFANYA KAZI
1: Ukishafungua duka piga stock na mtu atakayeuza
2:nunua dadtari 2 moja yako nyingine yake
3:chora daftar yako mistari kadhaa ainisha haya
Iterm name,
Idadi/kiasi
Bei ya kununua
Bei ya kuuza,
Faida
NB
Ukininua kila kitu hata kama ni pipi ingiza kwenye daftri yako kwa mfumo huo na yéye pia muelekeze afanye hivyo,
Ukitaka kupiga stock Rudi kwenye daftari lako mwambie yy pia alete lake
Jumlisheni faida zote kuanzia stock ya mwisho Hadi tarehe husika
Pia mkumbushe kuandika matumizi yote yanayotoka ukani mfano
Kodi
Ushuru wa taka
Malipo tra
Malipo manispaa
Nauli za kuleta vitu mjini
Na mengineyo
Ikumbukwe kwamba matumizi yanaweza kuandikwa kwenye daftri lilelile la kupokelea vitu vya mjini lakin figure zake ziandikwe kwenye mstari wa FAIDA Ila ziwekewe mabano ili mtu ajue hiyo hela imetoka na siyo faida
Kwa mfumo huo hata mfanyakazi akinywa soda lazima kwenye stock utakuta shoti ya 600/=
Mimi ndio ulinisaidia Hadi hapa nilipo!
Nina duka Zaid ya moja Ila Cha kumshukuru mungu Nina duka linaweza kuuza 500k Hadi 700k kwa siku
Mimi natumia mfumo huo na mara nyingi nakuwa hapo usiku tu kuwahudumia na kujua changamoto za wateja wangu na kujua nini Cha kuongezea dukani na ni kitu gani kipya kimeuliziwa na Sina,
Conclusion
Biashara ya duka inalipa Ila unatakiwa kuwa smart
Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
Nimeanza na 1.7 na eneo ni zuri kwakweli, nilikua na 2.3,kama 600 ikapungua kwenye kodi,kurekebisha fremu kidogo na kuandaa baadhi ya vifaaMtaji kiasi gani mkuu? Nina ki 2.5m nataka niingie huko,, sina cha kufanya graduate mimi
Hongera mkuu.Nimeanza na 1.7 na eneo ni zuri kwakweli, nilikua na 2.3,kama 600 ikapungua kwenye kodi,kurekebisha fremu kidogo na kuandaa baadhi ya vifaa