Niulize chochote kuhusu biashara ya duka la rejareja

Habari wakuu:

Nafanya biashara ya duka la rejareja yapata miaka 6 sasa mafanikio makubwa nimeyapata kupitia hii biashara hakika sijutii kuingia katika hii biashara...
Biashara kitu kizuri sana
 
Haya mafuta futa mengi sana kwenye ngazi,japo huwa yanapendezesha sana duka lakin faida yake huwa ni nzuri kweli
Faida yake ni ndogo sana. Ni moja ya sababu zilizonifanya nikabadili biashara aisee. Biashara ya duka la takataka buana, wateja kumi wanakuachia faida ya elfu 5 wkt biashara kama ya nguo au urembo hiyo elfu 5 unaipata kwa mteja mmoja.

Wadau watatetea kwamba unapata wateja wengi kwenye duka la takataka, sikatai ila faida ya hiyo biashara inaumiza kichwa sana
 
Hii biashara naidandia siku si nyingi.
Nanyemelea mwezi wa 12,, vimillion 3 vyangu nije nivibananishe huku, nimechoka masimango ya Mabossi.
 
Kazi ngumuu hiii,kunavitu mpaka vinaexpire hujaviuza na ulizika elaa
 
Hii imani mimi sina
Chuma ulete ni matokeo ya kuibiwa na mfanyakazi wako ama kuingiza matumizi binafsi kwenye fedha za mauzo.Hakuna kitu kinaitwa chumaulete hata mimi ningenunua hilo jini nile maisha
 
Hii biashara naidandia siku si nyingi.
Nanyemelea mwezi wa 12,, vimillion 3 vyangu nije nivibananishe huku, nimechoka masimango ya Mabossi.
Fanya mil5 itapendeza sana mkuu
 
Miaka ya 2011 niliwahi kufanya biashara hii ila si Kwa bidhaa zote mm nilishughulika na first consumed goods( FCG) aisee tuliuza na ndugu yangu hadi ilikuwa sio poa na tulikuwa karibu na soko , yaan hadi tuliwekewa kikao Cha Siri maana ndani ya mwezi mmoja tulibadili upepo wa wateja Kwa mbinu Moja mjarabu hii biashara inaitaji sehemu ya watu wa kipato Cha kati hadi chini . Hadi Leo Banda letu bado lipo ingawa tulilikodisha any time naweza Rudi kuchukua heshima yangu hata nikiwa likizo uwa nikiludi home naenda mitaa Ile wamama uwa wananipigia saluti wanaielewa moto tuliowapelekea mitaa Ile .
 
daaah mkuu hapa umetusaidia wengi sana
 
a
asante
 
Mtaji kiasi gani mkuu? Nina ki 2.5m nataka niingie huko,, sina cha kufanya graduate mimi
Nimeanza na 1.7 na eneo ni zuri kwakweli, nilikua na 2.3,kama 600 ikapungua kwenye kodi,kurekebisha fremu kidogo na kuandaa baadhi ya vifaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…