Hi swali nilishawahi kulijibu katika thread nyingine. Overhaul ya engine yoyote kwanza huwa siyo jambo la lazima sana labda kama gari ilitumika vibaya bila kuwa na oil na coolant ikafikia kuunguza Crankshaft bearings na mpaka kuharibu pistons.
Overhaul yoyote hupunguza ubora injini hiyo kwa sababu huondoa genuine parts na kuweka OEM parts ambazo hazina ubora kama ule wa genuine parts. Mara nyingi overhaul huwa siyo ya lazima kwa sababu injini nyingi huchoka kwa kuharibika vitu vichache tu ambavyo zaidi ya Spark plugs na ignition coils, ni pamoja na oil seals, bearings, AC/Clutch, timing belt, valve lifters(tappets), fuel pump, timing belt, fuel filter, fuel pressure regulator, labda na sensors za injini kama air flow sensor, oxygen sensor, manifold absolute pressure sensor, throttle position sensor na sensor nyingenezo ambazo utazitambua kwa kupitisha injini yako kwenye computer scan. Vyote hivyo huweza kubadilishwa bila kufanya engine overhaul.
Matatizo ya kufanya Overhaul hasa unapofikia kubadilisha pistons ni kuwa mara nyingi piston unazoweza huwa hazina uzito sawa na zilie zilizokuwamo mwanzo, na hapo ndipo mwanzo wa matatizo ya injini kushindwa kazi, na tatizo hilo huwa ni kubwa zaidi iwapo utabadilisha piston chache tu na kuacha nyingine. Tatizo jingine la overhaul ambalo ni rahisi sana kufanywa na mafundi wasiokuwa makini ni kukosea kidogo sana ile crank angle ya TDC na BDC. Ni pembe ndogo sana lakini inapokosewa basi nayo huleta matatizo makubwa katika utendaji wa injini yako. Kuna injini ambazo ni sensitive sana kwenye makosa hayo na kuna injini ambazo ni robust kiasi cha kuyahimili..
Mwisho ni vigumu kukupa jibu sahihi mpaka nikague injini yako, majibu hayo hpo juu ni yale ya jumla jumla tu.