Kama walisafisha radiator vizuri; na bado gari linachemsha basi sababu kubwa itakuwa ni water pump. Kwa kawaida gari ikiwa na km 150,000 unatakiwa ubadilishe vitu kadhaa kama vile water pump, idler pulley na AC clucth, na iwapo inatumia timing belt, basi nayo ubadilishe. Sasa kama gari yako ikow kwenye range hiyo ya km 135,000, hadi 165,000 basi huenda water pump yako ndiyo mgomvi wako mkuu. Kama sivyo huenda pia motor ya fan nayo itakuwa imeaza kuchoka, lakini tatizo nina imani kubwa kuwa adui yako ni water pump tu.