Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
- Thread starter
- #301
Nishawahi kukatazwa na dealer wa Toyota kutumia injector cleaner,yeye alisema once ukianza basi inatakiwa utumie kila unapojaza mafuta hasa kwa kuwa filling station nyingi kwa bongo zinauza mafuta machafu (ambapo sikumuelewa kwa kweli)
1. Je, kuna ukweli katika hilo?
2. Nikiweka mafuta kwenye vituo vya kawaida gari haina mis,lakini nikiweka kwenye vituo vya TOTAL then nikarudi kwa vingine mis hutokea na sometimes gari kuzima na kusumbua kuwaka,Je,ni formula ya mafuta kutofautiana au kuna sensor kwenye gari haipo sawa?.
Shukrani.
Huyo dealer alikudanganya, labda alitaka ukishakpata matatizo umrudie. Injector cleaner ukiitumia vizuri, hasa ukitumia ratio nzuri, chupa moja kwa full tanki labda mara moja kila baada miezi miwili unaongeza sana maisha na ubora wa injector zako; ndiyo maana hizo cleaner zipo madukani. Ni kweli kuwa kuna vituo siyo waaminifu, wanauza mafuta yasiyo na Octane number inayotakiwa. Kwa bahati mbaya sina jibu rahisi kukusaidia, kwani ubora wa amafuta ni kazi ya wachujaji. Labda sehemu nyingine huchanganya Regular na Super kwa sababu hizo zina octane number tofauti.