Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Shukrani mkuu.Nina injini hii ya 1ZZ-FE, (1794cc), kwenye hii injini, vibrations ni kitu cha kawaida, ila ikizidi, mwambie fundi aangalie engine mounts, kama zile bushes zake zimechoka, ndani utapata mtikisiko mkubwa ukiweka drive na ukasimama kama ukiwa kwenye foleni.
Pili, muungurumo kuwa mkubwa kunaweza sababishwa na oil uliyoweka. Kama umeweka oil nzito mfano 20w 40, lazima injini itakuwa na mvumo mkubwa hasa asubuhi ukiiwasha. Na gari huchelewa kuchanganya.
Tatu, injini hiyo, muundo wake ni kuwa, hasa asubuhi, ukiiwasha, muungurumo huwa juu, na kadri inavyopata moto, muungurumo unashuka. Ukiwa ndani utaona mshale wa RPM unashuka taratibu, ukifika kwenye 650-700 kutoka kwenye 1500, utaona inakuwa calm kabisa, na unaweza kuondoka sasa.
Nne, safisha air filter mara kwa mara. Unapoenda kujaza upepo, toa air filter nayo ipigwe upepo kutoa vumbi.
NB: nimetumia gari yenye injini hii kwa miaka 5 sasa, hayo yote niliyoelezea nimeyapitia. Oil weka 5w 30. Leo nimenunua ya Toyota lita 4, elfu 75.
Usishangae kuhusu utambulisho huu. Mimi sasa ni ASE Certified Service Consultant wa magari madogo yanayotumia petroli hasa ya Ford, GM, na Chrysler. Nimepata license yangu hivi majuzi tu mwaka huu baada ya kuitafuta kwa muda kidogo through part-time activities kwani hiyo siyo kazi yangu kuu. Certification hiyo inahitaji siyo tu kufaulu mtihani wake, lakini pia uwe na uzoefu wa kutosha kwenye auto-repair shop. Nimekamilisha experience hiyo inayotakiwa mwaka huu na kupata license yangu.
Kwa vile injini nyingi za petroli zinafanana katika utendaji, jisikie free kuniuliza swali lolote kuhusu matatizo ya injini ya gari yako model yoyote inayotumia mafuta ya petroli.
Siahidi kuwa majibu yangu yote yatakuwa ni sahihi, lakini sehemu kubwa itakuwa ni sahihi, na hata yale ambayo hayatakuwa sahihi yanaweza kukusadia kujua wapi pa kuanzia.
Nilikutana nayo, gari ilikuwa inaishiwa nguvu kwenye miinuko na overtaking ikawa changamoto. Ukikanyaga accelerator, inachukua sekunde 4-5 kujibu. Baada ya kuweka fuel pump mpya, tatizo likaondoka. Ni kama mwezi mmoja uliopita.Shukrani mkuu.
Nitayazingatia haya.
Vipi kwenye mfumo wa mafuta hasa usukumaji, hujawahi kutana na changamot?
Dah! Nimeweka hii kwenye Starlet unanishauri nini mkuuHapana, oil hiyo ni nzito sana kwa injini ndogo; nakushauri usiweke oil inayozidi 10W-30 kwenye gari ndogo. Ushauri kamili ni 10W-20, 5W-30, 10W-30. Ukiweka 10W-40 au SAE40 kwa gari lenye milage kubwa sana utalisikia pia muungurumo wake ukibadilika kuwa kama wa trekta.
Hata mimi hii ya kuchelewa kuchanganya inanipata na hata ukitaka ku overtake inabidi ujipange hasa.Nilikutana nayo, gari ilikuwa inaishiwa nguvu kwenye miinuko na overtaking ikawa changamoto. Ukikanyaga accelerator, inachukua sekunde 4-5 kujibu. Baada ya kuweka fuel pump mpya, tatizo likaondoka. Ni kama mwezi mmoja uliopita.
Maeneo ya Tabata Baracuda kwa laki na nusu.Hata mimi hii ya kuchelewa kuchanganya inanipata na hata ukitaka ku overtake inabidi ujipange hasa.
Pump ulipata kwa bei gani na wapi mkuu.
Uzito wa hii oil ndugu umeingia chaka tayari. Ni nzito sana kwa gari ndogo. Kuna Canter moja, recommended oil yake ni 15w40, Canter ya kubeba mchanga. Wewe umeweka oil ya gari kubwa zaidi hata ya hiyo Canter.Dah! Nimeweka hii kwenye Starlet unanishauri nini mkuu View attachment 1245472
Oil la katapila hiloDah! Nimeweka hii kwenye Starlet unanishauri nini mkuu View attachment 1245472
Ngoja nijipange kumuona fundi.Maeneo ya Tabata Baracuda kwa laki na nusu.
Mkuu, kwanza nikushukuru wewe na wadau wote kwa elimu hii. Nimekuwa kwenye mgogoro wa engine ya ESCUDO G16 ni oil gani inafaa. Hii ni baada ya kununua engine nyingine (used) baada ya ile ya kwanza kushindikana. Fundi anashauri nitumie SAE 40 lakini nikambishia baada ya kupitia uzi huu. Ndiyo kwanza tumeipandisha kwenye gari na hatujabadili oil. Gari haina 'manual'. Nahitaji ushauri wako/wenu tafadhali, maana ni mgeni kwenye hii tasnia.Hiyo siyo injini ya gari ndogo bali ni ya katapila.
Tumia mojawapo ya hizi: SAE30, 5W-30,10W-30Mkuu, kwanza nikushukuru wewe na wadau wote kwa elimu hii. Nimekuwa kwenye mgogoro wa engine ya ESCUDO G16 ni oil gani inafaa. Hii ni baada ya kununua engine nyingine (used) baada ya ile ya kwanza kushindikana. Fundi anashauri nitumie SAE 40 lakini nikambishia baada ya kupitia uzi huu. Ndiyo kwanza tumeipandisha kwenye gari na hatujabadili oil. Gari haina 'manual'. Nahitaji ushauri wako/wenu tafadhali, maana ni mgeni kwenye hii tasnia.
Mkuu, Ubarikiwe sana kwa ufafanuzi wako. Nimefanikiwa kupata aina mojawapo kama inavyoonekana kwenye picha hapa chiniTumia mojawapo ya hizi: SAE30, 5W-30,10W-30
Hizo SAE40 hadi SAE50 ndizo zinazowaulia injini mapema na kusababisha wengine wafanye overahaul kwa sababu ni nzito sana na zinasababisha piston rings kusagika haraka sana.
Hii wamekuuzia sh. Ngapi mkuu,Mkuu, Ubarikiwe sana kwa ufafanuzi wako. Nimefanikiwa kupata aina mojawapo kama inavyoonekana kwenye picha hapa chini
Asante sana.
Alikuwa anauza 110,000/= lakini tumepunguziana mpaka TSH 100,000/=. Niko Mwanza.Hii wamekuuzia sh. Ngapi mkuu,
Safi sana mkuu.Alikuwa anauza 110,000/= lakini tumepunguziana mpaka TSH 100,000/=. Niko Mwanza.
Hii unaimwaga baada ya km ngapi..??Alikuwa anauza 110,000/= lakini tumepunguziana mpaka TSH 100,000/=. Niko Mwanza.