Mkuu kuna scenario imenitokea juzi nimeshindwa kuielewa. Kuna Nissan Serena 2011 engine ya C26 ina kama week tatu. Nilivyoifuata bandarini tulifanya service na wakaweka oil ya Takumi kama inavyonekana kwenye picha
Juzi nilikiwa safarini kutoka Arusha kwenda Iringa, asubuhi nikacheck oil na ilikuwa poa kabisa na nikaanza safari mpaka iringa, nilikiwa naenda 130-150kph na nilifika salama Iringa kabisa. Asubuhi yake nikacheck engine oil kabla ya kuanza safari nyingine nikakuta engine kavu kabisa hamna oil! Nikamfuata fundi kuja kucheck naye akasema hamna oil. Basi tukafuata oil ya total quartz 9000 (synthetic) na kuongeza ili tuweze kuipeleka gari garage ili tuweze kuiangalia kwa undani. Cha kushangaza hakukuwa na leakage yoyote! Baada ya kuhakikisha hakuna leakage nikaendelea na safari ya kama km 400 na nilifika salama na oil ipo level ile ile tuliongeza! bado najiuliza ile oil ya mwanzo ilipotelea wapi?
View attachment 1252356