Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Bin Chuma75,
Maswali ya ulaji wa mafuta yameshajibiwa sana hapa; hakuna jibu moja la kwa nini gari yako inakula mafuta sana. Inahitaji fundi alikague gari lako hasa sehemu zifuatazo: (a) Spark plugs an Injectors, (b) Air flow sensor (c) manifold air pressure sensor, (d) air cleaner, (e) fuel pump, na (f) fuel pressure regulator. Vile vile angalia upepo kwenye matairi yako, pamoja na wheel alignment.
 
Wakuu nnakigari changu Aina ya Verrosa , Kuna muda inakosa nguvu kabisa, Sasa wataalam wakanishauri nibadili gear box, nikabadili lakini bado tatizo Hilo naliona bado linarejea.
Ushauri wazee

Sent using Jamii Forums mobile app
Fundi aliyekuwambia ubadili gia box alikuingiza kwenye chaka la simba, na wala usijemrudia kabisa. Uziefu wangu wa magari mbalimbali unaonyesha kuwa tatizo lako linatokana na fuel system tu. Culprit mkubwa atakuwa ni fuel pump kwa asilimia kubwa sana. Baada ya hapo angalia sehemu nyingine za fuel system kama vile fuel pressure regulator, na injectors.

Kama gari yako ina fuel filter, basi iangalie hiyo pia, ila magari mengi ya siku hizi fuel filter imejengewa kwenye fuelr pressure regulator. Iwapo gari yako ina sifa ya kula mafuta sana, basi angalia pia air cleaner yako, kwani inachangia uchomaji wa mafuta kwenye injini hata kama mafuta yamefika vizuri. Yakishakosa hewa ya kutosha basi hayatachomwa na hivyo injini kukosa nguvu huku mafuta yote yakitupwa kwenye exhaust bila kufanya kazi yoyote ya maana kwenye injini.
 
Mkuu Kichuguu samahani binafsi ninamiliki landcruiser 70 series yenye engine ya 3b. Je ni oil ipi nzuri. Mileage is about 253000 kms. Pia nina hilux 12r ya zamani kidogo nani itumie oil ipi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Kichuguu samahani binafsi ninamiliki landcruiser 70 series yenye engine ya 3b. Je ni oil ipi nzuri. Mileage is about 253000 kms. Pia nina hilux 12r ya zamani kidogo nani itumie oil ipi

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa gari ndogo yoyote, oil ni 5W-30 au 10W-30 tu. Ni kwa magari makubwa pamoja na ya dizeli ndipo unapoweza kutumia oili nzito zaidi ya hapo.
 
Kiongozi naomba kujua hasara ya kutoa thermostat na faida ya kuwepo thermostat kwenye gari

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna watu wengi ambao huondoa thermostat kabisa, na bado magari yakaendelea kufanya kazi. hata hivyo, kufanya hivyo hupunguza ubora wa injini kwa sababu kadhaa kuhusiana na joto la injini. Unapoondoa thermostat, unakuwa umefungulia maji ya cooling system kama vile umeacha bomba wazi, kwa hiyo yanaanza kuzunguka mara tu unapowasha injini, hivyo yanazunguka kwa presha ndogo ambayo husababisha yasipooze injini yako vizuri mpaka joto liwe kubwa sana ndipo pressure ya maji pia inaongezeka. Matokeo yake ni kuwa injini inakuwa inapata joto kubwa sana, na vile vile kupoa mpaka joto la chini sana kwa kujirudiarudia. Sasa huo mzunguko huo wa joto la juu, na joto la chini husababisha expansion na contraction ya mara kwa mara ambayo huweza kupasua cylinder head. Kazi kubwa ya thermostat ni kuhakikisha kuwa joto la injini liko katika kiwango fulani, siyo chini sana wala juu sana.
 
Kuna watu wengi ambao huondoa thermostat kabisa, lna bado magari yakaendelea kufanya kazi. hata hivyo, kufanya hivyo hupunguza ubora wa injini kwa sababu kadhaa kuhusiana na joto la injini. Unapooondoa thermostat...
Naenda kuweka ya kwangu.Kuna fundi aliitoa, gari ilikuwa ina overheat.

Nakushukuru kwa maelezo mujarab
 
Noah old model inasumbua sana kuwaka wakati wa asubuhi unaweza kupiga self hadi mara 10 ndio iwake, ila ikisha waka haisumbui tena tatizo ni nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio hata mm ka vist kangu niliondoaga.
Mafundi wengi huwa wanashauri kuondoa thermostat kwenye gari kutokana na hali ya hewa ya joto ya huku Je kuna ulazima wa kufanya hivyo?

121.
 
Gari yangu aina ya Nissan pickup ina jam sana breki za mbele naomba msaada. Nimepiga msasa piston lakini bado zinajam

Sent using Jamii Forums mobile app
Inawezekana kuna upepo kwenye line ya brake fluid; je umeshafanya bleeding? Au Brake calippers hazina gris, je umeangalia kama brake calipers zina gris ya kutosha, au disks za brake zimeshalika.
 
Habarini wakuu.

Mi nahitaji kusaidiwa vitu vyoote muhimu kafika gari kwa ufupi na kwa uhakika zaidi.

Msaada kwenu wadau.

Nimenunua gari haina hata siku 5.

Mileage 35,000. Ist engine 2NV. Cc1290.
Nahitaji kusaidiwa kanuni za kitaalamu juu ya ukaguzi na utunzaji sahihi wa hii gari ili iweze kudumu mda mrefu.

Ukaguz wa kila siku.
Oil na lubricant zingine.
Service kubwa kubwa utaratibu wake.
Na mengineyo kibao...

Maana ninachojua ni kuendesha tu na si kingine... Sasa nahofia kuia gari mapema pasipo kujua.

Msaada wakuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msaada hapa basi au mnangoja mpaka tuziue mje mdis
Habarini wakuu.

Mi nahitaji kusaidiwa vitu vyoote muhimu kafika gari kwa ufupi na kwa uhakika zaidi.

Msaada kwenu wadau.

Nimenunua gari haina hata siku 5.

Mileage 35,000. Ist engine 2NV. Cc1290.
Nahitaji kusaidiwa kanuni za kitaalamu juu ya ukaguzi na utunzaji sahihi wa hii gari ili iweze kudumu mda mrefu.

Ukaguz wa kila siku.
Oil na lubricant zingine.
Service kubwa kubwa utaratibu wake.
Na mengineyo kibao...

Maana ninachojua ni kuendesha tu na si kingine... Sasa nahofia kuia gari mapema pasipo kujua.

Msaada wakuu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom