Mkuu nimekuelewa vyema sasa tujiulize gari inatoka Japan ina Km 80,000 kwetu huku tunaiita mpya, hii hii gari kwetu ikija tembea 30,000 km utaishangaa. AC hazifanyi kazi, mlio wa engine ni tofauti inachoka sana (sisemei kwa zote) tatizo hapa linakua nini mkuu?
Kuna mji China unaitwa Harbin baridi inakua mpaka -6 huku ndio nilijua matumizi ya right oil to your car.
Kuchoka kwa gari kunategemea sababu nyingi sana..
Sababu ya kwanza mazingira...Gari limetoka Japan almost kila sehemu ni lami kwa hiyo gari linakuwa linatembea bila shuruba na mikikimikiki hivyo engine haitumii nguvu kulinganisha na huku kwetu..
Vipuri duni vya kufanyia service..Kwa mfano engine oil na oil filter..
Kwa mfano ukiagiza gari used Japan, likifika tu mafundi wetu hawa wanakushauri umwage oil iliyokuja na gari uweke SAE 40 eti ndiyo inayofaa Tanzania..
Hapo inakuwa ni sawa na wewe una damu group O, unalazimishwa kuwekewa group B ..lazima utaumia.
Hiyo oil yenyewe wakishaweka SAE 40, wanakuwekea na oil filter ya 3500/-..
Hapa lazima Engine ichoke mapema sana na kuanza kubadilisha milio..
Watu pia hawaweki spark plugs ambazo zimependekezwa...huwezi kuqmini mtu amenunua gari milioni 13, anaweka plugs za buku 4 kwa moja..hapa lazima Engine itakuwa ina... struggle ili kipata full combustion..
Mafundi wetu wanatabia common ya kutoa thermostat, kisha wanakushauri usiingie gharama ya coolant, uweke maji ya bomba..
Kipato duni kinafanya magari yetu yachoke mapema...kwa mfano mtu anamiliki gari dogo kama Passo au IST, hilo hilo ndiyo la kwenye lami na tope, mjini na mashambani, milimani kama Upareni na Tambarare...kama ana duka hilo hilo gari ndiyo lakubebea bidhaa za dukani...lazima gari lichoke mapema.
Wenzetu kwenye nchi zilizoendelea utakuta ana gari zaidi ya moja...na mara nyingi huwa ni SUV, Gari ndogo na pick up kubwa kama Amarok, Takoma au Navara....kwa hiyo kila gari inakuwa na matumizi yake.
Mafuta ya petrol yenye kiwango duni...na hiki ndiycho kilio kikubwa, kikifuatiwa na SAE 40 pamja na maji ya bomba.
Mwisho Watanzania wengi hatuna desturi ya kutunza mali zetu, hatufuati kanuni zilizopendekezwa na manufacturers na tunaogopa bei ya spea genuine na hii ndiyo sababu watu wengi wameegemea kwenye Toyota vile wana uhakika wa spea feki za bei rahisi