Habari kiongozi.
Nina tatizo kubwa saaana nahitaji msaada wako,
Nina gari IST ya 2006 old model, cc1290
Nilipitisha muda wa oil hadi ukoko ukanasia kwenye sample tukasafisha na petrol tukamwaga nikaweka filter mpya na oil mpya...
Nikatembelea kwa week tatu oil mpya yoote ikapotea kwenye gari na hakuna leakage yoyote.... Gari ikawa inatoa moshi mkubwa saaana mweupe huku inalia mlio km wa cherehani.
Nikaenda kwa fundi akakagua gari akasema service ni ya Overhaul gesket seal zoote na piston Ring. Kwa kuwa ilikuwa ugenini mbali na dar nikamuuliza km naweza tembea nayo nikafanye servic dar akasema ndio ila niwe nahakikisha oil inakuwa level... Nikajaza oil, nikachenj plug zilikua zinamis nikaanza safari ya km 600 non stop......
Nafika nyumban tu taa ya engine kupata joto ikawaka... Nikaenda kwa vitu akasema oil haiusian na nikaipima oil iko sawa haijapangua... Cooling system yoote nikiwa na maana feni, motor, radiator zipo poa ila ukijaza maji ukitembea km 8 tu inachemsha vibaya mno na maji yoote yamekata... Tukahisi ni thermostat ikatolewa lakini shida ndio ile ile hakuna kilichosaidia... (]Msaada wako mkuu)
Kingine, kuhusu izo gasket seal sijui valve na piston ring nimeambiwa ni gharama kubwa sana ni zaid ya laki 3 na kwa engine ndogo kufanya hvyo ni kuipoteza kabisa engine kwan hakuna vifaa original hvyo nimeshauriwa iyo engine niitupe kabisa ili ninunue engine mpa mswaki toka japan iwekwe ambayo pia ni gharama zaidi... Sasa kwa ushauri wako kitaalamu tunafanya vipi hii issue, usawa mgumu gari haitembei na ndio source ya income.
Msaada wakubwa