Niulize chochote kuhusu matangazo ya kulipia Facebook na Instagram

Niulize chochote kuhusu matangazo ya kulipia Facebook na Instagram

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Mimi siyo expert wa kutangaza online kwenye Facebook na Insta lakini nina uzoefu kidogo wa kama miaka miwili hivi kutangaza huko.

So niulize swali lolote kuhusiana na sekta hiyo nami nitakujibu.

Nikishindwa watakuja wataalamu zaidi na mimi nitazidi kujifunza.

Karibuni.
 
Nikitaka kupata followers Instagram kupitia ads inabidi nifanyaje yani mfano kwa siku niwe napata hata followers 50 au 100
Kuna ads za kutaka watu watembelee profile yako. Nadhani zipo na za kucall watu wakufollow. Hizo ndiyo huleta followers wengi. Mapastor wengi wanajitangaza sana kwa style hii😃
 
Hiyo USD nalipia kwa mfumo gani? Na utaratibu ukoje kwa ujumla?
Unalipa kwa visa au mastercard kupitia benki yako. Au hizi virtual cards za kama voda, tigo nk. Ila huwa mara nyingine zinazingua. Ni bora uwe na kadi ya benki.
 
Mimi siyo expert wa kutangaza online kwenye Facebook na Insta lakini nina uzoefu kidogo wa kama miaka miwili hivi kutangaza huko.

So niulize swali lolote kuhusiana na sekta hiyo nami nitakujibu.

Nikishindwa watakuja wataalamu zaidi na mimi nitazidi kujifunza.

Karibuni.
Bandiko nzuri mimi nataka nitume matangazo yangu kwa online je ni sehemu gani rahisi kupata wateja Facebook au Instagram?
Process za kutuma tangazo zipoje?
 
shida naona kama inazinguaga hivi kwenye location unaweza weka dar pekee lakin likaonekana hadi mbeya
Ile ishu ya anuani ya makazi ilitakiwa kusolve kitu kama hiki. Wao sijui walisolve nini!!?. Ila asilimia zaidi ya 90 ya watu utapata ni kutoka Dar. Kama unatangaza ni vyema biashara yako ikawa ya Tz nzima au ya Dar. Mikoani ni wachache sana wako mitandaoni.
 
Monday najilipua $15 kwa siku tatu target ni whatsapp massage

wajuzi wakucheza na algorithm mjee
Uwe unajilipua hivyo tarehe za mwisho wa mwezi. Ndiyo tarehe zinakuwa na biashara sana. Tarehe 21 hadi kuelekea tarehe 5
 
Bandiko nzuri mimi nataka nitume matangazo yangu kwa online je ni sehemu gani rahisi kupata wateja Facebook au Instagram?
Process za kutuma tangazo zipoje?
Kote hakutofautiani sana. Sema facebook unaweza kuweka picha nyingi, kuandika maneno mengi na pia watu hucomment kuliko insta. Ni kama attention span ya watu wa insta ipo chini sana.
Pia watu wazima wengi utawapata facebook na vijana wengi insta.
 
Back
Top Bottom