Niulize chochote kuhusu Nyuki na Asali

Madume hayawezi kutoroka ili yasiuliwe?
🎶Wanaume tumeumbwa , matesooo🎵
Hawa wanawake na majike kweli Ni balaa, Mara watuwekee limbwata tuwe MAZEZETA, Mara na madume ya nyuki yauliwe.....
Ndio maana Mungu anawaadhibu sana wanawake na majike.

Wanawake hawapendi kuchosha Ubongo wao kwa kujisomea au kujiombea AU KUFANYA MAMBO BINAFSI........ndio maana KILA KANISA ZURI YUPOOOO......KILA NABII MZURI YUPOOOO..........KILA MAOMBI ANATAKA AOMBEWE YEYE............

ukiwa kanisani mchungaji akiita watu watoke mbele UNAKUWEPOOOO😂😂😂

Wagonjwa waje niwaombee...........na wewe umoooo.
WAKATI HUNYWI MAJI YAKUTOSHA.
HULALI KWENYE CHANDARUA.
HUMEZI DAWA ZA MINYOO.

*Wenye madeni watoke mbele niwaombee.............na wewe umoooooooooo*
MCHUNGAJI WAKO MWENYEWE KIWANJA CHA KANISA ALIKOPA NA ANALIPA MKOPO KWA WAKATI.
Hata kama wewe ni mdogo wake wa TB JOSHUA kanuni za pesa zinakutaka kulipa deni na sio kumuombea mwenye deni asahau au afe😂

Wanaotaka kufungua biashara watoke mbeleee...........na wewe umooooo.
HUJAWAHI HATA KUUZA GENGE UNATAKA KUFUNGUA SUPER MARKET.
HUJAFANYA HATA RESEARCH YA BIASHARA UNAYOIWEA LAKINI UNATAKA KUWEKEWA MIKONO.

Wenye kutaka safari za nje ya nchi toka mbeleeee........na wewe umoooooo.
PASSPORT YENYEWE HUNA
KIJIJINI KWENU KWENYEWE UNA MIAKA MITANO HUJAENDA KUSALIMIA WAZAZI lakini unataka kwenda Ulaya😂

*Wanaoteseka kwenye ndoa watoke mbeleee..........na wewe umoooo.
KISIRANI HUONGEI NA MUMEO VIZURI.
SIO MSAFI
HUMPIKII MUMEO JAPO KWA WIKI MARA MOJA.
HUJUAGI HATA KAMA BOXER ZAKE ZIMETOBOKA.
HUJUI HATA MUMEO LEO KAMA AMEBEBA KITAMBAA CHA KUJIFUTIA lakini bado unataka kuombea

Wanaotafuta kazi watoke mbele niwaombee..........na wewe umoooo.
HUJAWAHI HATA KUANDIKA MAOMBI YA KAZI.
HUNA HATA MPANGO WA KUJIAJIRI KWA ELIMU YAKO....
HUWEZI HATA KUJITOLEA KUFANYA KAZI BILA MALIPO....
HUJAWAHI HATA KUTEMBEA KWENYE MAOFISI MATANO UKAPAELEKA BARUA ZAKO kutwa uko kanisani unaombewa yaani upate kazi kwahiyo unataka kazi ikufuate hapo kanisani?

Wanaoota Ndoto mbaya usiku watoke mbele niwaombee........... na wewe umoooooooo.
KUTWA UMESHINDA NA KISIRANI....
KUTWA UNA HOFU YA KUSHINDWA.
KUTWA NZIMA UNAWAZA MAMBO MABAYA sasa unataka usiku ukiingia uote nini?
Uko mbinguni na malaika?
Wakati siku nzima ulikuwa na maushetani tuu

Wanaotaka viwanja vya kujenga aaa............na wewe umooooooo.
CHUMBA ULICHONACHO TUU HUKIPENDI HUWEZI HATA KUPAKA RANGI.
HUWEZI HATA KUPANDA MAUA ENEO LAKO....
HUWEZI HATA KUPAFAGIA PAKAELEWEKA.....je hiyo nyumba utaifanyaje?

*Wanaotaka magari watoke mbele niwaombeeeee.........na wewe umooooo.....*.
HUJACHUKUA JAPO HATUA YA KUSOMEA UDEREVA.
HUJAWAHI HATA SIKU MOJA KWENDA PALE SHOWROOM UKAULIZIA JAPO BEI.
HUJAWAHI HATA KWENDA GARAGE UKIDADISI MAFUNDI NA KUJUA CHANGAMOTO ZA WENYE MAGARI...ila unataka gari sasa ata ukilipata si utaliuza tuu mwanamke?

Waliiomba mkopo ukagoma watoke mbele niwaombee.........na wewe umooooooo.
UNA MADENI KILA KONA NA YOTE UNASUMBUA KUWALIPA WENYEWE BADO UNATOKA KWENDA MBELE KUOMBEA ILI UPATE MKOPO MPYA.asante Mungu siku hizi mabenk wanashirikiana ukidanganya tuu imekula kwako.

Wanaotaka watoto wao wafauluuuu..........na wewe umooooooo.
HUNA MUDA WA KUHIMIZA WATOTO KUWA NA BIDII YA MASOMO
HUJAWAHI HATA KUFUATILIA HOMEWORK ZAO.
HUJUI HATA JINA LA MWALIMU WAKE WA DARASA JAPO AKUJUZE MWANAO ANAVYOENDELEA.
HATA SOMO ALILOFELI HUJUI NI KWANINI lakini uko mbele kuombewa ili wanao wafaulu mweeeeeeeeee.......😂

Wanaosumbuliwa na wasichana wa kaziiii...............na wewe umoooooooo.
KWANZA MSHAHARA WAKE HUJAMPA MPK LEO eti unamtunzia?
Kwanini usimfungulie akaunti ya benk kama ni kweli ?
AKIVUNJA VYOMBO UNAMKATA.
CHAKULA UNAMBAGUA.
DADA WA KAZI HUMPI MUDA WA KUTOKA NA YEYE AKAPUMZIKE.
KUTWA UNAWAZA ATATEMBEA NA MUMEO.
AKIKOSEA UNAFOKA ASUBUHI MPK JION NA KUMPIGA JUU.
MKIMALIZA KULA NDIO DADA WA KAZI ANAKULA KILICHOBAKI.
WATOTO WAKO HUTAKI WAMSAIDIE KAZI MDADA KWAKUWA ETI ANALIPWA MSHAHARA.
DADA ANAKULELEA WATOTO WAKO LAKINI UNAMTUKANA MATUSI MAKUBWAA.
UKIRUDI HUWEZI HATA KUMLETEA ZAWADI DADA ANAYEKUCHUNGIA NYUMBA.....kisha umenyoosha mikono pale mbele eti wadada wa kazi wanakusumbua

*Waliotupiwa mikosiiii na kulogwa watoke mbele niwaombeeeeee.............na wewe umoooooo.*
KUTWA UNAWAOMBEA WENZIO WAPATWE NA MABAYA.
KILA MAMA NANII AKIFANIKIWA WEWE UNAUMIA.
HUWEZI HATA KUMSHAURI MWANAMKE MWENZAKO JAMBO LA MAENDELEO ETI ASIJE KUKUPITA.
MWINGINE AKIPENDEZA HUWEZI HATA KUMWAMBIA KUWA KAPENDEZA.

*Wanaotaka wanaume zao wasiwasumbueeee..............na wewe umooooooo.*
WEWE MWENYEWE MSUMBUFU TANGU JANUARY MPK DECEMBER BADO UNATAKA MWANAUME ASIKUSUMBUE.?

JIULIZE UPO HAPA DUNIANI UNAFANYA NINI KAMA KILA KITU MTU MWINGINE ATAKUFANYIA?

MUNGU AMEKUPA AKILI ILI YALIYO NDANI YA UWEZO WAKO UYAFANYE NA YALE YALIYO NJE YAKO UMWAMBIE MUNGU AKUSAIDIE.

TUWAPUNGUZIE WATUMISHI WA MUNGU MIZIGO JAMANI NA WAO NI BINADAMU
 
Mimi ni mtaalamu katika sekta ya ufugaji nyuki, kama kuna kitu unahitaji kujua kuhusu Nyuki na Asali niulize nitajibu kadri ya uelewa wangu. Karibuni. "Without bees man will have only 4 years to live on earth" Albert Einstein!
Nani anayewagawia na kuwapangia kazi nyuki wakiwa mzingani?
 
Jibu safi.
Kumbe ndio maana nilipata kusikia asali ya Zanzibar Ina ladha ya karafuu na Ni ghali. Kwa hiyo inawezekana kufuga nyuki karibu na shamba la vanilla ili kupata asali yenye ladha ya vanilla??
 
Sawa mkuu!
 
namna gani ya uhakika kutofautisha asali mbichi na asali ya kuchemsha? naskia kuna hadi asali yenye sukari guru.
Kwa kuangalia hutaweza, labda kama utainusa na kupata harufu ya moshi. Lkn kwenye vipimo unaweza kujua kwa kupima chemical inaitwa hydromethyl furfural (HMF) ambayo inaongezeka kwenye Asali kadri inavyopata joto, na hivyo kuharibu ubora
 
1. Kwanini ukipaliwa na asali unakufa?
2.inasemekana ukila matango na ukanywa asali unakufa...je Kuna ukweli wowote mkuu?
Kupaliwa ni tatizo sio kwa asali tu, hata wali unaweza kukuua ukipaliwa nao.
Hili la tango na Asali hata mimi nimekuwa nikilisikia since I was a little boy, lkn hakuna aliyethibitisha. No one wants to try it and prove![emoji23][emoji23]
 
Mkuu utajuaje kama hii asali nzuri? Huku mitaani wengi wao wanauza asali feki imejaa sukari guru
Kuna njia nyingi sana za kugundua Asali bora na iliyochakachuliwa
 
Wanaweza kuwa ni wale wale au wengine.
 
Hii ni kweli, hakuna mahali nimepinga.
 
Jibu safi.
Kumbe ndio maana nilipata kusikia asali ya Zanzibar Ina ladha ya karafuu na Ni ghali. Kwa hiyo inawezekana kufuga nyuki karibu na shamba la vanilla ili kupata asali yenye ladha ya vanilla??
Ndio. Lakini mind you, sio kila mmea nyuki wanachukua Nectar. Kama Vanilla inatoa Nectar ambayo nyuki wanachukua unaweza kupata Asali yenye Harufu au ladha ya vanilla
 
Nyuki anaweza kutoka katika mzinga mmoja na kuhamia mwingine ambao kuna nyuki wengine?
 
Kwenye mzinga wa nyuki kunakuwa na malkia wa ngp?
Na kwann nyuki dume akifanya mapenzi anakufa?
Lakini malkia anaishi?
 
Kwenye mzinga wa nyuki kunakuwa na malkia wa ngp?
Na kwann nyuki dume akifanya mapenzi anakufa?
Lakini malkia anaishi?
Haya maswali yote ameshayajibu
Malkia anakuwa ni mmoja.
Nyuki madume hayafi yakifanya mapenzi bali yanauawa na nyuki workers baada ya asali kumalizika kutengenezwa.
Malkia anakufa iwapo akipandwa na madume wakati ashamaliza kuzaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…