Niulize chochote kuhusu Nyuki na Asali

Niulize chochote kuhusu Nyuki na Asali

Namna gani ya uhakika kutofautisha asali mbichi na asali ya kuchemsha? naskia kuna hadi asali yenye sukari guru.
 
Mtaalamu Mimi nauliza kama kuna ukweli kwamba kung'atwa na nyuki ni dawa ya mishipa,pia kwanini wengine waking'atwa huvimba wengine hawavimbi,je malkia ana paa au hubebwa kama nadharia nyingi zinavyosemwa
Kuna hiyo nadharia kuwa bee venom ni dawa, lkn utafiti unahitajika hapa.
Kuhusu kuvimba, kila mtu ana react tofauti na bee venom, wapo ambao hata akidungwa mkononi na nyuki mmoja tu, anavimba mwili mzima, lkn wengine hata adungwe na nyuki 30, havimbi sana.
 
Ukifuga nyuki karibu na makaazi ya watu, au kwenye makaazi ya watu, haitawezekana kwa nyuki kutengeneza asali hata kama kuna maji na maua ya kutosha?
Nyuki wanatengeneza Asali popote. Suala la makazi ya watu ni suala la usalama tu na kuepuka contamination hasa km kuna kilimo cha kutumia dawa
 
Kuna uvumi ushawahi kuwepo kwamba asali ukiitumia mda mrefu inafanya mifupa iwe milaini, ni kweli?
 
Muwe mnasoma mbona mtaalamu kaeleza nyuki wanaenda kuchota maji mtoni halafu wanakimbia haraka nyumbani kwao kutakausha watu wengine mnavichwa vigumu kweli kuelewa
Acha tabia ya kuvamia maswali!
 
1. Kwanini ukipaliwa na asali unakufa?
2.inasemekana ukila matango na ukanywa asali unakufa...je Kuna ukweli wowote mkuu?
 
Mkuu utajuaje kama hii asali nzuri? Huku mitaani wengi wao wanauza asali feki imejaa sukari guru
 
Nyuki wanatengeneza Asali popote. Suala la makazi ya watu ni suala la usalama tu na kuepuka contamination hasa km kuna kilimo cha kutumia dawa
Kwa mfano, nyuki wameweka makazi katika nyumba; ukiwafukuza (kwa njia yoyote ile) watatoka na kupotea kabisa. Lakini baada ya miezi kadhaa kupita, utashangaa wamerudi tena eneo hilo hilo.
1. Je, nyuki hao wanaorudi, wanakuwa ni wale wale waliotimuliwa hapo awali? Kama ni ndiyo hao hao, swali la pili..
2. Kipi kinawafanya warudi tena ktkt makazi ambayo walitimuluwa hapo awali?
 
Mleta mada refer post #50 kuna technology ya kuzalisha malkia wa nyuki inasemekana worker yeyote anaweza kua malkia akipewa chakula/asali anayokula malkia ( chakula ya malkia ni tofaut na cha nyuki wengine) hivyo bas akipewa atakua mkubwa zaid na kua na uwezo wa ki malkia
 
Naendelea kusoma maswali na majibu.. ahsante mleta Uzi
 
Back
Top Bottom