Niulize chochote kuhusu siri ya kuwa tajiri

Niulize chochote kuhusu siri ya kuwa tajiri

Swali nzuri?

1, mimi nina ng'ombe 16 pamoja na mbuzi 20
pia ninafunga kuku wakienyeji na nimeweka mkatamba na mfanya biashara mmoja kila baada ya miezi miwili anakuja kununua kuku na mbuzi

2, nina mashamba ya kilimo pamoja na bunga heka 90.
kijijini

3, nina duka la ushonaji nguo za kina baba na kina mama pia nimeajili watu.

4,nina piki piki mbili ambazo pia nimeajiri vijana.

5, nafanya biashara ya kuwanunulia wakulima wezangu mpunga pamoja na mazao mengine.

6, nina majembe matatu ya kukotwa na ng'ombe, ambayo ikifika wakati wa masika nafanya biashara ya kuwalimia amba hawana ng'ombe


Hongera sana ukitokea ukame kwa miaka saba utafanya nini?
 
hahahahahaaaaaaaaaaaaaaaaa oky bestito
ngoja nikuache tu mana naona unanifurahisha
Hiini post ya 30+... Sijaona strong content kutoka kwa mleta mada..

Kaulizwa maswali mboga kabisa ya kuvutia marks lakini kajibu garbage tu!

He is not serious!

Hivi mtu akikuuliza tajiri ni nani utajibuje?

Hilo swali siyo rahisi kujibika japo ni rahisi kusomeka!
 
Utajiri
Kipato = Matumizi + Akiba

Kama hio equation itabalance basi wewe ni tajiri..., mtu ambaye kipato chake kinamtimizia matumizi yake yote bila kujibana na anabakiza akiba basi yeye ni tajiri..

Mtu mwenye kipato cha milioni kumi kwa mwezi lakini matumizi yake ni milioni ishirini kutona na watoto na wanaomtegemea lukuki sio tajiri Ingawa mtu mwenye kipato chake milioni moja ila matumizi yake ni laki nane ni Tajiri, kumbuka hapa siongelei bahiri
 
Mimi siyo tajiri ila nina malengo yakuwa tajiri namuomba mungu anijalie uzima.

Kubali kuwa wewe ni tajiri na ndo maana sote tuko hapa kwenye hii mada tunajadiri na kuelimishana, utajiri sio mali tu unazoweza ziona ama kuzigusa bali kuna aina nyingine ya utajiri ambayo naweza kuita UELEVU, mala nyingi nivigumu sana mtu kuwa tajiri kama ana uelevu mdogo, kuna jamaa humu janvini ametoa wazo kuwa kila mtu anayeweza kusoma agalau asome vitabu 100 kwa mwaka, ila cha ajabu wengi wetu tumemtusi na kusema hilo ni kupoteza muda/wakati, bila kujua kuwa kwa kusoma hivyo vitabu 100 kwa mwaka ukiweza itakuletea kupanua ulevu wako na kukuwezesha/kukulahishia kuwa tajiri

Take it or lieve it this is my opinion
 
This guy is a dreamer.
Unajua tatizo ametoka kwenye umaskini sana kiasi ambacho hapo alipo anahisi atakua tajiri. Well, simkatishi tamaa na inawezekana kabisa atakuja kujiweza. Lakini atambue kuwa utajiri ni kitu "relative" kwa kiswahili sifahamu neno lake. Ila ni kwamba kwake anachokiona utajiri wengine ndio mwanzo wao.

Wewe Shy land nyumba 3 viwanja 5 ngombe 20 magari 7 unaweza ona UTAJIRI lakini kuna watu wanavyokua na akili timamu za kuanza maisha wana vyote hivyo au thamani ya zaidi ya hapo na hawajioni matajiri!

Hivyo basi, usiseme una siri ya utajiri, utajiri wako wewe unaweza kuwa umaskini wangu mimi. Wewe sema unatoa ushauri wa mbinu za kujikwamua kiuchumi. Utajiri sio kitu easily definable. Ndio maana wengi wanakuuliza na unashindwa kujibu vizuri!
 
Last edited by a moderator:
Ikumbukwe kutokuwa tajiri hakumfanyi mtu asfundishe watu kuwa matajiri.kuna watu wamejaaliwa talanta ya kuona njia za utajiri lakini wao wamekosa karama ya UDHUBUTU.Kwa hiyo mtu mwenye karama ya udhubutu akifundishwa njia za utajiri atapaa kumuacha mwalimu wake.


take it from me
 
Ukitaka kuwa tajiri bongo fungua gesti hausi
 
Ndgu wana jf sijaandika huu uzi kwa kujindai kwamba eti mimi ninajua sana kuhusu siri ya utajiri

lengo langu kuu nikuweza kujadili hili somo ambalo limekuwa adimu sana kulipata darasani.
kwa hiyo tukikusanya mawazo yetu wote tunaweza kupata siri zito kuhusu utajiri.

siyo kwamba ninachokujua mimi unakijua na wewe
na
unachokijua wewe mimi pia sikijui. karibu sana kwa mjadala wakuu.
 
Mtoa mada kajifunze kiswahili kwanza ndio urudi.. Humu JF hakuna watoto wenzako. Unaulizwa maswali unaleta kejeli, alafu mtu upo ndotoni unataka utufundishe nini??

Kuna vitabu vinaandikwa na watu matajiri kama kina Donald Trump na Kayosaki hivyo ndivyo vinafundisha jinsi ya kufikia malengo yako..
 
Mtoa mada kajifunze kiswahili kwanza ndio urudi.. Humu JF hakuna watoto wenzako. Unaulizwa maswali unaleta kejeli, alafu mtu upo ndotoni unataka utufundishe nini??

Kuna vitabu vinaandikwa na watu matajiri kama kina Donald Trump na Kayosaki hivyo ndivyo vinafundisha jinsi ya kufikia malengo yako..

Asante sana kwa ushauri wako mkuu. wazo lako nitalifanyia kazi,
lakn sidhani kama kiswahili kitanisaidia lolote sababu sina malengo ya kuwa mwandishi.
 
Mtoa mada fikra zako zimefifishwa na mazingira yaliyokuzunguka, umechanganya sifa za anaejimudu maisha unampa tajiri, kwa ufupi tu, tajiri ni mtu aliyewekeza na kumpatia mapato ya muda mrefu, hata kama akifa au kupoteza uwezo wa kutafuta bado mapato yataendelea kutiririka. sio ukifa na mali chali,kwa sasa ulipofikia ni adimu kutimiza labda kwa vilembwe na vitukuu vyako.
 
we binti si ndo ulikuwa unamvua nguo kaka yako kwenye uzi wako wa juzi!?leo elimu ya utajiri umeitoa wapi?
 
Back
Top Bottom