Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg

Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Seapiano yangu imezima ghafla, kwanza ilianza kuua flash ninazotumiaa kuweka nyimbo, pili ikazima mwanga kwenye display ila ile inayozunguka spika ikawa inawaka, ikawa inapiga then inajizima yenyewe ila mwanga wa blue kwenye spika bado upo ni kama mtu aliyezimaa na remote.
Ikaja ikazimaa ghfla mpaka leo, nmepeleka kwa fundi, power surply ipo fresh ila tatizo sijajua ni nn maanaa fundi imehangaikaa nayo ikaimba then ikawa inaimba na kuzima kama awali, mpaka sasa fundi hajaipatia ufumbuzi, naombeni msaada nini kifanyike.
 
Mziki poa weka geto kama ndo budget yako imefikiapo, ila kama pesa ipo vuta JBL ya watts 300 or 510wt

Natamani niuze sony 600wt HT ya soundbar 5.1

Jbl parefu mkuu huko maji marefu[emoji1] acha nipambane nichukue hyo tu kwa sasa,maana naona sabufa nayotumia inanipigia kelele tu[emoji23]
 
Seapiano yangu imezima ghafla, kwanza ilianza kuua flash ninazotumiaa kuweka nyimbo, pili ikazima mwanga kwenye display ila ile inayozunguka spika ikawa inawaka, ikawa inapiga then inajizima yenyewe ila mwanga wa blue kwenye spika bado upo ni kama mtu aliyezimaa na remote.
Ikaja ikazimaa ghfla mpaka leo, nmepeleka kwa fundi, power surply ipo fresh ila tatizo sijajua ni nn maanaa fundi imehangaikaa nayo ikaimba then ikawa inaimba na kuzima kama awali, mpaka sasa fundi hajaipatia ufumbuzi, naombeni msaada nini kifanyike.

App ya jf haileti notifications...hivyo sioni details kwa wakati.....

Pole mkuu
Power supply ina shida!!!!!
Bila shaka hi subwoofer ni hizi New Model
Power supply yake ina output 2
IMG_7572.jpg

[emoji1369] ni card yake sio?

Output moja ya transfom inaendesha amplifier yaan sauti.... nyingine ina endesha display ,na mfumo wa frash
Hivyo kama inashida upande ule mwingine matokeo yake ndio hayo inazima mziki ila display inawaka

Aweke power nyingine kwanza aone
 
Kwema wakuu? Nina soundbar ya Sony HT RT-40 nilikua nimeunganisha na TV kwa kutumia optical cable na HDMI. Sasa siku moja nikaona optical cable imechomoka kwenye soundbar, imening'inia inawaka mwanga mwekundu.

Kila nikijaribu kurudishia kwenye port yake unaanguka.. yaani haukazi.
Nikasema nichomoe na kwenye tv.. hapo pia ikashindikana kurudisha. So nahisi port zile zimeharibika.

Swali langu ni, je inawezekana kutengenezeka? Na je kati na optical cable na Bluetooth connection ipi ipo vizuri kwenye kupata rich sound features.
 
Kwema mkuu....
Ule mwanga mwekundu ndio.... signals zenyewe mkuu....i

Mkuu kutengenezek inawezekana ila fundi atakae tengenezea!
Kuna mambo ni rahisi sana
Tatizo mafundi wengi wanatumia experiences tu ...mwisho wa siku ataiharibu zaidi
Maoni yangu n bora ukaitumia hivyo hivyo ikiwa haikunyimi uhondo...au kama kqmq inq namna nyingine ya kupata kilichokosekana

Kati ya optical cable na Bluetooth....
Kwanza kitu chochote ambacho ni wireless kuki pair na wired ni makosa
Still optical cable is the best one....
 
Kwema wakuu? Nina soundbar ya Sony HT RT-40 nilikua nimeunganisha na TV kwa kutumia optical cable na HDMI. Sasa siku moja nikaona optical cable imechomoka kwenye soundbar, imening'inia inawaka mwanga mwekundu.

Kila nikijaribu kurudishia kwenye port yake unaanguka.. yaani haukazi.
Nikasema nichomoe na kwenye tv.. hapo pia ikashindikana kurudisha. So nahisi port zile zimeharibika.

Swali langu ni, je inawezekana kutengenezeka? Na je kati na optical cable na Bluetooth connection ipi ipo vizuri kwenye kupata rich sound features.

Kwa quality ya sound tumia hdmi arc hii ndio njia bora kwa sasa kwa kusafirisha sauti zaidi ya hyo optical na bluetooth
Cha muhimu hapo nikuangalia kama tv yako ina hyo port ya hdmi arc
 
Back
Top Bottom