Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg

Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Mkuu hivi zile safuba za boss BS 1871-2L zinakuwa na surrounding speakers 5 ndo zikoje yan kwenye mambo ya RMS hebu nisaidie shule kidogo[emoji120]

Kaka hiyo redio sijaishika,wala kuitumia,wala kuisikia ikiongea

Ningeijua ngeiangalia kujua circuit system yake ni aina gani
Ningejua kama circuit yake ni sms au analog
Hivyo inaweza niwia vigumu kukujibu kwasababu SIIJUI

Ningeiona tu upande wa nyuma wa redio ningejua system yake ikoje
Au watengenezaji wangeiweka mtandaoni (ki maelezo)
 
Wakuu vitu kama hivi hapa kwa Samia vinapatikana wapiView attachment 2519291
Kenya hapo wana used na mpya nyingi sana kama hizo. Ukitaka kuagiza na kama mfuko unaruhusu unajichagulia kitu unatulia.

Zanzibar waweza pata ila kwa tabu kiasi, uwajue wauzaji na wakipata mzigo wakupe taarifa.

Kuna wanaopenda musics sana, badala ya home theatre wanaweza opt kwenda kwenye separates. Unakuwa na preamp, power amplifier, two decent speakers na source ya maana ya kuchezea mafaili yako.

Imagine kuna power amplifier ziko stable at 2.7 Ohms with no strains or distortions.. Kitu ambacho music systems nyingi ni changamoto kuweza afford.

Kuna wakati naamini kupenda musics and good sounds sio tu hobby bali ni kitu kinatoka ndani. Ndo maana kuna watu wanatumia muda na hela kupata vitu vizuri, either customs made au factory made.

Sent from my SM-N916S using JamiiForums mobile app
 
[emoji1374][emoji1374][emoji1374] Ahsante mkuu
Hizi line za mwisho umenyoosha sana...
Music ni kitu chakukipenda kutoka ndani..
Nb ukitaka kitu kizuri basi jua ghalama zinaongezeka
Usifunge wallet
 
Nimesoma sehemu kuna Mtu kaandika ukibadili Mfumo huu Umeme itakuwa inakula Unit 3 per day… Je hili Lina ukweli?

Ulaji wa umeme unategemea na vifaa vyako vya ndani
Inawezekana fridge ikatumia umeme mchache kuliko taa tu
Watts ndio jambo kubwa kuliko kitu chochote

Sasa mkuu umeweka pioneer yenye watts 10000+
Bado na spik zingine
Jumla unakua kama na watts 1500! Unadhan utakula sawa na subwoofer yenye watts 40? Jibu ni Hapana

Nmewah kufanya majaribio kidogo
bass speaker yangu
Jbl 12 “ nkipiga hi bass umeme unaenda kuliko
Nkipiga midbass pekee
 
Kaka hiyo redio sijaishika,wala kuitumia,wala kuisikia ikiongea

Ningeijua ngeiangalia kujua circuit system yake ni aina gani
Ningejua kama circuit yake ni sms au analog
Hivyo inaweza niwia vigumu kukujibu kwasababu SIIJUI

Ningeiona tu upande wa nyuma wa redio ningejua system yake ikoje
Au watengenezaji wangeiweka mtandaoni (ki maelezo)
Hiyo hapo mzee wangu [emoji120]
IMG_20230217_182205_053.jpg
 
Back
Top Bottom