Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg


Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Kwanini haya makitu baada ya mda flani yanakoroma?
Mkuu uliwahi ipeleka kwa fundi yoyote? Kama ndio Basi ikiwa ilibadilishiwa ic Basi fundi hakuikaza vizur kwahyo ikipiga kwa muda ic inachemka haipotezi joto kwenye heat sink inaanza kukoroma.

Pia inaweza kua components zimelegea,itabidi kufanya soldering upya
Au speaker inashida
 
1. Nini maana ya 2.1 au 5.1 kwenye "SABUFA" aka Sub Woofer? Je kuna 3.1,4.1 ,1.1? Kama hakuna why? .1 ni nini kwanini isi .2?
2. Kama kuna "SABUFA" basi kutakuwa na "BUFA" aka WOOFER ,nini tofauti ya Sub woofer na Woofer?
2.1,5.1, hi inasimama ki technical kuelezea Aina ya music system yako
Ikiwa music system itaandikwa 2.0 maana yake hiyo Ni music system ya stereo yaani itakua na speaker mbili sawa
Ambazo speaker hizo zitadunda zitaimba hizo hizo
Ni music system ambayo inakupa Radha kamili ya muziki Ila ukiona 2.1 maana yake hiyo namba ya mbele inasimama baada ya channel (R,L)number Kisha hiyo ya nyuma Ni subwoofer yake(inayotoa low frequency yaani mdundo)

Kwahyo 5.1 maana yake inakupa tweeter 5 na bass moja. Ndio mkuu zipo 3.1 4.1 kitu Ni kile kile
Nkukumbushe tu kua channel za music ziko mbili tu R,L Channel zingine zinanyumbulishwa kutoka hapo hapo mfano
FL
FR
C
Na bass
Utofauti Kati ya subwoofer na woofer Ni ndogo Sana
Subwoofer Ni speaker ya woofer iliyopo kwenye box kabisa
Mfano wenye home theater Ile inayotoa mdundo ndio subwoofer
Ila woofer Ni speaker iliyotengenezwa kucheza low frequency kifupi Ni speaker ya bass
 
Subwoofer yangu spika moja hailii niki interchange upande mwingine inalia tatizo ni nini kwanini zisilie zote kwa wakati mmoja
Channel moja haifanyi kazi
Sababu inaweza kua driver ic ya hyo njia imeungua
Au waya wa signal wa njia moja umekatika au umelegea sehemu
Chakufanya itabidi uifungue uachalie signal Kama ipo kwenye ic husika,
Kama haipo ic inashida
Kama ipo Basi signal haziingii
 
Channel moja haifanyi kazi
Sababu inaweza kua driver ic ya hyo njia imeungua
Au waya wa signal wa njia moja umekatika au umelegea sehemu
Chakufanya itabidi uifungue uachalie signal Kama ipo kwenye ic husika,
Kama haipo ic inashida
Kama ipo Basi signal haziingii
Ni mpya kabisa
 
Kati ya sea piano,kodtec na aborder,ipi ni subwoofer nzuri na imara?
Mkuu leo hi unaweza kwenda China company yoyote ya electronics uka order mzigo mfano subwoofer 10000000 ukasema ziiye Teamanaconda wakaandika hivyohivyo ikiwa utaingia nao ubia.

Ndivyo ilivyo sea piano, codject na aborder Tena Kama hizo aborder nadhan tajiri wake Ni wasongea niliwah sikia ,ndio maana Zina maandishi yakiswahili. Kwahyo issue sio jina issue company inayotengeneza.

Aborder kiwanda chake sijakizingatia japo transformer zake Zina current nyingi,na circuit zake mpangilio Ni F
Sea piano fresh Ila ukipata old model. Ni nadra kukuta subwoofer imeandikwa Samsung au sonny
Ukiipata hyo usidhanie itakua 200000
Kuna mzee iringa anayo Samsung
Alinunua nje uko
 
Kwanini wachina wenyewe hawatumii hayo masabufa
Wanatumia.ila sio kwa kiasi chetu.
Nkupe mfano tu kunamzee anayo sonny Kama hiyo pichani Ni ndogo hata haya ma seapiano makubwa.ila aliagiza kwa pesa ndefu tu kwahyo sisi wa Hari ya mtu ndio hivyo tunashikana na 270 hivi

Lakini pia watu wanao nunua music system wapo Aina yatu
1
2
3....
Screenshot_20200907-175519.jpg
 
Back
Top Bottom