Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg


Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Mkuu vuta pumzi kisha soma taratibu....
Ntajibu swali moja baada ya lingine!
1
Operation amplifier au op amp na amplify ni kitu kimoja...zote zinaongeza nguvu ya sauti
Ila zinatofautiana output power
Opamp inapokea signal kutoka kwenye MP3 players,dvd players, au laptop itaongezea nguvu ya signal kabla yakuiingiza kwenye amplify.....
Alafu amplifier itaongeza nguvu ya nguvu ndogo iliyotoka kwenye opamp
Twende kwenye mfano
2.1 multimedia systems ambayo ndio hizi zinafahamika km subwoofer ile speaker ya bass hua inadunda tu alafu zile tweeter zinaimba sauti nyembamba sio!?
Lakini amplifier za ndani zote ni sawa
I mean channel ya bass na ya tweeter zote hutumia ic au transistors sawasawa
Kwahyo ni sawa na kusema amplifier inayosukuma ile bass inaweza sukuma tweeter zile pia
Ki kawaida amplifier yenyewe inakuza nguv ya sauti tu
Ila hizo sauti zinatofautiana frequency (usikivu)
Ile signal inayodunda tunaita low
Ila tweeter tunaita high
Lakini kumbuka kua hiz pc zinatoa stereo
I mean sio low wala high
Zikiingia ndani ndio zinakutana na opamp ambayo itaziongeza nguvu kwanza( kwasababu ni amplifier pia) kisha zitafanyiwa kitu kinaitwa filters Yaan kutengeneza hizo frequency sasa!
Hivyo output signal ya opamp inategemeana na aina ya opamp nikisema aina nnamaanisha inategemeana na filters walivyoitengeneza itoe aina fulani ya mziki
Alafu hizo output signal ndio zitaingia kwenye amplify


Zile power amplifier kubwa mfano wa hi apa chiniView attachment 2076071

Unajua kwanin haina vidude vingi vyaku tune saut zaid ya hivyo viwili( hivyo viwili havi tune mziki zaid vinaongeza na kupunguza SAUTI TU!)
Kwasababu hi ni amplifier tu haina opamp yeyote
Zile crossover , equalizer, zote ni opamp kwasababu zina tune signal kusikika tofauti tofauti lakin pia hizo zote zina amplify signal lakin kwa kiwango kidogo sana kias kua ili usikie unahitaj amplifier [emoji28][emoji28] yan sijui umepata picha?
!!!View attachment 2076084
Hi pia ni amplifier vilevile ila hi ina opamp!
Just understand
Angalia ina sehemu ya kuchomeka frash apo
Inamaana hiyo MP3 players ikitoa mzik itapeleka kwenye opamp ampapo utatune sound kama unavyoona hapo Alafu signal ndio zitaenda kweny amplify
Mkuu umepata mwanga?
Nimekusoma vema sana kuhusu tofauti na uhusiano kikazi kati ya opamp na amplifier, big up sana!
 
Swal la3 sijalisoma vizuri...unamaana gani? Kipi kinafanya saut ya amplifier (power) kuwa kubwa au ndogo au
Vitu gani vinafanya sauti kua kubwa au kipi mkubwa
Hili swali la tatu labda niliweke namna hii;
Mfano unapoongeza sauti au kupunguza sauti katika music system ni components gani hasa inahusika? Ni capacitors au ic?
 
Hili swali la tatu labda niliweke namna hii;
Mfano unapoongeza sauti au kupunguza sauti katika music system ni components gani hasa inahusika? Ni capacitors au ic?

Kinaitwa potentiometer kitaalamu
IMG_6294.jpg

Wengine wanaita volume
Hichi ndio kinatumika kuongeza na kupunguza sauti
Kinapokea signal kutoka kwenye mp3 player mfano alafu kina ruhusu iende kwenye amp
Je ulitak hivi au swal lako sijalielewa? Km n hiv basi nmby nielezee zaidi
 
Kinaitwa potentiometer kitaalamuView attachment 2076367
Wengine wanaita volume
Hichi ndio kinatumika kuongeza na kupunguza sauti
Kinapokea signal kutoka kwenye mp3 player mfano alafu kina ruhusu iende kwenye amp
Je ulitak hivi au swal lako sijalielewa? Km n hiv basi nmby nielezee zaidi
Dah uko deep! Nazidi kupata mwanga ila nitarudi kuelezea mazingira mazima ya tatizo lililonikuta mpaka kutaka kuyajua yote haya, issue nyingi napenda kujifunza na kusolve mwenyewe, hii potentionmeter sikua naijua kabla, nitai google kuielewa zaidi inavyofanya kazi, shukrani sana engineer!
 
Dah uko deep! Nazidi kupata mwanga ila nitarudi kuelezea mazingira mazima ya tatizo lililonikuta mpaka kutaka kuyajua yote haya, issue nyingi napenda kujifunza na kusolve mwenyewe, hii potentionmeter sikua naijua kabla, nitai google kuielewa zaidi inavyofanya kazi, shukrani sana engineer!
Na mm ningeoenda kuju kwamba pale unapoongeza sauti hicho kifaaa huwa kinapunguza volt ndo saut inapungua ama ni nn

Sent from my YAL-L21 using JamiiForums mobile app
 
Dah uko deep! Nazidi kupata mwanga ila nitarudi kuelezea mazingira mazima ya tatizo lililonikuta mpaka kutaka kuyajua yote haya, issue nyingi napenda kujifunza na kusolve mwenyewe, hii potentionmeter sikua naijua kabla, nitai google kuielewa zaidi inavyofanya kazi, shukrani sana engineer!

Yess hiyo n variable resistor...
Ukikwama popote naomba niambie ntakupa mwendelezo
Nipo
 
Na mm ningeoenda kuju kwamba pale unapoongeza sauti hicho kifaaa huwa kinapunguza volt ndo saut inapungua ama ni nn

Sent from my YAL-L21 using JamiiForums mobile app

Mkuu Hongera kwa kufikilia....
Lakini volts hazihusiki hapa
Pale ile sehemu unayochomeka flash kwenye subwoofer ndio chanzo kikuu cha mziki kwenye subwoofer
Ila mzik unaotoka pale hua n mdogo sana ndio maana unaenda kwenye amplifier ili usikike mkubwa kama ambavyo hua unasikia unadundaa[emoji23][emoji23]
Lakini kabla haujaenda kwenye amplifier ndio zinapita kwenye hizo potentiometer sasa kwahyo volts hazihusiki apo ni sauti tu
Hiyo nob ina pin 3
IMG_6295.jpg

Rejea picha hapo juu
Pin ya katikati ndio output signa
Kisha moja ni inpt n nyingine ni ground
IMG_6294.jpg

Hi yenye pin nyingi isikuchanganye
Hiyo n sawa na potentiometer 4 kwenye moja!
Muhimu kujua unataka kufanya nini
 
Back
Top Bottom