Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg


Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Kwanini Subwoofer nyingi zinatumia Ic ya 2003/2005/2030/2040/2050 badala ya Transistors?
Mkuu matakwa ya watengenezaji tu wakilenga zaidi soko lake.

Mchina hawezi akakuekea power transistor alafu akupe na 8ohm speaker hyo Ni never. Mala nyingi mchina hutumia vitu easy Ila vyenye matokeo makubwa.

Mfano anakupa tda 2050 Kisha anakupa na volts 18-+ na 8ohms
Apo subwoofer yako inakua inacheza at the peak kabisa ikiwa speaker itazingua tu unapata mosh kwenye ic kwahyo anafanya hivyo ili isiwe Bei juu kwenye manufacturer ili alinganishe Bei na kwa mtumiaji
Mbona powerful zipo Ila Bei yake so unaijua?
 
1. Kwanini Subwoofer zote zinatumia dual power?

2. Nini tofauti ya Subwoofer kutumia dual power na push pull amplifier?

3. We umesomea wapi? Na level yako ni ipi kwenye electronics?
Honestly kuhusu push power sina uelewa nayo kiwango chake
Ila amplifier ikitumia dual power supply inakua powered kuliko inayotumia supply yakawaida kwasababu speaker inakua inavuta both side
 
1. Kwanini Subwoofer zote zinatumia dual power?

2. Nini tofauti ya Subwoofer kutumia dual power na push pull amplifier?

3. We umesomea wapi? Na level yako ni ipi kwenye electronics?
Nna level three ya electrical installation,masuala ya electronics nimejifunza kupitia phone ndio ilikua Safar yangu yakuanza kusoma masuala ya electronics na amplifier kiujumla
Kwahyo naweza sema Ni practicing huku nnasoma mtandaoni tu
 
Je naweza kudesign Subwoofer kwa kutumia mfumo wa push pull. Na je ni kifaa gani kitakachoweza kuchange frequency ili kuweza kutengeneza bass pekee bila kutumia mfumo kama w Subwoofer?
Subwoofer zinatumia active crossover ya 4555 JRD
Kwa swali lako labda itumike passive crossover lkin haitakupa majibu
Au mim sijakuelewa?
 
Subwoofer zinatumia active crossover ya 4555 JRD
Kwa swali lako labda itumike passive crossover lkin haitakupa majibu
Au mim sijakuelewa?
Umejibu hapo kwenye cross over. Sawa, kwani system nzima ya amplifier ni kwenye ukuzaji tu wa sauti, lakini cross over ndio inayohusika kwenye kuchange tone.[emoji120]
4555D terminal 16.
 
Mkuu matakwa ya watengenezaji tu wakilenga zaidi soko lake
Mchina hawezi akakuekea power transistor alafu akupe na 8ohm speaker hyo Ni never
Mala nyingi mchina hutumia vitu easy Ila vyenye matokeo makubwa
Mfano anakupa tda 2050 Kisha anakupa na volts 18-+ na 8ohms
Apo subwoofer yako inakua inacheza at the peak kabisa ikiwa speaker itazingua tu unapata mosh kwenye ic kwahyo anafanya hivyo ili isiwe Bei juu kwenye manufacturer ili alinganishe Bei na kwa mtumiaji
Mbona powerful zipo Ila Bei yake so unaijua?
Ni kwasababu hizo IC zinatoa sauti nzuri yenye low distortion and low voltage.
 
Honestly kuhusu push power sina uelewa nayo kiwango chake
Ila amplifier ikitumia dual power supply inakua powered kuliko inayotumia supply yakawaida kwasababu speaker inakua inavuta both side
Push pull ni mfumo tu wa kielektronik ambapo huwa unatumia pair ya active device kwa ajili ya kusupply current au kuabsorb current kwenye load. Ambapo mfumo huu hupunguza distortion pia. Kiukweli hauna tofauti na Subwoofer zenye kutumia dual power.
 
Back
Top Bottom