Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg


Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Sub yenye mziki mzito base na sweet tweeter ni aina gani basi kishindo Kama zile radio za zamani JVC,Sony nk sio makeleele

Dah mkuu[emoji23][emoji23]
Zile na subwoofer ni vitu viwili tofauti
Mala nyingi siwezag kumshauri mtu kuhusu subwoofer hizi zakichina coz zinakua na sound output tofauti
Hebu check sea piano mfano wa hiyo hapo juu kwenye uzi juu
 
Habari mkuu. Nina mpango wa kuset home theatre nzuri. Tatizo bajeti hivyo nataka nianze kidogokidogo. AV receiver gani kali ya bei nzuri, yenye teknolojia ya sikuhizi kama 4k na dolby atmos. iwe na 7.2 Na Centre speakers gani nzuri, na subwofer gani nzuri. Nataka ninunue kwanza Receiver. Kisha subwoofer na centre piece.
 
Habari mkuu. Nina mpango wa kuset home theatre nzuri. Tatizo bajeti hivyo nataka nianze kidogokidogo. AV receiver gani kali ya bei nzuri, yenye teknolojia ya sikuhizi kama 4k na dolby atmos. iwe na 7.2 Na Centre speakers gani nzuri, na subwofer gani nzuri. Nataka ninunue kwanza Receiver. Kisha subwoofer na centre piece.

Mkuu unataka kutumia speaker hizi za mtumba?
 
Mkuu nina radio ndogo tuu ina Wats 45 ni Panasonic na nimeuziwa laki 3 aisee inapiga balaa hebu nieleweshe hapo ni mechanisms gani imefanyika

2.1 au 5.1?
By the way nliwah kusema humu kua mziki unaundwa kwa kuunganisha vitu vingi
Hivyo kimoja kati yake kikienda tofauti basi lazima kuna kitu kinapungua!
Mfano amp kubwa ila speaker ndogo,au speaker kubwa amp ndogo,au box design na operation amplifier pia
Hivyo hiyo yakwako iko planned mkuu
 
Habari mkuu. Nina mpango wa kuset home theatre nzuri. Tatizo bajeti hivyo nataka nianze kidogokidogo. AV receiver gani kali ya bei nzuri, yenye teknolojia ya sikuhizi kama 4k na dolby atmos. iwe na 7.2 Na Centre speakers gani nzuri, na subwofer gani nzuri. Nataka ninunue kwanza Receiver. Kisha subwoofer na centre piece.
bongo latest avr mtihani sana, lada kenya, bongo za kusaka kwa manati ila old school zipo
 
Kama yuko vizuri mfukoni ninaweza mconnect na mtu yuko nairobi, ana duka na anauza latest AVRs and used ones. Ila kwa hizi latest mfuko uwe umekaa vizuri boss.

Sent from my SM-N916S using JamiiForums mobile app
niulizie sony str dn1060 au str dn1080 naipata kwa ngapi,second hand, sio mupya, baana bei za wale jamaa wa kenya electrohub ni ndefu sana
 
Back
Top Bottom