Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg

Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Some updates..........
Je music system yako haina Bluetooth na unataka kuongezea easy sana na inawezekana pia ,kwa mafundi nnaweza kuwaelekeza,
Mkuu nina hii redio hapa chini

Sony.png

Ni ya zamani hasa lakini nimegoma kuitupa!!! Tatizo ni kwamba baada ya kuinunua na kuitumia kwa muda, nikawa nimesafiri na kwahiyo ikajaa mavumbi ya kufa mtu. Matokeo yake ni kwamba, CD Tray haifunguki ( haidhuru hata kama CD zimeshapitwa na wakati). Ingawaje umeme unaingia lakini hata nikiwasha hai-respond; it's like power on button haina maiwasiliano na makorokocho ya huko ndani!

Sasa, kuna fundi unayemfahamu anayeweza kurekebisha hayo matatizo ikiwa ni pamoja na speakers zote kuzisafisha ndani na nje?
 
Mkuu Extrovert usicheke!! Ingawaje wasichana waliozaliwa mwaka nilionunua hiyo redio wengine inawezekana wameolewa huku wengine wakiwa wanakaribia kumaliza Form IV, lakini NIMEGOMA kuutupa huo muziki! Laki 7 yangu bado haijaisha!!

Halafu ujana bhana, unajua hiyo laki 700 wakati ule ni takribani $700 ambayo ni +1.5M kwa sasa!!! Kazi niliyokuwa nafanya sasa!!!!
 
mziki wa ukweli sana huo usiutupe mzee...Kazi gani ilikupa laki 7 mwaka 2004?
 
mziki wa ukweli sana huo usiutupe mzee...Kazi gani ilikupa laki 7 mwaka 2004?
Kazi ya kunipa laki 7?! Nimesema "kazi niliyokuwa nafanya sasa" kuonesha kwamba mshahara wangu ulikuwa hauendani na gharama ya redio lakini ndo vile tena ujana! Kimahesabu, huo ulikuwa ni mshahara wa miezi 3 bila kupunguza hata sent!!
 
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza

KaribuView attachment 1559794

Niongezee pia kuelezea kuhusu Aina ya subwoofer
Je unataka kununua Basi zingatia
Zipo za Aina mbili old model na digital,.
Sio majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model
Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu
Ila kinafanya multipurpose ,ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid
Kifupi Mambo yote Ni in one button

Faida yake Ni kua
Aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater (Ila haijawahi[emoji2][emoji2]) inakua na umeme mnyoofu kidogo
Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi
Ni digital,yaani yakisasa,
Lakini pia display yake Ni LCD haitumii umeme mwingi

Je utaijuaje?
1 nob yakuongezea sauti ni moja tu na Zaid utakuta button za menu na input (inategemeana)
Ukiigeuza nyuma inakiplastic kidogo kilichozungushwa nati,yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko woote wa nyuma hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer

Hasara zake

1 Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000
Ila ukifika unaipachika tu huangaiki

2 Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob
3 Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde Sana
Kwahyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo Ni nzuri kwenye uzuri wake
Yenyewe ukiingalia utakuta Ina )nob( yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja
Yaani Cha master volume ,bass , tweeter na mic
Na ukivizungusha vinafika mwisho
Yenyewe ndani power supply yake Ni yakawaida inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida Kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kudambazwa ndani
Yaweza kua seapiano codjec aborder au vyovyote
Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma

Faida yake Ni....
1 ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
2 zinavumilia Sana
3 hata muziki upo pia
4 rahisi kuitumia
Hasara zake
1 display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoipa Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo
VFD inakula umeme
***********†***********†**********+*******†
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo,huzaliana na kuleta hitirafu kwa kukata nyaya na kula speaker
Waya wa speaker unachumvi chumvi hivyo akiingia hauachi
Simple way jinsi yakudhibiti
Pale kwenye tobo kunaki corn Cha duara hua wanakipachika unaweza kitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao
1 chukua maji ya moto kidogo na kitambaa
Kichovye kitambaa kwenye maji Kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano
2 Kisha chukua kisu
Tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani (sio Huku uliko Kanda kwa maji)
3 ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa ,kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu
4 paka gundi upande wa ndani Huku ulikokua unakanda na maji Kisha kibandike Tena Kama kilivyokua

NB hi ni kwazile subwoofer Kama pichani hapo juu
Ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara
Wale zinazotolea mbele chini Ni habari nyingine..
******†******†*******†*******†""""†""""""†*

Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates..........
Je music system yako haina Bluetooth na unataka kuongezea easy sana na inawezekana pia ,kwa mafundi nnaweza kuwaelekeza,

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5 yaani picture video inawezekana pia[emoji3][emoji3]
Hususani wale wenye tv zakizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer,unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer Hadi kwenye tv yako

Stay here....
More good things are here...
Vip kwa subwoofer ambayo BT yake haifanyi pairing na huwezi kuconnect na device nyingne
 
Mkuu nina hii redio hapa chini

Ni ya zamani hasa lakini nimegoma kuitupa!!! Tatizo ni kwamba baada ya kuinunua na kuitumia kwa muda, nikawa nimesafiri na kwahiyo ikajaa mavumbi ya kufa mtu. Matokeo yake ni kwamba, CD Tray haifunguki ( haidhuru hata kama CD zimeshapitwa na wakati). Ingawaje umeme unaingia lakini hata nikiwasha hai-respond; it's like power on button haina maiwasiliano na makorokocho ya huko ndani!

Sasa, kuna fundi unayemfahamu anayeweza kurekebisha hayo matatizo ikiwa ni pamoja na speakers zote kuzisafisha ndani na nje?

Pole sana mkuu
Hongera kwakumiliki two channel music systems
Je ni kua hakuna mtu aliyekua anaitumia?
Au haioneshi kama panya au mende waliingia?
Upo wap mkuu
 
Kazi ya kunipa laki 7?! Nimesema "kazi niliyokuwa nafanya sasa" kuonesha kwamba mshahara wangu ulikuwa hauendani na gharama ya redio lakini ndo vile tena ujana! Kimahesabu, huo ulikuwa ni mshahara wa miezi 3 bila kupunguza hata sent!!

Mkuu hiyo inabidi tuweke na Bluetooth na flash port kabisa
 
Hahahah

ulisumbua sana na migoma ya Bongo Records hapo mtaani 😂😂😂 sema chako chako tu mkuu!
Zama zile ukimiliki huo mziki ni heshima kubwa sana mtaani maana unavyogonga mtaa mzima lazma wajue upo 😂😂😂
 
Hata mie ningefanya the same kwa jinsi ambavyo napenda miziki 😁😁😁 its more of a hobby
 
Pole sana mkuu
Hongera kwakumiliki two channel music systems
Je ni kua hakuna mtu aliyekua anaitumia?
Au haioneshi kama panya au mende waliingia?
Upo wap mkuu
Unamanisha "Hongera kwa kumiliki 2 Channel Antiquity Music System 😀 😀 😀 "!!! Kujibu maswali yako, ni kweli, hakukuwa na mtu anayeitumia. Kuhusu Mende na Panya; wanakosekana vipi kwa mfano?! Hata hivyo, nina uhakika 90% speakers hazijaathiriwa na hao wapuuzi! System yenyewe haijaathiriwa vile vile kwa sababu system haina matundu ya viumbe kama hao kuingia ndani.

Kwa sasa nipo Masasi lakini kama upo Dar bado sio tatizo kwa sababu mara kwa mara huwa nakuja Dar, na nikishindwa kuja mwenyewe, naweza kumtumia mtu akaifikisha popote pale kwa Dar.
Mkuu hiyo inabidi tuweke na Bluetooth na flash port kabisa
Tena kama itawezekana hilo la flash port itakuwa ndo bora zaidi kuliko hilo suala la Bluetooth!!!
 
Mkuu unazungumziaje subwoofer za Kodtec? Una uzoefu nazo kidogo

@Extrovert mkuu zote hizi
Codtec
Seapiano
Alrang
Na zote hizi wanatengeneza zongtec
Kwahyo ni utunzaji tu
Kidogo utofauti anao huyu aboda yeye anatia current nyingi balaa
Uliwahi iona circuit ya aboda iliyoungua[emoji23][emoji23][emoji23][emoji1316][emoji1316]
All in all ukutane na subwoofer imeandikwa samsung au sonny dah utapenda mzee baba
Na kuna mdau anaitwa zec ao usiwaguse
Hawa wengine ukitumia vizuri itadumu
 
Hahahah

ulisumbua sana na migoma ya Bongo Records hapo mtaani 😂😂😂 sema chako chako tu mkuu!
Zama zile ukimiliki huo mziki ni heshima kubwa sana mtaani maana unavyogonga mtaa mzima lazma wajue upo 😂😂😂
Wakati naununua huu muziki, niliufaidi sana kwa sababu nilikuwa naishi kwenye low density residential area kwahiyo nikawa nauachia. Sasa kuna wakati nikaenda kufanya kazi Dar kwahiyo nikaenda na muziki wangu, nikawa naishi nyumba ya kupanga na raia wengine. Sikuufaidi kabisa kwa sababu inabidi uwe kauzu kweli kweli ndipo unaweza kuuachia kutokana na kelele zake, na lazima raia waku-mind kwa sababu lazima udondoshe mende na mijusi waliokuwa darini!
 
@Extrovert mkuu zote hizi
Codtec
Seapiano
Alrang
Na zote hizi wanatengeneza zongtec
Kwahyo ni utunzaji tu
Kidogo utofauti anao huyu aboda yeye anatia current nyingi balaa
Uliwahi iona circuit ya aboda iliyoungua[emoji23][emoji23][emoji23][emoji1316][emoji1316]
All in all ukutane na subwoofer imeandikwa samsung au sonny dah utapenda mzee baba
Na kuna mdau anaitwa zec ao usiwaguse
Hawa wengine ukitumia vizuri itadumu
Ahaaa lakini mbona Kodtec ana sound vizuri zaidi ya hao wenzie? Whats up? Nimeshakutana na Subs 2 za Kodtec mpaka sasa ila sound ni exceptional!
 
Unamanisha "Hongera kwa kumiliki 2 Channel Antiquity Music System 😀 😀 😀 "!!! Kujibu maswali yako, ni kweli, hakukuwa na mtu anayeitumia. Kuhusu Mende na Panya; wanakosekana vipi kwa mfano?! Hata hivyo, nina uhakika 90% speakers hazijaathiriwa na hao wapuuzi! System yenyewe haijaathiriwa vile vile kwa sababu system haina matundu ya viumbe kama hao kuingia ndani.

Kwa sasa nipo Masasi lakini kama upo Dar bado sio tatizo kwa sababu mara kwa mara huwa nakuja Dar, na nikishindwa kuja mwenyewe, naweza kumtumia mtu akaifikisha popote pale kwa Dar.

Tena kama itawezekana hilo la flash port itakuwa ndo bora zaidi kuliko hilo suala la Bluetooth!!!

Nimekusoma mkuu japo mim nipo iringa ila tunaweza kuangalia namna yakufanya
Itafaa tuweke kitu kama hichi mkuu
IMG_1745.jpg
 
Back
Top Bottom