Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg


Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Ahaaa lakini mbona Kodtec ana sound vizuri zaidi ya hao wenzie? Whats up? Nimeshakutana na Subs 2 za Kodtec mpaka sasa ila sound ni exceptional!

Kaka sounds pia inategemeana na box design mkuu si unajua box anachonga mtu mwingine ila circuit ni mtu mwingine!
Lakini pia inategemeana na alie itengeneza
Mbona hata hiz seapiano kuna nyingine sound good zingine zinazingua kaka
 
Nimekusoma mkuu japo mim nipo iringa ila tunaweza kuangalia namna yakufanya
Itafaa tuweke kitu kama hichi mkuuView attachment 1698605
Dah! Sasa naona suala la matengenezo ya hiyo system ishakuwa issue manake Masasi-Iringa, ni balaa lingine hilo! Ingekuwa Dar wala isingekuwa taabu kwa sababu kuna bro na mdogo wangu pale!
 
@Extrovert mkuu zote hizi
Codtec
Seapiano
Alrang
Na zote hizi wanatengeneza zongtec
Kwahyo ni utunzaji tu
Kidogo utofauti anao huyu aboda yeye anatia current nyingi balaa
Uliwahi iona circuit ya aboda iliyoungua[emoji23][emoji23][emoji23][emoji1316][emoji1316]
All in all ukutane na subwoofer imeandikwa samsung au sonny dah utapenda mzee baba
Na kuna mdau anaitwa zec ao usiwaguse
Hawa wengine ukitumia vizuri itadumu
Hawa Sony ni mwisho wa maneno kwa mziki nimewakubali.
 
Kaka sounds pia inategemeana na box design mkuu si unajua box anachonga mtu mwingine ila circuit ni mtu mwingine!
Lakini pia inategemeana na alie itengeneza
Mbona hata hiz seapiano kuna nyingine sound good zingine zinazingua kaka
Unajua mi siamini kama ni kiwanda kimoja mpaka sasa 😂😂😂 hao watu! Sababu kuna mtu alinambia hata Circuit zao ni tofauti na kweli hata mziki wake ni tofauti. Kodtec ana dynamic range bass ila Sea piano ana boom bass! Kuna aina flani za bass hazisikiki kwenye sea piano ila kodtec zinasikika both punchy and midrange bass notes.
 
Unajua mi siamini kama ni kiwanda kimoja mpaka sasa [emoji23][emoji23][emoji23] hao watu! Sababu kuna mtu alinambia hata Circuit zao ni tofauti na kweli hata mziki wake ni tofauti. Kodtec ana dynamic range bass ila Sea piano ana boom bass! Kuna aina flani za bass hazisikiki kwenye sea piano ila kodtec zinasikika both boomy and midrange bass notes.

Yess mkuu viwanda tofauti ila wana print hizo nembo tu
Kwenye music wanajitahid na wapo tofauti sana
Ukisikilza codjc ya musa yofaut na ya omali japo watts n sawa[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Yah ni ile analog mzee yenye knobs! Ile ya Circuit ya Card tu iliharibiwa na umeme prematurely since then haipo sawa. Japo nzima tu nilibadili capacitor ili blow out!
Upande wa AUX hauna sauti kama wa Bluetooth na FM

Nazikubal sana mkuu ziko good saaana
 
Wakati naununua huu muziki, niliufaidi sana kwa sababu nilikuwa naishi kwenye low density residential area kwahiyo nikawa nauachia. Sasa kuna wakati nikaenda kufanya kazi Dar kwahiyo nikaenda na muziki wangu, nikawa naishi nyumba ya kupanga na raia wengine. Sikuufaidi kabisa kwa sababu inabidi uwe kauzu kweli kweli ndipo unaweza kuuachia kutokana na kelele zake, na lazima raia waku-mind kwa sababu lazima udondoshe mende na mijusi waliokuwa darini!
Hahaha mi ilionikuza ni Sony CFS-717 !!!
Nilikuwa naipigisha ngoma kweli enzi hizo tape 1,500 umekamata

Album ya zote kali 😁😁😁! Mtaani tulikuwa na league na mwanangu Ayubu, kila mtu akitoka school lazma akiwashe kwao 😂 uzuri tulikuwa Mid density Areas kwahio mijengo imepangika kuko kimya ni kuchapa mziki tu.
 
Hahaha mi ilionikuza ni Sony CFS-717 !!!
Nilikuwa naipigisha ngoma kweli enzi hizo tape 1,500 umekamata

Album ya zote kali [emoji16][emoji16][emoji16]! Mtaani tulikuwa na league na wanangu kila mtu akitoka school lazma akiwashe kwao [emoji23][emoji23][emoji23]

[emoji23][emoji23]penyewe hazinaga bass ile low kabisa
 
Back
Top Bottom