Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg

Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Yess mkuu viwanda tofauti ila wana print hizo nembo tu
Kwenye music wanajitahid na wapo tofauti sana
Ukisikilza codjc ya musa yofaut na ya omali japo watts n sawa[emoji23][emoji23][emoji23]
Bhana we, nimetoka juzi Mlimani City dukani kwao kabisa. Kuna toleo limetoka lina bass 3; speaker 2 ubavuni na moja mbele. Kaka inasound vizuri kama mziki wa gari ile ya kina dicksound!

Mpaka nikashawishika!
 
Hahaha mi ilionikuza ni Sony CFS-717 !!!
Nilikuwa naipigisha ngoma kweli enzi hizo tape 1,500 umekamata

Album ya zote kali 😁😁😁! Mtaani tulikuwa na league na mwanangu Ayubu, kila mtu akitoka school lazma akiwashe kwao 😂 uzuri tulikuwa Mid density Areas kwahio mijengo imepangika kuko kimya ni kuchapa mziki tu.
Duh! 😀 😀 😀 😀

Tumetoka mbali sana kama taifa! Nazikumbuka vema hizo redio, home tulikuwa nayo moja lakini kwa bahati mbaya ikawa haifui dafu mbele ya mashine la mtumba ambalo alituleaga bahari mmoja hivi, enzi hizo akipiga sana route za far east hususani Japan!! Halafu yale madude ya mtumba sijui yana matatizo gani manake jamaa alituleteaga friji ya mtumba na tukaitumia hadi tukachoka nayo, ikawekwa stoo baada ya kuonekana inakula sana umeme lakini mashine bado ilikuwa konki manake ilikuwa ukisahau soda juu kwa masaa mawili na bila kupunguza ubaridi, basi hesabu utakuta vipande vya chupa!!
 
Narudisha mpira kwa wadau!!!

Wakuu natafuta mzuri anayeweza kufufua huu mziki! Kama kuna mtu anayemfahamu fundi wa kweli, au hata wale wanaotumika na Sony, please naomba taarifa zake.

Sony.png

Radio ni ya zamani hasa lakini nimegoma kuitupa!!! Tatizo ni kwamba radio iliacha kutumika kwa muda mrefu sana na kwahiyo ikajaa mavumbi ya kufa mtu. Matokeo yake, CD Tray haifunguki ( haidhuru hata kama CD zimeshapitwa na wakati). Ingawaje umeme unaingia lakini hata nikiwasha hai-respond; it's like power on button haina maiwasiliano na makorokocho ya huko ndani!

Sasa, kuna fundi unayemfahamu anayeweza kurekebisha hayo matatizo ikiwa ni pamoja na speakers zote kuzisafisha ndani na nje?
 
Ahahhah madude ya mtumba ni noma
 
Narudisha mpira kwa wadau!!!

Wakuu natafuta mzuri anayeweza kufufua huu mziki! Kama kuna mtu anayemfahamu fundi wa kweli, au hata wale wanaotumika na Sony, please naomba taarifa zake.

View attachment 1699063

Radio ni ya zamani hasa lakini nimegoma kuitupa!!! Tatizo ni kwamba radio iliacha kutumika kwa muda mrefu sana na kwahiyo ikajaa mavumbi ya kufa mtu. Matokeo yake, CD Tray haifunguki ( haidhuru hata kama CD zimeshapitwa na wakati). Ingawaje umeme unaingia lakini hata nikiwasha hai-respond; it's like power on button haina maiwasiliano na makorokocho ya huko ndani!

Sasa, kuna fundi unayemfahamu anayeweza kurekebisha hayo matatizo ikiwa ni pamoja na speakers zote kuzisafisha ndani na nje?

Awe wap mkuu
Mim hadi iringa mkubwa
 
Na hiyo ndo sababu hadi sasa sijaipeleka kwa fundi! Nafikiria nikienda Dar, nikawaulizie mafundi wa Sony ambao zamani ofisi yao ilikuwa Mikocheni Industrial Area!

Yess hapo utakua umefanya kitu good mkuu
Mziki mzuri huo
 
No kuna bro alikuja nayo toka Canada, ilikuwa inakaa kishenzi na battery, ukiweka Duracell au Energizer ndio unasahau hata week 2 ila battery za kibongo zile Panasonic zilikuwa unakula ngoma mpaka siku 4 ndio zimeisha.

Niliwah kua nako ka moja hivi
Nliona katantia umasikini nkakitupa huko

Kipindi nnakua mzee amenichapa sana sana kwenye mission za ufundi redio daaah

Kuna day karudi kakuta nyumba yote mwangaa[emoji23][emoji23]
Kuna dumu lipo chini ya sofa linahema mbayaa[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Za kibongo nyingi zilikuwa chenga! Zinakula betri kama mchwa 😂😂😂! Ukimaliza CD ya nyimbo 16 na hela imeisha 😂😂😂!!!

Hizo mission za madumu kaka acha tu, kulikuwa na speaker za kichina kwa wamachinga nimenunua sana zile. Nikawa na connect redio ya mkulima na dumu geto.

Baadae Sound niliihamishia kwenye baskeli! Kreti la pepsi la mbao nililigeuza subwoofer kwenye baskeli yangu 😁😁😁 nikawa natimba nayo skonga!
 
Back
Top Bottom