Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg


Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Hii ni ya kisasa zaidi. Ina bluetooth
Kuna sabufa ambazo, ukiongeza sauti unasikia base ila ukipunguza base inapotea. Lakini hii sea piano. Sijajuta kuwa nayo.
Nenda duka la karibu yako kisha waambie wakusikilizishe muziki kupitia sea piano.
Usihangaike kuchukua aborder sijui sunder, ongeza hela hapo. Hakika hautajuta
Hivi hii inayo Bluetooth??
 
Johnny Impact
kelphin kepph

Hivi inawezekana vipi mtu anaweka volume hadi 30 kwenye hii sea piano ?.

Maana nimeenda kupanga sound kwenye hii subwoofer ila sikumbuki kama hata nimefika volume 15 kwenda juu. Lakini nilivyotoka ili kuwaaga majirani kila mtu niliona huzuni machoni.

Tafsiri ya watu kuniangalia nilihisi nimenunua kitu ambacho kitasababisha wao wasilale alafu sikai hapo.

Hela yanGu imekuwa adhabu kwao daah niliona huruma sana na mtu niliemnunulia hiyo kitu namjua vizuri

Nawasilisha

20211117_143928.jpg
 
Hii ni ya kisasa zaidi. Ina bluetooth
Kuna sabufa ambazo, ukiongeza sauti unasikia base ila ukipunguza base inapotea. Lakini hii sea piano. Sijajuta kuwa nayo.
Nenda duka la karibu yako kisha waambie wakusikilizishe muziki kupitia sea piano.
Usihangaike kuchukua aborder sijui sunder, ongeza hela hapo. Hakika hautajuta
Nitaijuaje kuwa hii ndo sea piano SP-1002? Kuna ishara yoyote au nembo au maelezo ya kujulisha kuwa hiyo ndo yenyewe?
 
Johnny Impact
kelphin kepph

Hivi inawezekana vipi mtu anaweka volume hadi 30 kwenye hii sea piano ?.

Maana nimeenda kupanga sound kwenye hii subwoofer ila sikumbuki kama hata nimefika volume 15 kwenda juu. Lakini nilivyotoka ili kuwaaga majirani kila mtu niliona huzuni machoni.

Tafsiri ya watu kuniangalia nilihisi nimenunua kitu ambacho kitasababisha wao wasilale alafu sikai hapo.

Hela yanGu imekuwa adhabu kwao daah niliona huruma sana na mtu niliemnunulia hiyo kitu namjua vizuri

Nawasilisha

View attachment 2016120

1 Mziki una upana wa kupigia!
Yaan ili uisikie vema upana wa chumba na kama ina dali au la ni vitu vyakuzingatiwa sana
Kama ni geto na kuna dari itapiga zaid ya nyumba isiyo na dari
2 hizo digits sio issue kubwa
Utakutana na nyingine ina 80 ila ikawa ovuo kuliko yenye 15,20
Kifupi hizo zinakupa uwezo wakuona tu kinachofanyika,haziongezi ufanisi wa upigaji wa mziki
 
Back
Top Bottom