Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg


Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Mkuu..
Hivi ni kwanini mziki wa kwenye gari unakua na Base zuri saana?
Wanatumia vitu gani na je naweza funga gheto ili niendelee kula base la nguvu?

Betri ya gari ni 12volts ila current ni 70,40
Umeme wa nyumbani ni 240volts ila currts unakuta hata 20 hazifiki
Kwenye gari kuna currents nyingi sana sana sana mkuu
Lakini pia ni setting za equalizer zinaongezea
Na mwisho kabisa ile bass inakua n 12nchies ambayo kama ni pioneerunakuta dukani hadi 120 hiyo ni speaker tu bado box yake na carpets
Wakati hiyo 120 n bei ya subwoofer ya mtu[emoji23] je mtapata sound sawa?
Ukitaka kuitumia home inabidi uwe na transfoma ya high currents ili kupata unachotaka
Kama sivyo basi itengenezwe mashine ya highcurrent na speaker ziwe kubwa kitu ambacho n kuanzia laki6
 
Betri ya gari ni 12volts ila current ni 70,40
Umeme wa nyumbani ni 240volts ila currts unakuta hata 20 hazifiki
Kwenye gari kuna currents nyingi sana sana sana mkuu
Lakini pia ni setting za equalizer zinaongezea
Na mwisho kabisa ile bass inakua n 12nchies ambayo kama ni pioneerunakuta dukani hadi 120 hiyo ni speaker tu bado box yake na carpets
Wakati hiyo 120 n bei ya subwoofer ya mtu[emoji23] je mtapata sound sawa?
Ukitaka kuitumia home inabidi uwe na transfoma ya high currents ili kupata unachotaka
Kama sivyo basi itengenezwe mashine ya highcurrent na speaker ziwe kubwa kitu ambacho n kuanzia laki6
Shukrani mkuu..
Maana juzi kati nimepanda chuma za Mbeya Njombe, Dere akawa kam haelewi ni mwendo wa bass tu.

So mimi naependa bass nivute home theater? Hi-Fi au Subwoofer?
 
Johnny Impact
kelphin kepph

Hivi inawezekana vipi mtu anaweka volume hadi 30 kwenye hii sea piano ?.

Maana nimeenda kupanga sound kwenye hii subwoofer ila sikumbuki kama hata nimefika volume 15 kwenda juu. Lakini nilivyotoka ili kuwaaga majirani kila mtu niliona huzuni machoni.

Tafsiri ya watu kuniangalia nilihisi nimenunua kitu ambacho kitasababisha wao wasilale alafu sikai hapo.

Hela yanGu imekuwa adhabu kwao daah niliona huruma sana na mtu niliemnunulia hiyo kitu namjua vizuri

Nawasilisha

View attachment 2016120
Hii sea piano naielewa sana inagonga haswa japo mziki sio dynamic kama wa Kodtec
 
Kila kitu ni muhimu.....
Ndani ya speaker kuna coil
Urefu wa coil n wingi wa Ohms
Unene wa coil ni wingi wa watts
Amplifier zina guide watts na ohms ni vyema kuzingatiaa vyote
Speaker za twita za subwoofer n 4ohms ila watts 15
Speaker kubwa za PA ni 4ohms ila watts 800
Je unadhan ukiunganisha ile ya subwoofer kwenye ca 32 inayohitaj 4ohms watts 1000 itakuaje?
Spika ya watt 800 itaunguzwa ukiiweka kwenye CA32

Basi tukubaliane kuwa kitu pekee cha kuzingatia ni watts...
 
View attachment 2055850
[mention]Zabron Hamis [/mention] [mention]Smart Guy [/mention] [mention]Extrovert [/mention] [mention]That Gentleman [/mention]
Dundo linasukwa hilo
4.1 channel
Nina maswali mengi kuhusu hii circuit.

1.Je hizo tip huwa ni kwaajili ya base? na tda ni kwaajili ya tweeters?

2.Je hiyo circuit inahitaji volts tofauti tofauti ndiyo maana ina Rectifier bridge mbili?
 
Kuna rafiki yangu anayo iyo ailing sub woofer naitamani mpaka kesho kanunua 2012 mpaka leo inapiga mziki mzito na wenye viwango vya juu ukiweka na home theatre ya kijinga kijinga haioni ndani, huwa namwambia aniuzie hataki
Yanagonga sound kweli ila mengi niliokutana nayo mabovu
 
Spika ya watt 800 itaunguzwa ukiiweka kwenye CA32

Basi tukubaliane kuwa kitu pekee cha kuzingatia ni watts...

Watts!!?
Mkuu hivi nkuulize swali
Ukichukua 4ohms ya watts 800
Na 4ohms ya watts 15
Ukazifungua zile coil unadhan urefu wa waya ni sawa!?
 
Nina maswali mengi kuhusu hii circuit.

1.Je hizo tip huwa ni kwaajili ya base? na tda ni kwaajili ya tweeters?

2.Je hiyo circuit inahitaji volts tofauti tofauti ndiyo maana ina Rectifier bridge mbili?

Yah huku kwenye transistor ni bass
Afu hizo tda ni tweeter tu

Kuhusu volts n sahihi pia
Huko kwenye transista kuna 30v 0 30v ac ambayo ukiipeleka kwenye dc unasogea had kwenye 42+_
Ila tda n 18 0 18v +_
 
We jamaa upo wapi?[emoji28] nmelipenda hilo

Iringa boss,nlikua dar juzi ila nmerud nlifata baadh ya vitu
IMG_5915.jpg

Hi 8ohms bass speaker nch12! Ya sonny
Moja inaenda 100000 dar!
Ili zinipe sound nzur na deep bass naweka mbili kwenye box moja ya central line zitashuka hadi 4ohms [emoji16][emoji16]
957E7533-2C5C-4266-86BA-BAE42B2FDE5A.jpg

Hizi tda 4 zitapewa tweeter 4 kila moja na channel yake
Afu nakuruhusu njoo na HT yako yoyote tushindane
Utanipita kwenye digital sound tu na muonekano wa box kidoooogo sana
 
Back
Top Bottom