Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg

Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Iringa boss,nlikua dar juzi ila nmerud nlifata baadh ya vitu
View attachment 2056778
Hi 8ohms bass speaker nch12! Ya sonny
Moja inaenda 100000 dar!
Ili zinipe sound nzur na deep bass naweka mbili kwenye box moja ya central line zitashuka hadi 4ohms [emoji16][emoji16]
View attachment 2056787
Hizi tda 4 zitapewa tweeter 4 kila moja na channel yake
Afu nakuruhusu njoo na HT yako yoyote tushindane
Utanipita kwenye digital sound tu na muonekano wa box kidoooogo sana
Kwahio hio mitambo ndio ipo ndani ya speaker box au inakuwaje maana ma capacitor mawili makubwa hayo!
 
Nikifikia huku ni shangwe

Mkuu jifunze kusuka circuits
Itakupa uwanja mpana zaidi kwenye kazi yako
Kuna redio utapewa imeshapita kwa mafundi 40 inabid utengeneze irud ifanye kazi
Hutaweza kama hutasuka mwenyewe.
2 kuna circuit hazipatikan tena dukani zikizingua je mtu atupe speaker zake? No itabidi usuke amp isukume hizo speaker
Kuna kitu kidogo sana kinawasumbua mafundi wengi
Yaan kati ya mafundi 10 basi 9 had 10 hawafahamu how op amp working
Hapa ndipo shida ilipo!
Huwezi kutengeneza bass nzuri na hata tweeter pia
Ndio maana hata mimi bado najifunza zaidi na zaidi

Yote kwa yote andaa pesa kias ya components
Na vifaa
Me ntakupa basic free kabisa
 
IMG_2938.jpg

Hapa nlikua nafanya majaribio ya relay system
Ilifanikiwa
Ukiwasha subwoofer kuna lile li mlio la puuf!!
Hi ni suluhisho
Ukiweka hi circuits utawasha redio yako itawaka
Baada ya sekunde kadhaa ndipo speaker zitaanza kufanya kazi
 
Iringa boss,nlikua dar juzi ila nmerud nlifata baadh ya vitu
View attachment 2056778
Hi 8ohms bass speaker nch12! Ya sonny
Moja inaenda 100000 dar!
Ili zinipe sound nzur na deep bass naweka mbili kwenye box moja ya central line zitashuka hadi 4ohms [emoji16][emoji16]
View attachment 2056787
Hizi tda 4 zitapewa tweeter 4 kila moja na channel yake
Afu nakuruhusu njoo na HT yako yoyote tushindane
Utanipita kwenye digital sound tu na muonekano wa box kidoooogo sana
Huu mzigo uki kamilika tuma picha tuuone
 
Digital sound zikoje mkuu
 
Mkuu jifunze kusuka circuits
Itakupa uwanja mpana zaidi kwenye kazi yako
Kuna redio utapewa imeshapita kwa mafundi 40 inabid utengeneze irud ifanye kazi
Hutaweza kama hutasuka mwenyewe.
2 kuna circuit hazipatikan tena dukani zikizingua je mtu atupe speaker zake? No itabidi usuke amp isukume hizo speaker
Kuna kitu kidogo sana kinawasumbua mafundi wengi
Yaan kati ya mafundi 10 basi 9 had 10 hawafahamu how op amp working
Hapa ndipo shida ilipo!
Huwezi kutengeneza bass nzuri na hata tweeter pia
Ndio maana hata mimi bado najifunza zaidi na zaidi

Yote kwa yote andaa pesa kias ya components
Na vifaa
Me ntakupa basic free kabisa
Shukrani kaka. Nitafanya hvyo
 
Huto tu MP5 tuna kelele sana yani hicho ndio kinaniudhi! Yani hata redio ikiwa standby bado kama mvumo ule wa vuuuuuuuuu!!! Unauondoaje?

Connect waya mnene kutoka kwenye ground ya mp3 had kwenye power supply
Au punguza gain ya amp
 
Back
Top Bottom