Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg

Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Kwa mujibu wa picha hapo chini nikizima hii sub kisha nikawasha basi nakuta hapo inakuja zero. Ikiwa hapo stereo inapotea na sauti inakuwa kama mtu aliyezibwa mdomo. So nikizungusha mwenda moja au zaidi ndio angalau sauti inasikika vizuri. Nawezaje kutatua hili?

IMG_20220117_205451.jpg
 
Kuna true power
Na plate power
Plate power Hizo n za mauzo tu mkuu
Muhimu ni kuangalia watts ya amp yenyewe
Ukitaka kujua watts ya amplifier voltage ya transformer ni muhimu pia
Afu pia unapoongeza sauti ndio watts zinazidi (hapo kama unatumia kipimo kupima)
Kifupi nyingi wanaandika tu kuvuta wateja
Kwa kutumia multimeter nawezaje kujua watts za kifaa
 
Natumia Sony DAV-DZ350, ina tatizo kwenye Bluetooth kwa muda mrefu kidogo sasa. Ni mara chache sana Bluetooth inakubali ku'connect (labda mara 1 kwa mwezi). Tatizo limeanza tu out of blue, haikuwahi kudondoka wala kupigwa shoti. Ukiwasha bluetooth inasoma vizuri kama inasubiri iwe connected, ila haionekani kwenye device yoyote kila uki'search.
Tatizo linaweza kuwa nini?
 
Kaka kuna vitu kadhaa Kwann ht zinauzwa ghalama
1 sound system yake inakua computerized zaidi...i mean signals zake zinapita kwenye chip ambayo inazicontrol kabla yakuingizwa kwenye amplifier zake...that’s why utaona zinasikika vyema zaidi.
2 nyingi zake zinamifumo ya protection ...inapotokea hitirafu yeyote nyingi zinajizima ili zisiharibu mfumo wake.
3 speaker na box design inakua ya hari ya juu sana...mbali na muonekano wake kiujumla
4 inakupa true 5.1 channel .... hdmi output na component nyingine kama optical cable.
5 bland pia inahusika
Mtu ukimtajia SONNY tayari kuna picha unaijenga kichwan
Kwahyo inaongeza value kiasi

Ht haimanishi kua inapiga mzikiiii mkubwaaaaa zote Hapana
Inategemeana sana na watts zake
Mkuu kuna subwoofer zingine zinagongaa[emoji3][emoji3] yan zinagonga sio kidogo....
Ni vile tu imani imejengeka kwao
Mkuu kwa faida ya wengi miongoni mwa hizo sabufa ni zipi labda.
 
msaada, kuna sabufa langu sea piano limepigwa short ya umeme kutokana na radi ya mvua, ilikuwa haiwaki kabisa nikapeleka kwa fundi mmoja akafanya yake ikaanza kupitisha umeme mbele ikawa inawaka lakini haitoi saut wala ikawa haijiswitch off wala on mpaka uichomeke au kuichomoa kwenye umeme,, mpaka hapo ilipofika wadau shida nin ili napoenda kwa fundi mwingine niwe hata naufaham kidogo
 
Kwa mujibu wa picha hapo chini nikizima hii sub kisha nikawasha basi nakuta hapo inakuja zero. Ikiwa hapo stereo inapotea na sauti inakuwa kama mtu aliyezibwa mdomo. So nikizungusha mwenda moja au zaidi ndio angalau sauti inasikika vizuri. Nawezaje kutatua hili?

View attachment 2085457

Hiyo ni tweeter mkuu
Ikiwa zero n kama umetoa mziki wa tweeter hadi uipeleke zaidi ndio utapata mziki
Ikiwa zero maana yake huwezi kupata mchicha
Subwoofer iko sahihi nadhan labda huenda inajisahau ila yenyewe iko sawa tu
 
Natumia Sony DAV-DZ350, ina tatizo kwenye Bluetooth kwa muda mrefu kidogo sasa. Ni mara chache sana Bluetooth inakubali ku'connect (labda mara 1 kwa mwezi). Tatizo limeanza tu out of blue, haikuwahi kudondoka wala kupigwa shoti. Ukiwasha bluetooth inasoma vizuri kama inasubiri iwe connected, ila haionekani kwenye device yoyote kila uki'search.
Tatizo linaweza kuwa nini?

Ic kujisahau ni kitu cha kawaida sana... na nyingine hua zinachanganyikiwa kabisa
Issue n kua kwenye ht signals zinakua processed na processors
Hivyo ukianza tu kuishika shika inaweza ongeza shida
Kwa haraka hapo jaribu simu nyingine tofauti au weka Bluetooth module
 
msaada, kuna sabufa langu sea piano limepigwa short ya umeme kutokana na radi ya mvua, ilikuwa haiwaki kabisa nikapeleka kwa fundi mmoja akafanya yake ikaanza kupitisha umeme mbele ikawa inawaka lakini haitoi saut wala ikawa haijiswitch off wala on mpaka uichomeke au kuichomoa kwenye umeme,, mpaka hapo ilipofika wadau shida nin ili napoenda kwa fundi mwingine niwe hata naufaham kidogo

Subwoofer yako ni hizi za kisasa?
Huku nyuma kuna ki plastic hiv cha kufungua?
 
Mkuu..
nikitaka nisuke/ unisukie sound system yenye bass ya kiwango kwa ajili ya matumizi ya Gheto la kijana inawezekana?

Na kama inawezekana gharama inaweza range shilingi ngapi?

Mimi siyo mtu wa masuala ya umeme, ni kijana mtundu_tundu ambae mtu akinielekeza kitu naweza fanya.

Nb
Nataka iwe na speakers 2 ndefu ndefu za box.
Niko Mbeya
Natanguliza shukrani.
 
Kama unaweza kusuka naweza kukupa basic ukafanya mwenyewe
Ghalama inategemeana na sound unayotaka na vifaa vyake mfano nayoitengeneneza now bass zake tu speaker zinaghalim 120 hizo n bei ya speaker dar
Bado box sijachonga
Tu assume kua 180-200 hi ni bass speaker na box zake
Wakati hiyo 200 ni subwoofer mpya!

Kwahyo estimate cost inategemeana na aina ya mziki unaotoka
Lakini pia unaweza tengeneza ya kawaida tu ila inayokita vizur tu
Mimi zakwangu naanzia 150-200,350,450
650 nakuendelea hiz ni bass kubwa mfano wa zile za kwenye magari
Na mala nyingi wanatengeneza watu wenye grocery
Hi ukiweka geto dah[emoji28][emoji28]
 
Mkuu nimekusoma vilivyo..
Ngoja niandae 450 ili tufanye hiyo kazi.
Maana napenda bass😋😋
 
Back
Top Bottom