Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg


Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Hi inakupa deep mzee
Haiwez kua dynamic
Ingawq hizi deep sasa zinatofautiana freq sas
Zipo zinapika ile low kavu
Na hiz subwoofer kawaida
Hizi freq zinaenda sawa na uwezo wa amplifier
Uwezo wa amp unaenda sawa na power supply

Power supply ni umeme unaotumika kwenye amplification
Subwoofer nyingi zinacheza kati ya 9v hadi
27v 0 27v
Zile za kwenye magari zinazogonga saba bass unakuta zina 35+_
Current ndio balaa! Unaweza kuta had 40[emoji16]
Wakat hiz za nyumban current yake unakuta ikizid sana ni2,6




Mziki mzuri ghalama [emoji1316]
Nakubali mkuu
 
Hili jambo bado linakutesa bado mkuu
Ukishaona sound system kuna speaker zinaimba afu nyingi inadunda bass(mkito) pekee kama subwoofer hiyo ni deep
Kama speaker inaimba huku inadunda (stereo mode) hi ni dynamic
Anhaa sawa mkubwa nimekusoma vizuri kabisa
 
Nkupe urahisi
Pamoja na [mention]Smart Guy [/mention] ukiona sounds system yako ina .1 ujue hiyo ni deep
Mfano 2.1,2,2
Au 5.1

HT ni 5.1

Nkupe urahisi
Pamoja na [mention]Smart Guy [/mention] ukiona sounds system yako ina .1 ujue hiyo ni deep
Mfano 2.1,2,2
Au 5.1

HT ni 5.1
Mkuu nimeinunua hii samsung aiseee inatoa mziki heavy tena deep bass kuliko ile lg home theater 5.1, najiuliza kwanini Soundbar ya watt 410 tena 2.1 inakuwa na mziki mzito kuliko home theater ya 5.1 tena watt 1000 Kwanini?
 
Tafta subwoofer ya Kodtec mkuu hutajuta
Welcome back bro.

Ile Kodtec yetu hivi itafaa kwa movies? Au ni kwa music tu.

Hafu kuna mtu hapa: Ana pesa ndogo 450,000 ameniuliza kati ya Hisense Soundbar Watt 200 au Sony DAV TZ140 Ya Watt 320 aende na ipi.

Yeye ni mdau wa Movies na PS4 Sanaa. Music sio sana ila anasikiliza sometimes.
 
Kuna Swahiba wangu alininunuaga Sobwoofer Dukani mpya kabisa, zilikua Speker 2.... pale Dukani zote zilipiga ila alivyornda kwake ikawa inapiga moja.... hata akiijaribu kwa Jirani zinapiga zote 2 ila akiileta kwake inapiga moja nyingine inakaa kimya au inakoroma..... hadi leo anatumia moja tu..... shida inaweza kua nini??????
 
Mkuu nimeinunua hii samsung aiseee inatoa mziki heavy tena deep bass kuliko ile lg home theater 5.1, najiuliza kwanini Soundbar ya watt 410 tena 2.1 inakuwa na mziki mzito kuliko home theater ya 5.1 tena watt 1000 Kwanini?

Sababu ni nyingi
Ila moja inayoweza kua sababu ni kua
Bass ipo moja ....ila tweeter ni nyingi
Inaweza kua range inatofautiana kidogo
2.1 speaker ni chache

Pia kuna vitu vingine ni technical kidogo
 
Kuna Swahiba wangu alininunuaga Sobwoofer Dukani mpya kabisa, zilikua Speker 2.... pale Dukani zote zilipiga ila alivyornda kwake ikawa inapiga moja.... hata akiijaribu kwa Jirani zinapiga zote 2 ila akiileta kwake inapiga moja nyingine inakaa kimya au inakoroma..... hadi leo anatumia moja tu..... shida inaweza kua nini??????

Ic
Au huenda loose kidogo tu....
Ipo mkoa gan?
 
Back
Top Bottom