Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg


Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Hili jambo bado linakutesa bado mkuu
Ukishaona sound system kuna speaker zinaimba afu nyingi inadunda bass(mkito) pekee kama subwoofer hiyo ni deep
Kama speaker inaimba huku inadunda (stereo mode) hi ni dynamic
Dynamic Sound ni 45Hz Frequency upto around 120Hz, But Sub bass ambazo ndio Frequency zake ziko below hio range ya 45Hz. Zinashuka mpaka kufikia range ya deep bass ambayo ni in-audible 20Hz mpaka 0Hz
 
Mkuu nimeinunua hii samsung aiseee inatoa mziki heavy tena deep bass kuliko ile lg home theater 5.1, najiuliza kwanini Soundbar ya watt 410 tena 2.1 inakuwa na mziki mzito kuliko home theater ya 5.1 tena watt 1000 Kwanini?

Mkuu nimeinunua hii samsung aiseee inatoa mziki heavy tena deep bass kuliko ile lg home theater 5.1, najiuliza kwanini Soundbar ya watt 410 tena 2.1 inakuwa na mziki mzito kuliko home theater ya 5.1 tena watt 1000 Kwanini?
inasababishwa na distribution ya watts katika speaker, hiyo sound bar, full range ni 160 watts h bass ni 250watts @4ohm wakati hiyo sony ya 1000w bass yake ni 180 watts @ 3ohms, hivyo haiwez kushindana na hiyo sound bar kwa maana ya deep bass hata kidogo
 
[mention]benwise [/mention]
Pow mkuu za kwako?

Kitu chakwanza wewe unataka sound ya aina gani?
Aina ya sound unayoitaka ndio itaamua uwe na nini?
1 tupate concept ya equlizer
Na crossover
2 crossover zipo mbili active na passive
S
Definitely unaongelea active sio?
Kila kimoja na kazi yake ikitegemeana na unachokitaka
Zipo equlizer zipo crossoved
Kazi ya equlizer ni kutengeneza output signals zikiwa na effects
Utachagua vocal,bass na vinginevyo kwa namna upendayo
Yaan kuset freq tofauti tofauti
Ila kazi ya crossover ni kutenganisha signals
Low,mid,tweeter hivyo tu
Ila sasa je wewe unataka kwa matumizi yapi?
Miziki ya kwenye magari?
Au kwa matumizi ya kawaida mfano wa library
Au kwenye PA System?
Nashukuru mkuu,ninayotaka ni Kwenye pa system hasa kwa vyombo vya mziki wa live kama bendi
 
inasababishwa na distribution ya watts katika speaker, hiyo sound bar, full range ni 160 watts h bass ni 250watts @4ohm wakati hiyo sony ya 1000w bass yake ni 180 watts @ 3ohms, hivyo haiwez kushindana na hiyo sound bar kwa maana ya deep bass hata kidogo
Ahsante mkuu, kwa sasa masikio yangu yanausikia mziki wenyewe niliokuwa nautaka.
 
Kuna mwanangu anasukuma huu mzigo kwa 450k. Una spika moja...kwa hiyo bei niuchukue

Kuna mwanangu anasukuma huu mzigo kwa 450k. Una spika moja...kwa hiyo bei niuchukue??View attachment 2269336View attachment 2269337
hii ni Sony LBT 705 ,ni redio ndogo sana, specs zake hizi hapa

Specifications​

Power output: 60 watts per channel into 6Ω (stereo)

Frequency response: 10Hz to 50kHz

Total harmonic distortion: 5%

Input sensitivity: 1mV (mic), 2.5mV (MM), 200mV (line)

Output: 180mV (line)

Dimensions: 355 x 132.5 x 320mm

Weight: 6.6kg

Year: 1991
 
Back
Top Bottom