Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg

Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Hivi unajua kwamba amplifier/avr nyingi haziwezi kuwa stable for long kwa load ya 2 ohm?.
Umesema nyingi na sio zote

Hizo kulingana na class yake ndo zinafanya zinakuwa hivo

Kuhusu ku work harder

Kuhusu ku work harder ngoja nikupe mfano

Boschmann amp yenye inatoa 65w at ohms load kwa channel nne ukiweka load za 4ohms kwenye hizo channel nne utapata jumla ya 260w

Ukitumia spika za 2ohms utapata Mara mbili ya hicho kiwango ndipo amplifier inaweza chemka kirahisi Sana hata mosfet za power supply sababu utakuwa unavuta umeme mwingizaidi

Kuhusu kuwa stable at load flani inategemea na technology iliotumika undia hio amp
Watu wanapiga mziki kwenye sherehe , concept mbali mbali na spika zinaungwa for the final load of 2ohms watu wanakula burudani Hadi asubuhi

Unazijua class H vizuri
 
Jambo lingine msingi sio uwezo tu wa kusukuma Ohms ndogo, vipi kuhusu ubora, THD ikoje?. Mimi siko familiar sana na amplifiers za magari so huko siwezi comment sana.

Ila kwa hizi za muziki wa nyumbani niko well informed. Maana sio swala tu la uwezo wa amplifier na speaker kuproduce sound, ila ni sound bora kiasi gani.

Mimi binafsi nilitoka kwenye HTIB, nikahamia kwenye separates, ni expensive move ila unapata mziki mzuri. Pia for music listening situmii kabisa subwoofer/active ones. Ni pure stereo ndo napenda.
 
Mziki wa gari majumbani na sehemu pa vinywaji chakula nk nimefunga Sana

Ni rahisi Sana funga mziki wa gari nyumbani au popote penye 220VAC

Current unayosema 40A je umezidisha na 12v ukajua Ni watts ngapi?

Huwezi sema 12v 40A Ni kubwa kuliko 50v 20A

Umeme wa majumbani Ni mwingi Sana na sio Ampere 13 Ni umeme mwingi Sana ndo Mana watu wanafunga dual 18inch bass spika na mids zake Ni wewe tu kwenye gari huwezi hata uwe na inverter kubwa kiasi gani ..altenator haiwezi fua umeme huo thou Kuna after market zinaweza fua Hadi 200A

Turudi kwnye mziki wa gari

Amplifier ya gari inahitaji 12vdc -14.6VDC as input japo amplifier hazitumii volt hizo ,, zinaenda ongezwa ndani kwnye dc to DC converter

Unachohitaji Ni power supply inayotoa 12v na current ya kutosha kwa hio boschmann kwa nyumbani normal 30A is enough power supply zimejaa tele 20,30,50,80A zipo Bei Hadi laki plus

Hili la kuwepo kwa power supply zenye current nyingi nmekuja kufahamu now kua zipo

Je nje ya hap ungewezaje kuweka transfoma ndogo ya kawaida ika kupa hizo currents ? Definitely haiwezekani
Thus kwenye maelezo yangu nasema issue ni power supply na sio HAIWEZEKAN!
 
Je hizi busta utaziwasha na nini? Ok tuseme uweke transformer ili ipunguze voltage then ugeuze ac hizo kwenda dc hi ni rahisi na inawezekana ila je hiyo transformer yako itakupa 40+ current? Definitely inawezekana kuwa ngumu kidogo
Ndio maana inawezekana kua vigumu kidogo kutumia system hizi kwenye nyumbani

[mention]Sambinyakwe kitololo [/mention]
Hi ni line yangu ya mwisho kimaelezo mkuu
Hakuna sehemu nasema haiwezekan
Kwasababu hata mimi nimeona pia
Ila lazima ac transfom iwe 9VAC
Ili zikigeuzwa zifike kuanzia 12
Wakati huo lazima secondary coil iwe nene kutengeneza current nying kwenye rectification

Pia sikua najua kam kuna power supply za dc hadi Wicalu aliponiambia chimbo zilipo.
Na je nje ya hapo ikiwa mtu amesikosa inakuaje? Ndio ilikua point yangu but kusema HAIWEZEKANI kwenye dunia ya leo iliyosheheni technology ni kujidanganya
 
Jambo lingine msingi sio uwezo tu wa kusukuma Ohms ndogo, vipi kuhusu ubora, THD ikoje?. Mimi siko familiar sana na amplifiers za magari so huko siwezi comment sana.

Ila kwa hizi za muziki wa nyumbani niko well informed. Maana sio swala tu la uwezo wa amplifier na speaker kuproduce sound, ila ni sound bora kiasi gani.

Mimi binafsi nilitoka kwenye HTIB, nikahamia kwenye separates, ni expensive move ila unapata mziki mzuri. Pia for music listening situmii kabisa subwoofer/active ones. Ni pure stereo ndo napenda.
0.05% THD Ni Bomba kabisa,, unaangalia amp unardhika na specs zake even at low impedance Kisha ndo unafanya manunuzi

Unatumia spika za aina gani
 
Je hizi busta utaziwasha na nini? Ok tuseme uweke transformer ili ipunguze voltage then ugeuze ac hizo kwenda dc hi ni rahisi na inawezekana ila je hiyo transformer yako itakupa 40+ current? Definitely inawezekana kuwa ngumu kidogo
Ndio maana inawezekana kua vigumu kidogo kutumia system hizi kwenye nyumbani

[mention]Sambinyakwe kitololo [/mention]
Hi ni line yangu ya mwisho kimaelezo mkuu
Hakuna sehemu nasema haiwezekan
Kwasababu hata mimi nimeona pia
Ila lazima ac transfom iwe 9VAC
Ili zikigeuzwa zifike kuanzia 12
Wakati huo lazima secondary coil iwe nene kutengeneza current nying kwenye rectification

Pia sikua najua kam kuna power supply za dc hadi Wicalu aliponiambia chimbo zilipo.
Na je nje ya hapo ikiwa mtu amesikosa inakuaje? Ndio ilikua point yangu but kusema HAIWEZEKANI kwenye dunia ya leo iliyosheheni technology ni kujidanganya
Power supply zipo nyingi sana

Hata desktop PSU unaangalia yenye specs unataka Nina ya 12v 20A hii inaweza beba amp mbili fresh zile single channel zinazokujaga na sabufa za kichina zenye amp yake hapo hapo 10inch sub, zile kubwa sijawah jaribu mbili kwa psu hio ila Moja uhakika
 
Owky Sawa Ahsante
 
Mkuu una ufahamu wowote wa namna speaker inavyofanya kazi au umenijibu tu?, embu fanya research yako vizuri. Soma vitabu na pitia mitandao kisha turudi hapa kujadili

Sent from my SM-N916S using JamiiForums mobile app
View attachment 2551470
Cnet ni one of the reputable website ambayo wataalam mbalimbali hufanya reviews za new amplifiers/AVRs/BDPs etc kila zinapotoka. Wanachambua na kutoa overall best product.

Sasa impedance ya speakers haiwi constant kama unavyosema wewe. It changes with the frequency inayokuwa produced.

Sent from my SM-N916S using JamiiForums mobile app
 
Ngoja nimeze panadol kwanza maana shule ya humu ni balaa 😁😬😬

kelphin Nimeona mizigo aisee lakini naona sitatoboa kwa njia ya separate though nilikua naipenda na ntabaki kuihusudu, for now ngoja nipate tu Sony Soundbar moja hivi nimeipenda kuanzia muonekano na bei.

Kipindi nikiwa sina mambo mengi ntaanza kukusanya ayo ma amplifier na ma pre amp😁😁😁
 
Preamplifier mkuu. Hii huwa inatumika pamoja na power amplifier. Pre amplifier inakuwa na Volume knob, inakuwa na selector/sources mfano cd, tuner, dvd etc. Nyuma unaweza chomeka cables mbalimbali toka kwenye tv, cd, tuner etc.

Zinakuwa amplified kidogo kabla ya kuruhusiwa kwenda kwenye power amplifier/hii haina sehemu ya kuongeza volume wala kuchagua source.

Kwenye picha hapo, ya juu yenye knob ya sauti ndo preamplifier na hiyo ya hini ndo power amplifier
View attachment 2545279View attachment 2545280
niliona.moja dodoma mitaa ya sabasaba, brand ya Sony ES series
 
Ngoja nimeze panadol kwanza maana shule ya humu ni balaa 😁😬😬

kelphin Nimeona mizigo aisee lakini naona sitatoboa kwa njia ya separate though nilikua naipenda na ntabaki kuihusudu, for now ngoja nipate tu Sony Soundbar moja hivi nimeipenda kuanzia muonekano na bei.

Kipindi nikiwa sina mambo mengi ntaanza kukusanya ayo ma amplifier na ma pre amp😁😁😁
Nibalaa mzee wenzangu😅

Tuione iyo sound bar
 
Back
Top Bottom