Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg


Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
ushauri wangu kama unataka ufaidi vizuri hiyo power amp tafuta graphic equlizer na pre amp, mimi natumia vyote hivyo,nina eq ya sansui 10 band kwa ajili ya mziki wa sebuleni na kenwood 7band,natumia na kichwa cha yamaha ex600 kama pre amp kwa ajili ya chumbani, natumia format ya bi amp katika power aplifier (left bass,right mid&hi) kwa mziki wa chumbani, maana spika zangu ni bi wired(separate bass line na mid&hi)
Equalizer unachomeka kwenye tape in?, naamanisha wapi unailink kwenye preamplifier yako?

Sent from my SM-N916S using JamiiForums mobile app
 
nunua ht ya sony, ila.kama.uko vizuri, nunua avr, tower spiker na sorround zake na powered sub
Yeye anazungumza kuhusu laki 4 wewe unamwabia kuhusu Avr mkuu?

Avr mpya ya 5.1 tu ni zaidi ya milioni...hapo hujaja kwenye Speakers na sub... going separates is very expensive and it's not for the weak. (Unless mtu aende kwenye mtumba, ingawa nako pia ni expensive for separates)
 
Yeye anazungumza kuhusu laki 4 wewe unamwabia kuhusu Avr mkuu?

Avr mpya ya 5.1 tu ni zaidi ya milioni...hapo hujaja kwenye Speakers na sub... going separates is very expensive and it's not for the weak. (Unless mtu aende kwenye mtumba, ingawa nako pia ni expensive for separates)
hahahaa, mdogo mdogo anafika, na anakamilisha sound aitakayo
 
Mkuu ni nini kinasababisha redio kulia kama inamafua hivi wakat ikidunda yan ile bes ikigong kwa ndan unaskia km inagong kit kinaton kmlion km kukwaruz wahun wanasem inamafua… hii shid inakua n nn
 
Mkuu ni nini kinasababisha redio kulia kama inamafua hivi wakat ikidunda yan ile bes ikigong kwa ndan unaskia km inagong kit kinaton kmlion km kukwaruz wahun wanasem inamafua… hii shid inakua n nn

Inategemeana
Mala nyingi hua ni circuit components hazijakaa sawa
Inawezekana zimelegea
Wakati mwingine huenda Hata speker haijakaa vizuri
Ingawa sio mala nyingi kua n spika
Zaidi hua ni circuit components hazijakaa vizuri

Je Naweza iona aina ya subwoofer
 
Inategemeana
Mala nyingi hua ni circuit components hazijakaa sawa
Inawezekana zimelegea
Wakati mwingine huenda Hata speker haijakaa vizuri
Ingawa sio mala nyingi kua n spika
Zaidi hua ni circuit components hazijakaa vizuri

Je Naweza iona aina ya subwoofer

hapo kidogo nimekuelew maan hua sio mara zote inalia na wakat ikilia nikikaa pale kweny spik nakua nahisi n waya ndan unagongana na ule mshindo wa spika ikiend mbele na kurud …ni sound bar ya sony S700RF kuna mda unaisikia na kuna mda huiskii
 
unaweza, mosty ya satelite speaker z mchina zina ohms sawa
Asante, na je Kuna speaker ambazo zinabass nzuri inayojitegemea? Subwoofer yangu ina spekaer 5 lakini zote Zina cheza kama tweeter tu hazina bass, Bass inatoka Moja kwa Moja kwenye Radio yenyewe. Nilikua nataka nifaham kama Kuna speaker ambazo angalau Bass yake ni nzuri ambayo ikiungana Ile inayotoka kwenye radio itatoa kitu kizuri
 
Asante, na je Kuna speaker ambazo zinabass nzuri inayojitegemea? Subwoofer yangu ina spekaer 5 lakini zote Zina cheza kama tweeter tu hazina bass, Bass inatoka Moja kwa Moja kwenye Radio yenyewe. Nilikua nataka nifaham kama Kuna speaker ambazo angalau Bass yake ni nzuri ambayo ikiungana Ile inayotoka kwenye radio itatoa kitu kizuri

Tweeter haiwezi kukupa low freq(bass) kwasababu zina watts chache
Ukitaka sounds yenye bass kavu + midbass basi ni HIFI system ...ya 2.1 au na kadhalika
Ukitaka kuzifahamu ingia google andika 2.1 HIFI sounds systems utaziona
Ila subwoofer itatoa low ile bass tu na hakuna zaidi ya hapo
 
Back
Top Bottom