Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg


Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Hapa ndio hasa mnapopishana, jamaa wanazungumzia name brands ila kwa kipato cha wengi hatuzimudu hizo redio za Klispch, SVS ama sijui Polk Audio. Those are indeed expensive.

Ila kwa level yetu wengi ya miziki ya 200K-1000K Sony huwa ndio mtawala wa sound arena. JBL amekuja on top of Sony kwa affordability ila quality still hawajaachana sana.

Ila tukija in terms of perfomers ndio tunagundua kumbe kuna underdogs ambao wanaweza kuwazidi hata giants kwa perfomance ndio tunakutana na watu kama Kodtec. Hatuongelei ushabiki ila kwa music enthusiasts kama mimi nimesikiliza sound nyingi sana. Nikisikia mziki wa kweli naujua 😂😂😂 regardless ya brand name.

Kodtec wanaweza kupitia hizo speakers zao za subwoofer wanaweza kutengeneza best sounding bass speakers. Ukiniambia tofauti ya quality ya bass ya JBL na hawa Kodtec ntakwambia ni almost unnoticed ila JBL anaweza kuwa na crispy highs kumzidi Kodtec.

Ukija kwa Sony technically bass production ya Kodtec iko vizuri kuliko mule. Bei sasa ndio utacheka maana Kodtec haina jina sokoni kama Sony ni ngumu kumshawishi mtu anayependa name brands ila music enthusiast can easily tell the difference.
mkuu unafahamu maduka ya kodtec subwoofer unisaidie
 
kama uko kko nenda karibia na jengo la simba karibu na duka.la Lampard electrinics, shuka maduka ya ground floor au kama.unaenda mnazi mmoja barabara msimbazi kabla ya kitu cha mafuta total kama sikosei, upande kwa kushoto
 
Wakuu habari,naomba kuuliza kuhusu subwoofer yangu aina ya Seapiano ikiwa inaongea twita moja kunasikika ka kelele kwa mbali kanakolia siiiiii, hv shida itakuwa nn hapo kwa uzoefu wenu
 
Kelphin na Wataalamu wengine wa music systems. Mimi nina bajet ya 1.5 M, nichukue music sound gan, naombeni ushauri wenu.

1. Wenye Souti iliyochujika.
2. unapopiga vyombo vyote vinasikika.
3. Uwe unatema kweli, nikifungulia chumba kinatetema.
 
Inategemeana
Mala nyingi hua ni circuit components hazijakaa sawa
Inawezekana zimelegea
Wakati mwingine huenda Hata speker haijakaa vizuri
Ingawa sio mala nyingi kua n spika
Zaidi hua ni circuit components hazijakaa vizuri

Je Naweza iona aina ya subwoofer
Hata langu lilianza hivyo,saizi linakoroma.
 
Kelphin na Wataalamu wengine wa music systems. Mimi nina bajet ya 1.5 M, nichukue music sound gan, naombeni ushauri wenu.

1. Wenye Souti iliyochujika.
2. unapopiga vyombo vyote vinasikika.
3. Uwe unatema kweli, nikifungulia chumba kinatetema.
Chukua min HiFi system hizi za kisasa. Ukipata ile yenye spika 3 (moja ni Sub woofer) nadhani itakufaa.
 
habari mkuu, nina speaker system (rich sound) inshida ya earth, yaani ukiwa na contact nayo tu kwenye metal lazima urushwe. nini tiba ya hii kitu, nipo mbali na mafundi. yaani nikiipima earth na tester kwenye extension cable taa haiwaki. ila nikipima kwenye sound system yaa ya tester inawaka.
 
Back
Top Bottom