Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg


Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Nina banda la kuonyesha mpira
Wananzengo wanasumbua wanataka sauti kubwa na sio spika za tv

Ninunue sub woofer gani imara na ya bei nafuu bila kujali sana quality ya sound
Maana hii ni kwaajili ya kuwasikiliza wachambuzi na watangazaji wa mpira

Maoni yenu tafadhali
Mkuu hapo labda utafute hiz speakeer kubwa za kati
Subwoofer utaziumiza tu
 
Aisee nimekupata Sana mtaalam na kweli bongo tuko nyuma Sana ya wakati kwenye maswala haya ya midundo, nafikiri pia swala la kipato linachangia. Ila vipi man nataka nichukue hili dundo SONYView attachment 2616547 la mtumba umelionaje maana nimechoka na masabufa machina haya.
Yess ziko pow sana mkuu
Sema tu ni za mtindo wa kizamani ila sounds yake ni safi
Nankitu pow ni kua inawezekana kuweka Bluetooth pia
 
Aisee nimekupata Sana mtaalam na kweli bongo tuko nyuma Sana ya wakati kwenye maswala haya ya midundo, nafikiri pia swala la kipato linachangia. Ila vipi man nataka nichukue hili dundo SONYView attachment 2616547 la mtumba umelionaje maana nimechoka na masabufa machina haya.
Nafikiri litapiga fresh ila design-wise na functional-wise ni la kizamani.

Mziki wa kisasa ambao utakuwa rahisi kwako kuishi nao ungekuwa ni kupata Powered Speakers (option no 2 niliyoielezea pale juu).

Ila pia inabidi pia na mfuko wako uwe umechangamka.

Kiukweli kama unataka mziki wa kweli, (nazungumzia mpya not used), kimaskini sana inabidi uwe na kuanzia 1.5m na kuendelea. Na kwa bahati mbaya Bongo hapa hutoupata madukani.

Kwenye used sina uhakika napo, ila maybe ndio utapata kwa hela ya kawaida kidogo. Ingawa kwenye used utapata za kizamani.

Music is an expensive hobby kwa kweli.
 
Kwenye audio system kuna kitu kinaitwa (equlizer)
Hapa ni sehemu ambayo unatengeneza music usikike kwa (frequenc) tofauti tofauti
Ukiiseti ukiwa chumbani ni tofauti na ukiseti ipige kwenye sebule
Ile hali yakuchange freqnc ndio kazi ya equlizer
Lakini sasa humu kwenye home theater wana rahisisha kidogo kiuchache kukuwekea hizo freqnc tofauti ili ukitaka kuitumia sehem nyingine tofaut na nyumbani uchague tu mwenyewe
Kwahyo kifupi unapoipgia seating room ni tofauti na kwenye ka getton au cinema room!
Nazungumzia setting ya home theatre ambayo tayari imeshasetiwa.
Ni aina gani ya setting unapiga mziki ambao Ni mzuri?
Bila kujali upo sebuleni au chumbani
Rocky,
Sterio,
Dance,
Pop,
Jaz,
Studio,
Stadium,
Rhumba,
SAMSUNG HOME THEATRE,,
setting ipi hapo unatoa music mwanana?
 
Nimekupata vyema Sana mtaalam na sijui kwanini siku hizi nayachukia sana haya mabufa ya mchina, nimeuza sea piano sasa hivi naziwinda sana hizi Hi Fi za mtumba.. kuna hili dude la SONY hapa vipi unazipata hizi, nisijeingia chaka Mzee..
View attachment 2616548


mcheki huyu jamaa ana vinu vingi kama hivyo
 

Attachments

  • Screenshot_2023-05-11-14-00-19-54_a23b203fd3aafc6dcb84e438dda678b6.jpg
    Screenshot_2023-05-11-14-00-19-54_a23b203fd3aafc6dcb84e438dda678b6.jpg
    201.3 KB · Views: 26
Nazungumzia setting ya home theatre ambayo tayari imeshasetiwa.
Ni aina gani ya setting unapiga mziki ambao Ni mzuri?
Bila kujali upo sebuleni au chumbani
Rocky,
Sterio,
Dance,
Pop,
Jaz,
Studio,
Stadium,
Rhumba,
SAMSUNG HOME THEATRE,,
setting ipi hapo unatoa music mwanana?
hizo zote auto eq zinakuwa zinafanya kazi vizuri kulingana na jinsi mziki ulivyorekodiwa studio,mfano hiyo stadium ina ina echo,hivyo ukiieeka kwenye mziki ambao tayari una echo,echo inakuwa juu zaidi na hivyo kupoteza ladha
 
Nazungumzia setting ya home theatre ambayo tayari imeshasetiwa.
Ni aina gani ya setting unapiga mziki ambao Ni mzuri?
Bila kujali upo sebuleni au chumbani
Rocky,
Sterio,
Dance,
Pop,
Jaz,
Studio,
Stadium,
Rhumba,
SAMSUNG HOME THEATRE,,
setting ipi hapo unatoa music mwanana?

Zote ni NZURI!
Ila inategemeana na aina ya nyimbo unayosikiliza
2 inategemeana na ukubwa wa eneo la kupigia
3 ni wewe ndio unaamua na kupendeza na aina furani.. kulingana na usikivu wake.
Kwa wepesi niseme tu zote nzuri
 
Nazungumzia setting ya home theatre ambayo tayari imeshasetiwa.
Ni aina gani ya setting unapiga mziki ambao Ni mzuri?
Bila kujali upo sebuleni au chumbani
Rocky,
Sterio,
Dance,
Pop,
Jaz,
Studio,
Stadium,
Rhumba,
SAMSUNG HOME THEATRE,,
setting ipi hapo unatoa music mwanana?
Samsung home theatre kawaida nilikua naweka stereo... Inabalance sound nyingi.

But you can go to a specific tune kutegemea na music unaopiga kwa wakati huo. If ni pop weka pop if ni rhumba weka rhumba itakupa ladha ya bit, mdundo, chombo kwa chombo....

And hakuna auto hapo..... ni chaguo lako
 
Samsung home theatre kawaida nilikua naweka stereo... Inabalance sound nyingi.

But you can go to a specific tune kutegemea na music unaopiga kwa wakati huo. If ni pop weka pop if ni rhumba weka rhumba itakupa ladha ya bit, mdundo, chombo kwa chombo....

And hakuna auto hapo..... ni chaguo lako
Sawa mkuu shukran sn
 
Zote ni NZURI!
Ila inategemeana na aina ya nyimbo unayosikiliza
2 inategemeana na ukubwa wa eneo la kupigia
3 ni wewe ndio unaamua na kupendeza na aina furani.. kulingana na usikivu wake.
Kwa wepesi niseme tu zote nzuri
Oy mtaalam kuna mdau ananishauri nichukue hii PANASONIC vipi Kwa ujuzi wako hii ni home thietre au!? Na kimziki inapiga vizuri!!?
IMG-20230516-WA0006.jpg
 
Back
Top Bottom