Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg


Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
oooh so hpa hta ukitaka kuunda system ya sound for home use hasa kutumia speakers za gari basi ni vyema uwe na 2 amps sio moja for mids(stereo amp) and other one monoblock for subwoofer right?

so kma mono ni njia 1 , unakuta mono 1 imbeba sub hta zaidi ya 2

pale inakuwaje in terms of performance??
Unakuta una monoblock inasoma 800w @1ohms

Ukiweka spika ya 4ohms hautapata max power ya hio amp , ndo unakuta mtu anaweka spika mbili in parrallel za dual 4ohms ili kupata 1ohms


Ni maamuzi yako unaweza tumia mono hata kwa spika ndogo tu in watts na ikawa 4ohms, sema utakuwa umelipia amp yabei ghali ambayo hutumii Bora upate 2ch amp nibei Chee kidogo inawafaa wasio na matumizi makubwa
 
Unakuta una monoblock inasoma 800w @1ohms

Ukiweka spika ya 4ohms hautapata max power ya hio amp , ndo unakuta mtu anaweka spika mbili in parrallel za dual 4ohms ili kupata 1ohms


Ni maamuzi yako unaweza tumia mono hata kwa spika ndogo tu in watts na ikawa 4ohms, sema utakuwa umelipia amp yabei ghali ambayo hutumii Bora upate 2ch amp nibei Chee kidogo inawafaa wasio na matumizi makubwa
Parralel ya 4ohms si unapata 8ohms mkuu, sasa huoni hiyo amp itakuwa ndogo kusukuma 8ohms? Hiyo 800w @1ohms kwa 2ohms si ni sawa na 400watts ,na kwa 4ohms si ni sawa na 200watts?
 
Parralel ya 4ohms si unapata 8ohms mkuu, sasa huoni hiyo amp itakuwa ndogo kusukuma 8ohms? Hiyo 800w @1ohms kwa 2ohms si ni sawa na 400watts ,na kwa 4ohms si ni sawa na 200watts?
Parrallel ya 4ohms unapataje 8ohms mkuu afu series utapata ngapi Sasa?


Parrallel ya 4ohms Ni 2ohms

Na kwenye maraftari ndo hio hesabu uliotoa ila uhalisia 800w at 1ohms, Basi @2ohms sio 400w Ni zaidi ila haitaikaribia Sana 800w ..inaeza kuwa somewhere 600w


Amp ya transitor pia inayotoa 100w at 4ohms load ukiweka spika ya 8ohms 100w kwenye amp hio ..usidhani itakuwa inapokea max 50w Kama hesabu inavosema twice a load half a power NO
 
Nataka niAndae 200K ninunue mdundo mkali mzki mkubwa sound ya kueleweka je ni subwoofer gan nzuri kwa hy budget hii hometheatre yngu ntk niiuze haina bluetooth gademuuni

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu yani 200k ndio unataka ununue Mdundo mkali na mziki mkubwa na sound ya kueleweka, sifa hizo zote ndo kwa 200k serious?

Kwani hiyo Home theatre yako ni ya kampuni gani na ina ukubwa gani maana kumiliki tu huo mziki kungekupa taswira kuwa kwa 200k utapata mziki wa Aina gani
 
Mkuu yani 200k ndio unataka ununue Mdundo mkali na mziki mkubwa na sound ya kueleweka, sifa hizo zote ndo kwa 200k serious?

Kwani hiyo Home theatre yako ni ya kampuni gani na ina ukubwa gani maana kumiliki tu huo mziki kungekupa taswira kuwa kwa 200k utapata mziki wa Aina gani
Ni sony ya watts 100 mkuu
Kwa makisio yko redio gan kali mkuu na budget ipi
 
Nina Soundbar ya JBL sasa hivi haiconnect kwenye Screen ya TV na Decoder ya DSTV kupitia HDMI, tatizo linaweza kuwa ni nini?
 
Back
Top Bottom