Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg


Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Kingine Mkuu Mimi natafuta kasystem portable ambayo Haina manyaya nyaya Wala vispika vingi viwe viwili vikizidi vitatu tu iwe na Bluetooth nataka Kwa ajili ya Tv tu nienjoy nkiangali movie .......... what is your recommendations on this

Sound bar ya wireless itakua chaguo lako namba1
Na kwakua unataka kwa matumizi hayo basi hata ile ya watts 300 hivi bado ni nzuri kwako
Ufikapo dukani sema sound bar za wireless
Kisha angalia features zake
Mfano
HDMI ARC
Bluetooth
IMG_0788.jpg



Kadhalika…

Ila ikiwa budget yako ni ndogo
Unaweza tafuta sound zinaitwa all in one
Yaan bass na satellite speaker zake(twiter) zinakua kwenye box moja la kusimama
IMG_0787.jpg

Karibu..
 

Attachments

  • IMG_0787.jpg
    IMG_0787.jpg
    15.9 KB · Views: 20
Nahitaji kusikia mziki mzuri, kelphin kwa bajeti ya laki 3 mpaka 5 nisaidie maelekezo basi, na pia nasikia jbl ni kampuni bora sana kwa kutengeneza vinu, natanguliza shukrani

Ikiwa unatak mziki mzuri na mkubwa pia basi
Twende na kodtek hi
IMG_0789.jpg

Na uzuri [mention]Extrovert [/mention] aliwahi sema kua wana duka lao special k/koo( mimi sijawahi fika)
Ila pia kwa muziki wa kawaida na wastani basi chukua sound bar ya 2.1



Inakuja na watts 240! Na nzuri pia

Ni kweli jbl wako vizuri saana tena sana tu
Ila proce zao hua juu pia..
 
Sound bar ya wireless itakua chaguo lako namba1
Na kwakua unataka kwa matumizi hayo basi hata ile ya watts 300 hivi bado ni nzuri kwako
Ufikapo dukani sema sound bar za wireless
Kisha angalia features zake
Mfano
HDMI ARC
Bluetooth
View attachment 2873482


Kadhalika…

Ila ikiwa budget yako ni ndogo
Unaweza tafuta sound zinaitwa all in one
Yaan bass na satellite speaker zake(twiter) zinakua kwenye box moja la kusimama
View attachment 2873483
Karibu..
Ahsante Mkuu.....je hiyo soundbar ya watts 300 Ina base
 
Nahitaji kuiweka kwenye Sp 1002 kama inayo onekana kwenye pichaView attachment 2873219

Sawa kitu chakwanza utahitaji kuitoboa happ mbele ili uweze kuifitisha mp3 yako

Nb inahitaji umakini kwakua hapo ndipo show ya subwoofer yako ilipo
Ukimaliza itabidi uzingatie yafuatayo

Soma kwa makini
IMG_0790.jpg

Mp3 hizi hua na crip tatu
Ya umeme
Ya signal out
Ya signal input

Ikiwa redio yako iliwahi kua na mp3 awali basi umeme uleule ulioingiza pale utauchomoa na kuleta kwenye hi mpya unayoweka (zingatia +_ mark)
Hivyo hakikisha + inaunga kwenye waya nyekundu na negative au ground inaunga kwenye waya mweusi

Ile crip inayotoa muziki yaan R,L out unga na zile waya zilizokua zinatoa mziki hapo (kwenye mp3 ya zamanı)kupeleka kwenye subwoofer circuit yako
Kisha ile ya aux inayotoka kule kwenye zile pin za nyuma ingiza kwenye aux input


Kwa kufanya hivyo kazi itakua imekwishs

NB
Zingatia waya wa +_ kabla ya kuingiza kwenye mp3

Ikiwa haitafanya kazi au ukikwama nitaarifu
Na nitumie namba yako pm..
 
Ndio dada
Mfano ni hapaView attachment 2873492
Hiyo square iliyolala ni system yake ikiwa na speaker zake pia na control zake kabisa
Kifupi hiyo ndio redio yako
Afu hilo box jeusi nyuma ni speaker yake ya bass





Unapenda mdundoo[emoji23][emoji23]
Saaana mno je brand gani ni nzuri nkimaanisha quality haijalishi Bei as long as ni best quality Bei sio shida
 
Sawa kitu chakwanza utahitaji kuitoboa happ mbele ili uweze kuifitisha mp3 yako

Nb inahitaji umakini kwakua hapo ndipo show ya subwoofer yako ilipo
Ukimaliza itabidi uzingatie yafuatayo

Soma kwa makiniView attachment 2873489
Mp3 hizi hua na crip tatu
Ya umeme
Ya signal out
Ya signal input

Ikiwa redio yako iliwahi kua na mp3 awali basi umeme uleule ulioingiza pale utauchomoa na kuleta kwenye hi mpya unayoweka (zingatia +_ mark)
Hivyo hakikisha + inaunga kwenye waya nyekundu na negative au ground inaunga kwenye waya mweusi

Ile crip inayotoa muziki yaan R,L out unga na zile waya zilizokua zinatoa mziki hapo (kwenye mp3 ya zamanı)kupeleka kwenye subwoofer circuit yako
Kisha ile ya aux inayotoka kule kwenye zile pin za nyuma ingiza kwenye aux input


Kwa kufanya hivyo kazi itakua imekwishs

NB
Zingatia waya wa +_ kabla ya kuingiza kwenye mp3

Ikiwa haitafanya kazi au ukikwama nitaarifu
Na nitumie namba yako pm..
Nashukuru, Nimekupata vema, ngoja ninunue hiyo mp3 nifanye mambo.
 
Back
Top Bottom