Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg


Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Ikiwa unatak mziki mzuri na mkubwa pia basi
Twende na kodtek hi
View attachment 2873486
Na uzuri [mention]Extrovert [/mention] aliwahi sema kua wana duka lao special k/koo( mimi sijawahi fika)
Ila pia kwa muziki wa kawaida na wastani basi chukua sound bar ya 2.1



Inakuja na watts 240! Na nzuri pia

Ni kweli jbl wako vizuri saana tena sana tu
Ila proce zao hua juu pia..
Asante sana, chambua basi hizo za jbl juzi nilikuwa nazurula sehemu nikaona muziki wa mil 7,, nyie kuna watu wanaishi
 
Preference yako ni nini hasa kwenye mziki? Huo mziki pia sio zile LG og ya mkorea mwenyewe,huyo ni mchina asiye na viwango sana, ukimweka na sea piano sp 1002,anamkalisha hata kwa kuchuja mziki tu
Binafsi yangu kwenye redio cha kwanza uwa ni ule mkito pamoja na sauti. Ila nmekuelewa. Kabla ya kufanya maamuzi ya kununua music appliances kuna haja ya kuja pm kwako na wataalam wengine kwa ushauri na mapendekezo. I salute you
 
Binafsi yangu kwenye redio cha kwanza uwa ni ule mkito pamoja na sauti. Ila nmekuelewa. Kabla ya kufanya maamuzi ya kununua music appliances kuna haja ya kuja pm kwako na wataalam wengine kwa ushauri na mapendekezo. I salute you
Ila huyu mchina anazingua sana. Kila mahala yupo, wale wapenzi wa OG inatubidi kuhangaika sana
 
Ila huyu mchina anazingua sana. Kila mahala yupo, wale wapenzi wa OG inatubidi kuhangaika sana
Og kwa sasa uwe na kisu kikali na uanaweza kuwa na hicho kisu kikali na bado bongo usipate maaana kila kona pametapakaa mchina feki,hapo kenya ndio wana vitu vya maaana.,kama nimmoderate budget hamia kwenye mtumba ambapo ndipo nilipoangukia mimi
 
Og kwa sasa uwe na kisu kikali na uanaweza kuwa na hicho kisu kikali na bado bongo usipate maaana kila kona pametapakaa mchina feki,hapo kenya ndio wana vitu vya maaana.,kama nimmoderate budget hamia kwenye mtumba ambapo ndipo nilipoangukia mimi
Mkuu ntakucheki kwa mwongozo.
 
Mkuu kelphin , kuna Subwoofer, yenye single nob, ina display LED lights kwenye control circuit mbele tu, Digital display yake inabaki off na hakuna mandishi yanatokea no out yeyote no base no, no mid,... licha ya (5v) kutoka kwenye transistor inafika vizuri, lakini taa tu ndio zinawaka.

Circuit
ina ic PT 2313L
na tda 7379

Kwa uzoefu wako mkuu unaweza kushauri nini hapo?
 

Attachments

  • IMG_20240126_213145_734.jpg
    IMG_20240126_213145_734.jpg
    884.6 KB · Views: 34
Sijapata juisikiza
Nmeona tu kwa njia ya mtandao..

UMEISIKILIZA?
Hivi mkuu hizi vizio sound bar mtumba zinazotangazwa na kuuzwa na baadhi ya watu zipoje??
Mimi nahitaji music mzuri mzito lakini mtulivu sio makelele hasa kwaajili ya kusikiliza classic music., kwaya zile zilizoimbwa kwa viwango vya juu kabisa, sauti zote nne zisikike, vyombo kiasi, maneno na matamshi..
Je ninunue aina ipi sielewi kabisa.
Nimekuwa kwenye dilemma kwa mwaka na nusu.

Ukienda kwa wauzaji wengi blablah tuu hawajui kabisa aina na ubora wa mziki. Wao kipimo chao ni midundo na makelele kwa kuweka manyimbo ya bongoflavour tuu au tuu miziki hii sijui amapiano sijui Nigeria..
Hiyo miziki haiwezi kutambulisha ubora wa muziki system maana haijarekodiwa kwa madhumuni hayo wala mpangilio wa sauti au vyombo.

Mtaalam tusaidie na sisi tunaopenda viwango nijue ninue aina ipi, na ukubwa upi kwa matumizi ya sebuleni nyumbani tuu.
Ndani nisikie mziki mzuri ninaotaka lakini nje wasipate kelele ya yeyote labda mdundo kwa mbaali.
Vizio, lq, sony, jbl na nyingine unazozijua wewe kama mtaalam eg 5.1ch, Watt's, sound bar au HiFi au home thietre.
Mimi huwa sipendi na huwa siangalii movie kabisa... Hivyo nataka viwango vya music and not movie.

Asante In advance. Utakachoshauri nitaenda straight dukani kununua bila kuhoji hoji au kuwa na mashaka.
 
Back
Top Bottom