Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg

Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Mkuu kelphin , kuna Subwoofer, yenye single nob, ina display LED lights kwenye control circuit mbele tu, Digital display yake inabaki off na hakuna mandishi yanatokea no out yeyote no base no, no mid,... licha ya (5v) kutoka kwenye transistor inafika vizuri, lakini taa tu ndio zinawaka.

Circuit
ina ic PT 2313L
na tda 7379

Kwa uzoefu wako mkuu unaweza kushauri nini hapo?
Pole kaka
hizo taa hua ziko connected parallel na voltage hivyo hazina uhusiano na display
Ila display hua ina ic yake inayojitegemea
Na tawezekana imepata shida kidogo
Hivyo basi ili iendelee kufanya kazi itabidi kutafuta
Either ic hiyo
Au display nzima kwa mafundi
Kinyume na hapo itabidi uibadili iende analogue
Hivyo itafaa uweke nob za kawaida na ununue Bluetooth ya kawaida pia

Nb wewe ni fundi?
 
Hi
Hivi mkuu hizi vizio sound bar mtumba zinazotangazwa na kuuzwa na baadhi ya watu zipoje??
Mimi nahitaji music mzuri mzito lakini mtulivu sio makelele hasa kwaajili ya kusikiliza classic music., kwaya zile zilizoimbwa kwa viwango vya juu kabisa, sauti zote nne zisikike, vyombo kiasi, maneno na matamshi..
Je ninunue aina ipi sielewi kabisa.
Nimekuwa kwenye dilemma kwa mwaka na nusu.

Ukienda kwa wauzaji wengi blablah tuu hawajui kabisa aina na ubora wa mziki. Wao kipimo chao ni midundo na makelele kwa kuweka manyimbo ya bongoflavour tuu au tuu miziki hii sijui amapiano sijui Nigeria..
Hiyo miziki haiwezi kutambulisha ubora wa muziki system maana haijarekodiwa kwa madhumuni hayo wala mpangilio wa sauti au vyombo.

Mtaalam tusaidie na sisi tunaopenda viwango nijue ninue aina ipi, na ukubwa upi kwa matumizi ya sebuleni nyumbani tuu.
Ndani nisikie mziki mzuri ninaotaka lakini nje wasipate kelele ya yeyote labda mdundo kwa mbaali.
Vizio, lq, sony, jbl na nyingine unazozijua wewe kama mtaalam eg 5.1ch, Watt's, sound bar au HiFi au home thietre.
Mimi huwa sipendi na huwa siangalii movie kabisa... Hivyo nataka viwango vya music and not movie.

Asante In advance. Utakachoshauri nitaenda straight dukani kununua bila kuhoji hoji au kuwa na mashaka.
Ahsante kwa kuniamini boss
Nmekusoma taratibu tena zaidi ya mala moja
Ila kwa maelezo yako naweza kusema nmekuelewa vizui

Je tuna budget ya shilling ngapi?
 
Hi

Ahsante kwa kuniamini boss
Nmekusoma taratibu tena zaidi ya mala moja
Ila kwa maelezo yako naweza kusema nmekuelewa vizui

Je tuna budget ya shilling ngapi?
Asante sana kwa kunielewa na kutaka kunisaidia. Una moyo wa kipekee sana.
Suala la bajeti nipo flexible ingawa sio kwamba nina uwezo hapana ila kitu nikikipenda na likawa hitaji hasa la moyo huwa napambana mpaka nikipate.

Mimi sina starehe yeyote zaidi ya kutulia nyumbani baada ya majukumu ya kikazi na kutamani kusikiliza huo music tuu na tv documentaries muda wa ziada.

Ukiniambia minimum price (cost) inaanzia hapa kwenda juu nitaelewa vizuri.
Au ukisema specifications zake kuanzia level hii na kuendelea nitakuwa okay. Huenda ninacho hicho kiasi au nitakiwa nitafute cha ziada its okay.

Pole kwa kukusumbua kwa maelezo marefu badala ya jibu halisi.
 
Usijali mkuu
Japo hua napata ukalasi kidogo kuamua setups ya muziko MOJAKWAMOJA kwakua hua naweza kushuka down sana ya upendavyo au nkaenda high sana
By the way kwa sound normal per low price twende na 2.1 sounds bar ya evvoli 240watts
Nadhani kwa budget kati ya 400k hadi 450 hivi tunapata
Ila ukiwa ulipenda kupata na surrounding sound kidogo basi twende na
DAV-DZ650 itakua bora sana kwako
Na ikiwa sawa zaidi pata DAV 950!

Ila kumbuka 650 na 950 zinatofautiana tu MUONEKANO wa speaker na sio muziki!
Zote zinakuja na 1000Watts!

Ila pia kuna baadhi ya subwoofer za kawaida ziko bomba pia
Na hapa nnaongelea kodtek KT2812

Zaidi ya hapa tu chek 2.0
Hizo ni redio bomba piaa ambazo hupiga ile stereo pure kabisa
Mfano wa LG zile xboom
Japo kwenye review haijapokelewa vizuri na wateja
Kuna toleo moja la 2.0 nipe muda nilifuatilie ila nadhani tajwa hapo juu ni best sana
 
Asante sana Ndugu.. Nimepata uelewa mkubwa najua walao nichague namna gani.. Ingawa bajeti yangu ninaweza kufikia 1.5m kushuka chini.
 
Asante sana Ndugu.. Nimepata uelewa mkubwa najua walao nichague namna gani.. Ingawa bajeti yangu ninaweza kufikia 1.5m kushuka chini.
Duhhh kwa hiyo budget mkuu ningekuwa Mimi ningedaka JBL BAR 500 WIRELESS au SONY SOUNDBAR 1000W WIRELESS au SAMSUNG SOUNDBAR HW-B67E/XL

Hapo unapata quality ya mziki uliokuwa unauongelea, kutokana na ufinyu wa budget nilishindwa kudaka mizigo ya calibre hizo nikaambulia VIZIO SB3651

Nikapata kitu kulingana na uwezo wangu na nikakubaliana na hali ila ningekuwa na kibunda ningeenda for the big sharks
 
Umenipa nguvu zaidi ya kimaamuzi. Ni ushauri mzuri sana. Nakushukuru nitaleta mrejesho nikifanikisha.
 
Og kwa sasa uwe na kisu kikali na uanaweza kuwa na hicho kisu kikali na bado bongo usipate maaana kila kona pametapakaa mchina feki,hapo kenya ndio wana vitu vya maaana.,kama nimmoderate budget hamia kwenye mtumba ambapo ndipo nilipoangukia mimi
Naomba nitajie machimbo ya kenya mkuu.
 
Back
Top Bottom