Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg


Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Hivi mkuu hizi vizio sound bar mtumba zinazotangazwa na kuuzwa na baadhi ya watu zipoje??
Mimi nahitaji music mzuri mzito lakini mtulivu sio makelele hasa kwaajili ya kusikiliza classic music., kwaya zile zilizoimbwa kwa viwango vya juu kabisa, sauti zote nne zisikike, vyombo kiasi, maneno na matamshi..
Je ninunue aina ipi sielewi kabisa.
Nimekuwa kwenye dilemma kwa mwaka na nusu.

Ukienda kwa wauzaji wengi blablah tuu hawajui kabisa aina na ubora wa mziki. Wao kipimo chao ni midundo na makelele kwa kuweka manyimbo ya bongoflavour tuu au tuu miziki hii sijui amapiano sijui Nigeria..
Hiyo miziki haiwezi kutambulisha ubora wa muziki system maana haijarekodiwa kwa madhumuni hayo wala mpangilio wa sauti au vyombo.

Mtaalam tusaidie na sisi tunaopenda viwango nijue ninue aina ipi, na ukubwa upi kwa matumizi ya sebuleni nyumbani tuu.
Ndani nisikie mziki mzuri ninaotaka lakini nje wasipate kelele ya yeyote labda mdundo kwa mbaali.
Vizio, lq, sony, jbl na nyingine unazozijua wewe kama mtaalam eg 5.1ch, Watt's, sound bar au HiFi au home thietre.
Mimi huwa sipendi na huwa siangalii movie kabisa... Hivyo nataka viwango vya music and not movie.

Asante In advance. Utakachoshauri nitaenda straight dukani kununua bila kuhoji hoji au kuwa na mashaka.
Budget yako ni kiasi gani? I have good news for you.
 
Budget yako ni kiasi gani? I have good news for you.
Nipo tayari kupambana endapo kuna kitu kizuri.. Naweza nisiwe na kiasi fulani muda huo lakini nikakitafuta kufuatana na uzuri wa bidhaa. Nipo flexible nikishindwa nitakwambia hiyo siwezi. Hivyo unaweza kunishirikisha ili mimi nijue naiweza au laa.
 
Hili tatizo limeanza majuzi tu

Sabufa langu main speaker inanguruma

Kuna saa inatulia haingurumi but baada ya muda linaanza kunguruma?

Je, tatizo ninini?

Mwanzo lilikua likinguruma kwa nadra tu lakin kuna siku nilizidisha volume hadi mwisho likanguruma sana hapo ndo ikazid kunguruma sasa hv ndo imekua changamoto yake...mziki unapga but ule mngurumo wa spika yake kubwa ndo unakera...ukiweka Pause ule mngurumo unaendelea tu.

Wajuzi hili tatizo ninini?
Peleka fundi akuwekee gundi kwenye spika. Gundi ikiachia spika inaanza kuvibrate hovyo. Ni gundi tu linatulia
 
Wakuu Naomba kuuliza kwa mafundi na wenye uzoefu, nina sound bar ya Vizio imepata itirafu katika harakati za kusafirisha

Nilikuwa nasafirisha kutoka Dar kwenda Kigoma ila kwenye kufungwa, ikawa imefungwa vibaya na hatimae kufika Kigoma ikiwa na shida

Ukiwa unapiga mziki ile bufa inatoa sauti ya Puuu Puuu Puuu as if imeachia au kulegea, nikajaribu kuulizia nikaambiwa speaker ikishakuwa hivo na hasa za sound bar ndio basi tena haitengenezeki ispokuwa natakiwa kubadirisha kabisa speaker

kelphin DreezyD98

Kwahiyo natakiwa kutafuta speaker inayofiti kwenye hiyo box yake kisha nichange, sasa nimeona nije na huku kupata ushauri kabla sijafanya maamuzi, je ni kweli haitengenezeki?
IMG_20240415_095736.jpg
 
Wakuu Naomba kuuliza kwa mafundi na wenye uzoefu, nina sound bar ya Vizio imepata itirafu katika harakati za kusafirisha

Nilikuwa nasafirisha kutoka Dar kwenda Kigoma ila kwenye kufungwa, ikawa imefungwa vibaya na hatimae kufika Kigoma ikiwa na shida

Ukiwa unapiga mziki ile bufa inatoa sauti ya Puuu Puuu Puuu as if imeachia au kulegea, nikajaribu kuulizia nikaambiwa speaker ikishakuwa hivo na hasa za sound bar ndio basi tena haitengenezeki ispokuwa natakiwa kubadirisha kabisa speaker

Kwahiyo natakiwa kutafuta speaker inayofiti kwenye hiyo box yake kisha nichange, sasa nimeona nije na huku kupata ushauri kabla sijafanya maamuzi, je ni kweli haitengenezeki?View attachment 2964141
Ichunguze hiyo spika kama imechanika
 
Back
Top Bottom