Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

Niulize chochote kuhusu Subwoofer na Sounds system

kelphin

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
9,872
Reaction score
16,319
Ikiwa inakusumbua,ikiwa unataka kufahamu chochote kinachokutatiza.

Karibu
images.jpg


Nieleze kidogo kuhusu subwoofer
Je, unataka kununua, basi zingatia haya.

Zipo za aina mbili old model na digital. Siyo majina hapana ,yaani inaweza kua rising,seapiano,codjec,aborder au vyovyote Ila itakua digital au old model.

Hizo digital ni Aina ya subwoofer ambayo inamuundo wakisasa ,mala nyingi utakuta Ina (nob) kivingilisho Cha sauti kimoja tu.

Ila kinafanya multipurpose, ukibonyeza hyo hiyo nob unaweza ongeza sauti ,kuongeza bass, na mid.
kifupi mambo yote ni in one button.

Faida yake ni kuwa, aina ya power supply yake Ni ilitaka ifanane na ya home theater(Ila haijawahi[emoji2][emoji2inakua na umeme mnyoofu kidogo.

Zinakua na music mkubwa na mdundo zaidi ni digital,yaani yakisasa,
lakini pia display yake ni LCD haitumii umeme mwingi.

Je utaijuaje?
Nob ya kuongezea sauti ni moja tu na zaidi utakuta button za menu na input inategemeana). Ukiigeuza nyuma ina kiplastic kidogo kilichozungushwa nati, yaani ikiwa italeta shida fundi huku nyuma hafungui mfuniko wote wa nyuma, hufungua ki plastic tu hapo nyuma ndio kimebeba card zoote na subwoofer.

Hasara zake
  1. Ikitokea imeharibu card yake hauwez kubadilisha ,sababu ndani Ina circuit Kama ya phone mafundi weeengi hawana(hatuna) technology yakuitengeneza kwahyo unaenda dukani unanunua Tena kard na si chini ya 40000.
  2. Ila ukifika unaipachika tu huangaiki.
  3. Inahitaji utulie ili uioperate maana inatumia single nob.
  4. Speaker yake ya bass huwekwa ohms ndogo ili idunde sana kwahiyo usipende kuweka sauti kubwa Sana kwa muda mrefu.

Aina ya pili ndio zile old model
Hizo zinaitwa dunda udundavyo ni nzuri kwenye uzuri wake. Yenyewe ukiingalia utakuta Ina nob yaani vile vyakuongezea sauti zaidi ya kimoja. Yaani cha master volume, bass, tweeter na mic, na ukivizungusha vinafika mwisho.

Yenyewe ndani power supply yake ni ya kawaida, inatumia mtransformer wake na diodes za kawaida. kisha umeme huingia kwenye capacitor ndio unaanza kusambazwa ndani. Yaweza kuwa Seapiano, Codjec Aborder au vyovyote. Ukiigeuza nyuma mfuniko wote unafunguka wa nyuma.

Faida yake
  1. ikizingua unaiweza kuirekebisha kiurahisi tu
  2. Zinavumilia sana
  3. Hata muziki upo pia
  4. Rahisi kuitumia
Hasara zake
  1. Display yake ni VFD kama ni seapiano hapa mbele inakioo,inavyoimba Kuna vitu vinacheza cheza kwenye kioo(hii ni kwa baadhi ya subwoofer)
  2. Muonekano wake ni wakizamani ikilinganishwa na hizi mpya

Soma hi pia [emoji1427]
Ndani ya subwoofer panya hupenda kuishi humo, huzaliana na kuleta hitilafu kwa kukata nyaya na kula speaker.
Waya wa speaker una chumvi chumvi hivyo akiingia hauachi.

Simple way jinsi ya kudhibiti
Pale kwenye tobo kuna ki corn cha duara huwa wanakipachika unaweza kukitoa kwa kufuata mpangilio ufuatao:

  1. Chukua maji ya moto kidogo na kitambaa, kichovye kitambaa kwenye maji kisha kikande kuzunguka mduara kwa dakika tano.
  2. Kisha chukua kisu, tumia ncha yake kuingiza pembezoni mwa mduara bila kuikwajua. Huku ukiinua kidogo kidogo kuzunguka corn nzima,ukisha kitoa kitoboe vitundu vidogo kukizunguka upande wa ndani(sio Huku uliko Kanda kwa maji).
  3. Ukisha kitoa chukua waya mgumu usuke upande wa ndani kuzunguka uwazi wa duara wote mule ulimotoboa, kisuke hakikisha unaacha vyumba vidogovidogo kiasi kwamba kinaweza kupita kidore kidogo tu.
  4. Paka gundi upande wa ndani, huku ulikokua unakanda na maji kisha kibandike tena kama kilivyokuwa.

NB: Hii ni kwazile subwoofer kama pichani hapo juu, ambazo hutolea upepo pembeni kwenye kiduara. Wale zinazotolea mbele chini ni habari nyingine.

***
Kiasi chake mtanielewaView attachment 1560194View attachment 1560195

Some updates,
Je, music system yako haina bluetooth na unataka kuongezea? Easy sana na inawezekana pia, kwa mafundi ninaweza kuwaelekeza.

Lakini pia music system yako ulipenda itoe mp5, yaani picture, video inawezekana pia[emoji3][emoji3].
Hususani wale wenye TV za kizamani yaani unachomeka flash disk yako kwenye subwoofer, unapata mdundo alafu kuna cable itatoka kwenye subwoofer hadi kwenye TV yako.

Stay here.
More good things are here.
Welcome.

View attachment 1921368
View attachment 1921369
 
Wakuu nawapa machaka
Just found this amazing item on AliExpress. Check it out!
TZS128,946.51 30%OFF | 110-220V 200W 100W Heavy Subwoofer Digital Power Amplifier Board Active Power Amplifier Board Hifi Pure Bass 1CH 4ohm 8ohm
46.28€ 17% OFF|110 220V 200W 100W Schwere Subwoofer Digitale Power Verstärker Bord Aktive Power Verstärker Bord Hifi Reine bass 1CH 4ohm 8ohm| | - AliExpress wale wanapenda kufanya project zao za active subwoofers, circuit hizo hapo.

Tafuta driver yako ya maana, na fundi mzuri wa cabinet upate mkito safi.

Naona waliokwisha zinunua wametoa recommendations nzuri.
View attachment 3018635
Kaka umewahi nunua vitu huko?
 
kelphin Mzee wangu alinunuaga 2010 nimekuta home imewekwa stoo, nafkiria ninyanyuke nayo, ushauri wako please!
Ni vitu gani niongeze ili ifikie Requirement yangu.( Speaker haina)

N.b ;Mimi napenda bass mshindo.
Screenshot_20240814-230832.jpg
 
kelphin Mzee wangu alinunuaga 2010 nimekuta home imewekwa stoo, nafkiria ninyanyuke nayo, ushauri wako please!
Ni vitu gani niongeze ili ifikie Requirement yangu.( Speaker haina)

N.b ;Mimi napenda bass mshindo.View attachment 3070253
Tafuta spika zenye ohms sawa pamoja na watss zake, funga kidude cha bluetooth,dukani ni buku 10 ufindi buku 5 atakaye kufukiangia atumie mfumo wa kutumia charger ya simu na sio transorma iliyo ndani ya redio,itakuwa na mngurumo, ukienda kwa fundi nenda na charger ya simu
 
Pesa Pesa ndugu

JBL & Bose Moja ya bidhaa Bora Kabisa Hawa jamaa wanajua mno nini maana ya muziki safi , lain , mkito, Deep base, balance, tone , accoustic yaan ni Burudani tupu

Nina flip 5 Jbl naenyoj vibaya

Let her go - passenger [emoji2424]
Usinambie hako kadude kadogo kanoporomosha muziki heavy mkuu
 
Tafuta spika zenye ohms sawa pamoja na watss zake, funga kidude cha bluetooth,dukani ni buku 10 ufindi buku 5 atakaye kufukiangia atumie mfumo wa kutumia charger ya simu na sio transorma iliyo ndani ya redio,itakuwa na mngurumo, ukienda kwa fundi nenda na charger ya simu
Asante sana
 
Kuna mziki wowote unakua mdogo tu kama Box fulani la mfano wa box la sabuni lakini unapiga ileile? Sipendi hili limuonekano la sabwoofer kubwa kwenye Showcase..
 
Mkuu nina Jbl flip 6 nimeidondosha sasa hivi spika inakasauti fulani sio kazuri kama vile mtu ameweka mkono au kitu kwenye spika..kama ina paraza hivi..mkuu hii kitu inarekebishika??
Yawezekana kuna kitu kimevunjika kimekaa kwenye spika(kinabinya )speaker
Au speaker imecheza
Yess ni issue ndogo
 
Back
Top Bottom