Niulize chochote kuhusu Wilaya ya Sikonge Tabora

Lukula na Kipanga ni vijiji vya zamani
Vipi maembe mwakaka huu yapo mengi? Enzi za utoto tukikuwa tunayafata Lukula na Kipanga,Tena tulikuwa tunatoka kwetu Usunga one tunayabeba kichwani,Ni mazito balaa.
 
Ngoja anaesumbua anajulikana kwa jina la Koboko (Cobra) ambao kwa maeneo ya wilaya ya Sikonge hupendela kuishi katika mashimo ya visuguu au katika mapango ya miti

Jwani cobra ndiye koboko! Na black mamba utamwitaje kwa kiswahili!
 
Mashamba ni mengi sana na uzuri siku hizi tumbaku inalimwa katika kijiji chochote tofauti na zamani ambayo ilikuwa inalimwa katika vijiji maalumu.
Ila sikushauri ulime Tumbaku
Kwanini haunishauri nilime tumbaku Mkuu?, au ni kilimo kigumu sana nini Mkuu?, Tujuzane.
 
Inavituo shikizi vingapi au satellite skul ngapi?
 
Kumbe Sikonge ni wilaya, mimi nilijua kijiji.
 
Waarabu wapo maeneo hayo ya Sikonge na Tutuo ila waarabu wanatabia ya kuoana wenyewe mtoto baba mkubwa na mtoto wa baba mdogo mtoto wa mama mdogo na mtoto mama mkubwa

Hakuna shida hapo, mbona hakuna mtu ambaye yupo hapa duniani ambaye hakuoa ndugu yake! Soma Biblia au Q’uruan ujue kuhusu Adam na Eva/ Hawa!
 
Sijasema kuna shida mkuu
Hakuna shida hapo, mbona hakuna mtu ambaye yupo hapa duniani ambaye hakuoa ndugu yake! Soma Biblia au Q’uruan ujue kuhusu Adam na Eva/ Hawa!
 
Tumbaku ni zao gumu sana ambalo unawajibika takribani mwaka mzima pia zao ambalo linaharibu manzingira sana
Kwanini haunishauri nilime tumbaku Mkuu?, au ni kilimo kigumu sana nini Mkuu?, Tujuzane.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…