Niulize chochote kuhusu Wilaya ya Sikonge Tabora

Niulize chochote kuhusu Wilaya ya Sikonge Tabora

''Dada ukitaka kuolewa ukapata mwanaume wa kinyamwezi andika maumivu.Wanaume wa kinyamwezi wana tabia ya uswali sana kwa sababu ya waarabu.Mwanaume wa kinyamwezi akishakuoa anaweza kuondoka nyumbani akakutelekeza na watoto hata miaka3 amekuachia mzigo kwa ufupi wa hovyo sana''...................................alikikika mlevi mmoja anaongea kwenye kilabu cha pombe za kienyeji
 
Wenyeji wa wilaya hii ni wanyamwezi huku shughuli zao zikiwa ni kilimo ufugaji na uwindaji.
Wanyamwezi pia wamegawanyika katika makabila madogomadogo kwa mfano Wakonongo, wapimbwe nk,
Wilaya ya Sikonge ipo kusini ya Mkoa wa Tabora,
Hii ni wilaya kubwa pengine kubwa kuliko zote Tanzania kwa ukubwa wa takribani 27,873 kilometre za mraba, ni wilaya iliyosahaulika kabisa kimaendeleo tangu miaka ya Uhuru, wananchi wake wengi wao wanaishi katika dimbwi la umaskini mkubwa, Wilaya hii ilikuwa inajulikana kama Wilaya ya Tabora vijijini hadi miaka ya 2000 ndipo ikapewa hadhi ya kuwa wilaya kamili.
 
''Dada ukitaka kuolewa ukapata mwanaume wa kinyamwezi andika maumivu.Wanaume wa kinyamwezi wana tabia ya uswali sana kwa sababu ya waarabu.Mwanaume wa kinyamwezi akishakuoa anaweza kuondoka nyumbani akakutelekeza na watoto hata miaka3 amekuachia mzigo kwa ufupi wa hovyo sana''...................................alikikika mlevi mmoja anaongea kwenye kilabu cha pombe za kienyeji
ha ha ha

Hako ka tabia ka kiarabu ka umwinyi mwinyi kapo Tabora mjini tu sababu Tabora ilikuwa center ya biashara ya watumwa na ndiyo maana kuna shombe wengi mno wa kiarabu hapo Tabora mjini.

Lakini ndani ya wilaya ya Sikonge hakuna tabia ya umwinyi. .

Wanaume wa kimyamwezi sifa ya mwanza Wakarimu, wanajua kupenda na hawawapigi wake zao.....ila tatizo lao kubwa wanatumia pesa vibaya wakishazipa ( vimwaga).
 
Vipi Maisha kwa ujumla?

Ikiwemo Malazi, Chakula, mzunguko wa Pesa, Biashara, Ardhi nk
Wilaya ya Sikonge kwa muda mrefu haikuwa na barabara ya kukatisha kuingia na kutoka kwenye mikoa mingine - kifupi Wilaya ilikuwa kama kisiwa hivi. Kwa sasa ndiyo kuna barabara inajengwa toka Tabora mjini kupitia Sikonge hadi Katavi.

Barabara hii sasa ndiyo itahuisha biashara kati ya wilaya ya Sikonge na Katavi hadi Kigoma.

Ardhi ipo ya kumwaga, lakini kilimo chochote kinahitaji Mbolea, Mzunguko wa pesa hakuna - maisha ni magumu mno hasa wa vijana na kina mama.

Chakula kikuu ni Ugali wa Mahindi - Mboga ni Mlenda, Swalu, nsansa, kisanvu ma msusa - Mboga zote hizi zikiungwa kwa tui la karanga!! Uhodari wa wanawake wa Kinyawezi ni ile sifa yao katika mapishi - ni hatari.
 
Vip kuhusu kuloga/urozi na limbwata
haya mambo yanapungua sababu ya civilization inaongezeka miongoni mwa familia na koo - pia muingiiano mpya wa vijana toka mikoa mingine umesaidia.

Kwa mfano sasa hivi hata vijana wachache wa kinyamwezi ambao wanafanya kazi mijini wanarudi ma kwao kujenga nyumba za kisasa na hata kuwanunua magari wazazi wao - kitu ambacho hapo mwanzo hakikuwepo, ukijenga nyumba nzuri hulali humo maana ni vichapo mwanzo mwisho. ... na ukenda na gari nyumbani siku ya kuondoka haliwaki hata ulete mafundi unaowajua wewe .. hadi linafia hapo hapo!! labda uamue kulivuta.
 
huko sasa ndiyo kulikuwa na kambi za wachawi... ni kweli tarafa hizo zote zipo duni mno kimaendeleo. .. mitaa ya kambi katoto eee
haahaha huko nmepiga misele ile njia unakutana na wanyama wa kutosha aisee.....nitaambatanisha picha nikipata muda..
 
sikonge hiyo....
 

Attachments

  • IMG_20190904_140045.jpg
    IMG_20190904_140045.jpg
    176.4 KB · Views: 24
Watu wanaotaka kuwekeza kwenye ardhi basi waende wilaya ya Sikonge wakawekeze - kule heka 50 unaweza kupewa na kijiji bureeeee hata mia yako hawaitaki. Kule kuna mapori ya balaa..... hukatizi ukiwa muoga muoga
 
kuna kitu vijana wa siku hizi wanaita pisi kali,je hivi vitu huko wanalima?
Wanyamwezi ki asili ni watu waoga mno kufanya biashara zozote za magendo, hata hicho kilimo cha Ngada hawawezi kuthubutu, ila kama wewe unajiamini unaweza kwenda kulima - kuna mapori ya kufa mtu hata mapolisi misitu kufika huko ni mtihani.
 
Back
Top Bottom