Niulize chochote kuhusu Wilaya ya Sikonge Tabora

Niulize chochote kuhusu Wilaya ya Sikonge Tabora

Mashamba ni mengi sana na uzuri siku hizi tumbaku inalimwa katika kijiji chochote tofauti na zamani ambayo ilikuwa inalimwa katika vijiji maalumu.
Ila sikushauri ulime Tumbaku
Vipi huko mashamba ya kulima tumbaku yanapatikanika vipi ndugu yangu?
 
Achana naye huyo haijui Sikonge amesimuliwa tu watu wa huko ni wakarimu sana
Mkuu hayo maneno yako sio ya kweli kabisa ss kwa taarifa yako sikonge inajengwa na wageni na maendeleo ni makubwa sana watu wanaokimbia ni wa kutoka wapi?
 
Magufuli hakuwa na uwezo wa kubadilisha watu labda kwa kuwaharibia uchumi wao
Naamini JPM atawarekebisha wa-Tanzania wote wenye tabia hii, ukiachilia mbalii wasukuma. Halafu yule atakayemfuatia ndiyo atawabadilisha kabisa na kuwagueza kabisa mienendo yao, waelekee kwenye maendeleo perce
 
Huijui Sikonge nadhani umeaimuliwa au alienda kwa ya mambo hayo
Kwani mm nazuia watu wasiende wenyew waende tu....
wakajionee WENYEWE....

Kule Kuna mikasa mingi Sana na mabalaa.....

MAENDELEO hafifu na uduni wa maisha umetamalaki.......

Ushirikina Ni mwingi mno kule Kuna maeneo ukianzisha kujenga nyumba nzuri au ka ghorofa unapotezwa yaan unauwawa kichawi....

Sikonge Ni balaa Achanaa nao kabisa....
Watu wengi tu wameikimbia sikonge na hawataki kupasikia KWA sababu ya ushirikina....
 
Hapana ila Uwensato zamani palikuwa na chatu maana chatu kwa kinyamwezi ni Nsato na Iwe ni jiwe
Vipi maembe mwakaka huu yapo mengi? Enzi za utoto tukikuwa tunayafata Lukula na Kipanga,Tena tulikuwa tunatoka kwetu Usunga one tunayabeba kichwani,Ni mazito balaa.
 
''Dada ukitaka kuolewa ukapata mwanaume wa kinyamwezi andika maumivu.Wanaume wa kinyamwezi wana tabia ya uswali sana kwa sababu ya waarabu.Mwanaume wa kinyamwezi akishakuoa anaweza kuondoka nyumbani akakutelekeza na watoto hata miaka3 amekuachia mzigo kwa ufupi wa hovyo sana''...................................alikikika mlevi mmoja anaongea kwenye kilabu cha pombe za kienyeji

Sio kweli
 
ha ha ha

Iwensato ilikuwa ni kijiji kikubwa mno kabla ya operration vijiji miaka ya 70. Kwa sasa ni mapori matupu - tukiwa wadogo tulikuwa tunakwenda kule kuchuma Mapera, Maembe na matunda mwitu kama nsungwi, ntarali na zambarao nk
Ha ha we jamaa umenikumbusha mbali sana, kuna ntalali, fulu, ndaati, matunda kamasi, ntonga nk. [emoji23][emoji23]
 
Baadaye kutakuja endelea maana kule juu kuna majumba mazuri waliokuwa wanaishi Madaktari wa kizungu na kwa pembeni kuna Hospital ya Kidugalo
Hivi ile hospitali ya kidugalo si ndio inatibu hadi wenye ukoma? Hayo maeneo nimefika miaka ya 1996..
 
Back
Top Bottom