Niulize kuhusu fursa ya masomo Sweden

Safi umetisha mkuu mungu akujarie moyo huo huo kaka

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, binadamu wote tunatakiwa kuwa na msaada kwa wenzetu pale unapoweza. Sijui ni kwa nini Binadamu anakuwa na roho ngumu ya ubinafsi, jeuri na kiburi. Mie nadhani sifa ya Binadamu ni utu, unyenyekevu na kuwajali wanadamu wengine. Tofauti na hapo inakuwa umepoteza au umeishiwa sifa fulani na hivyo unatakiwa kujirejesha kwenye ubinadamu wako. Binadamu bila majivuno, majigambo, ubinafsi, jeuri, kiburi, nongwa, uchoyo na roho nyingine mbaya inawezekana kabisa..
 
Kwanza kabisa nikupongeze kwa namna ulivyoonesha upendo usio kifani kwa sisi watanzani wenzako,maana tupo wengi tuliokuwa na ndoto hizo za angalau kwa ngazi za masters na PhD kufanyia nje ya mipaka yetu. Binafsi nashukuru sana.

Nimejaribu kupitia kozi tofauti tofauti,ila nilichokiona kwenye entry requirement,nyingi zinataka muendelezo,yaani kama ulisoma Degree ya kilimo,basi chaguo lazima liwe la masters ya kilimo,kwamba kama ulisoma kilimo,basi huwezi kusoma masters ya Law au Political science.

Naomba unifafanulie kama sikuelewa vizuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, ulivyoelewa ndiyo sahihi kabisa. Wanataka muendelezo wa career yako. Hiyo ni muhimu kwa sababu hata wakati wa kuelezea work and leadership experience yako utahitajika kuelezea umefanya nini katika career yako.
 
Jibu safi kabisa maana najua ameuliza kinafki wakati kila kitu umeeleza kwenye post vizuri.

Distributed Denial-of-Service
 
Mkuu, ulivyoelewa ndiyo sahihi kabisa. Wanataka muendelezo wa career yako. Hiyo ni muhimu kwa sababu hata wakati wa kuelezea work and leadership experience yako utahitajika kuelezea umefanya nini katika career yako.

mkuu kwanza nakushukuru sana kwa elimu unayotupatia hapa! Unatupa mwangaza sana.

Swali langu nimeanza ku apply PhD in epidemiology huko sweden.. niliona wameandika nikipata nafasi nakua kama employed nalipwa salary.

naomba kuuliza kwa experience yako salary ni nzuri? inaeza nitosha hata nikafanya mambo mengine Tanzania au inaishia kula tu? na je kuna fursa za jobs baada ya kumaliza masomo ya PhD?

natanguliza shukrani


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ndiyo, ukiwa Mwanafunzi wa PhD Sweden unakuwa regarded kama employee, maana yake unapata stahiki zote kama employee. Maisha ya Sweden ni ghali, lakini kwa kiasi kinachotolewa kwa wanafunzi wa PhD itoshe kusema kwamba ukiishi maisha ya kawaida, kwa sisi tunaotoka katika nchi zinazoendelea (Developing countries) kinatosha kabisa kuweka akiba kwa ajili ya maendeleo yako binafsi. Ombea tu mkuu ili upate. Halafu swali lako kuhusu kazi ndiyo unaweza kupata, ni bidii yako tu.
 

nashukuru sana mkuu kwa taarifa


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mimi nitajaribu mwaka huu kuomba masters,

Japokuwa ufahuru wangu wa first degree ni dhaifu...


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mkuu; kukata tamaa ni sumu ya maisha. Kujiona mnyonge ni kukaribisha umasikini wa roho na mwili. Wenzetu wanachozingatia ni ufaulu tu. Kwahiyo kama ulifaulu tayari wewe ni mshindi. Ufaulu wa kwenye makaratasi usikupe shida mkuu. Muhimu ukidhi wanachokihitaji.
Mimi nitajaribu mwaka huu kuomba masters,

Japokuwa ufahuru wangu wa first degree ni dhaifu...


Sent from my iPhone using JamiiForums

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kaka naona umenitia moyo, lazima nifanye hivyo, maana siwezi kujua ngoja nijaribu, inaweza kuwa bahati yangu.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ebwana nikuulize ukiwa unasoma masters wanaruhusu kuja na familia huko...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata mimi nimetafuta scholarship sana bila mafanikio,na nyingi unazotuma maombi hayajibiwi,nikweli nahitaj school for masters program
Kama kuna uwezekano wa kunisaidia nitashukuru
Sent using Jamii Forums mobile app
 
vip kwa certificate pia wanatoa scholarship
 
Hata mimi nimetafuta scholarship sana bila mafanikio,na nyingi unazotuma maombi hayajibiwi,nikweli nahitaj school for masters program
Kama kuna uwezekano wa kunisaidia nitashukuru

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu fatilia posts zote za huu uzi kila kitu nimeweka wazi. Link na maelezo yote yapo. Kama utakuwa na swali zaidi uliza hapa hapa nitakujibu mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…