Kwanza kabisa nikupongeze kwa namna ulivyoonesha upendo usio kifani kwa sisi watanzani wenzako,maana tupo wengi tuliokuwa na ndoto hizo za angalau kwa ngazi za masters na PhD kufanyia nje ya mipaka yetu. Binafsi nashukuru sana.
Nimejaribu kupitia kozi tofauti tofauti,ila nilichokiona kwenye entry requirement,nyingi zinataka muendelezo,yaani kama ulisoma Degree ya kilimo,basi chaguo lazima liwe la masters ya kilimo,kwamba kama ulisoma kilimo,basi huwezi kusoma masters ya Law au Political science.
Naomba unifafanulie kama sikuelewa vizuri.
Sent using
Jamii Forums mobile app