Niulize kuhusu fursa ya masomo Sweden

Niulize kuhusu fursa ya masomo Sweden

Wakuu, imekuwa ni adimu sana kuona Wabongo tukishikana mikono ili kuvuka hatua moja kwenda nyingine yenye mafanikio. Tumezoea kupambana wenyewe na wengi wetu huwa hatupo wazi inapokuja suala la kumueleza mtu mwingine juu ya fursa fulani, tunapenda kuwa wabinafsi na wachoyo.

Kauli hii nimeithibitisha baada ya kutembelea nchi za wenzetu walioendelea (Ulaya) na kuona namna ambavyo Waafrika kutoka magharibi wanavyochangamkia fursa za hapa na pale na namna wanavyoshikana mikono ili kuvuka mahala.

Ni kwa mantiki hiyo basi, ili kuvunja kasumba ya ubinafsi wetu Wabongo, nipo hapa kujibu maswali juu ya fursa ya kimasomo unayoweza kuipata Sweden kwa ngazi ya Shahada ya Uzamili (Masters Scholarship).

Sio masuala ya kuja inbox, wewe uliza hapa hapa public nitakujibu. Sihitaji mtu kuja kunifuata inbox.

Karibuni.
Safi sana , thank you bro
 
Kuna limit ktk umri?
Ni hulka ya mwanadamu kuwa na tahadhari kwa kila jambo, hasa katika Dunia hii iliyojawa na kila aina ya uovu. Na hii inatoa picha na kudhihirisha wazi kuwa jamii yetu uovu ni mwingi kuliko mambo mema. Uovu umewajaza fikra Wanadamu kuliko wema. Mkuu, sihusiki wana sina haja ya kutapeli. Ndio maana nimeelezea hapo kwenye bandiko kwamba sihitaji mtu kuja inbox, uliza hapahapa na utajibiwa hapa hapa. Usiniulize nanufaikaje, waulize JF founders walioanzisha Platform hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
PhD vipi kwa upande wa renewable energy (solar)
Nina uzoefu kuhusu Scholarship za Masters. Sina uzoefu mkubwa wa PhD Scholarship, hata hivyo, naweza kuelezea kidogo nachofahamu. PhD kwa Sweden ukipata fursa ya Scholarship unakuwa regarded kama mwajiriwa. Yaani unapewa ajira ya muda mfupi kwa kufanya researches na wakati mwingine unaweza kuhusika kufundisha hapa na pale. Unalipwa kabisa mshahara kama mwajiriwa mwingine kulingana na matakwa. Zipo na unaweza kupata. Nimeona baadhi ya wanafunzi wa PhD wakiendelea na masomo yao katika chuo kimojawapo. Kwa maelezo zaidi, tembelea link hii>>>> PhD programmes in Sweden

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nina uzoefu kuhusu Scholarship za Masters. Sina uzoefu mkubwa wa PhD Scholarship, hata hivyo, naweza kuelezea kidogo nachofahamu. PhD kwa Sweden ukipata fursa ya Scholarship unakuwa regarded kama mwajiriwa. Yaani unapewa ajira ya muda mfupi kwa kufanya researches na wakati mwingine unaweza kuhusika kufundisha hapa na pale. Unlipwa kabisa mashara kama mwajiriwa mwingine kulingana na matakwa. Zipo na unaweza kupata. Nimeona baadhi ya wanafunzi wa PhD wakiendelea na masomo yao katika chuo kimojawapo. Kwa maelezo zaidi, tembelea link hii>>>> PhD programmes in Sweden

Sent using Jamii Forums mobile app
Shukran ngoja vijana wajaribu kama kunaweza kupatikana ujiko huko. Shule ni kama benki
 
mkuu ubarikiwe sana na je kuna scholarship za first degree kwa mtu aliyemaliza diploma??

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu sina ufahamu wa kutosha juu ya hili. Mie nina ufahamu zaidi kuhusu Masters. Hata hivyo, katika pita pita zangu sijawahi kusikia Scholarship za bachelor kwa Sweden. Vilevile, elimu ya bachelor kwa vyuo vingi ninavyo vifahamu hutolewa kwa lugha yao ya Kiswid. Hii pia inaweza kuwa mojawapo ya limiting factor.
 
Wakuu, imekuwa ni adimu sana kuona Wabongo tukishikana mikono ili kuvuka hatua moja kwenda nyingine yenye mafanikio. Tumezoea kupambana wenyewe na wengi wetu huwa hatupo wazi inapokuja suala la kumueleza mtu mwingine juu ya fursa fulani, tunapenda kuwa wabinafsi na wachoyo.

Kauli hii nimeithibitisha baada ya kutembelea nchi za wenzetu walioendelea (Ulaya) na kuona namna ambavyo Waafrika kutoka magharibi wanavyochangamkia fursa za hapa na pale na namna wanavyoshikana mikono ili kuvuka mahala.

Ni kwa mantiki hiyo basi, ili kuvunja kasumba ya ubinafsi wetu Wabongo, nipo hapa kujibu maswali juu ya fursa ya kimasomo unayoweza kuipata Sweden kwa ngazi ya Shahada ya Uzamili (Masters Scholarship).

Sio masuala ya kuja inbox, wewe uliza hapa hapa public nitakujibu. Sihitaji mtu kuja kunifuata inbox.

Karibuni.
Kila sholarship wanataka mtuawe amefanya pepa za TEOFL je na huko sweden nao wana haya mambo?

Je watu wao mawasiliano wanatumia english? Na ubaguzi huko upo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante mkuu kwa kuruhusu kuulizwa.

Natamani saana kusoma masters hiyo nchi ila pesa haitoshi.

Nimesoma hapo juu wasema tumechelewa. Kwa hiyo mwezi wa 10 nikiomba chuo nikapata nafasi.

Hapo ndiyo patamu.
1. Utaratibu wa kuomba chuo gharama zipoje? Wanahitaji nini na nini?

Nianzie hapo kwanza.
 
TOEFL na IELTS sanasana ni kwa nchi ambazo their first language is English kama vile UK, US, CANADA, Australia n.k

Kwahiyo kwa nchi za Ulaya kama vile Scandinavian (Sweden, Finland, Norway, Denmark) na nchi nyingine za Ulaya kama Austria, France, Germany na Netherlands ambako lugha yao ya kwanza siyo English, hizo mambo za IELTS na TOEFL kwa uzoefu wangu, kwa kiasi kikubwa sijaona wakiomba uwe umefanya hiyo mitihani.

Hivyo, kwa jibu fupi, ili usome Sweden kwa sisi Wabongo ambao tunatumia English kuanzia Sekondari hadi Chuo Kikuu, tunahitajika kuwa tumefaulu English O-level. Hicho ndicho kigezo pekee ninachokifahamu.

Katika swali lako la pili; nchi zilizoendelea(Ulaya) wanathamini sana Utamadumi wao; hivyo lugha ya mawasiliano ni lugha yao. Kwa Sweden wanatumia Kiswidi(Swedish). Hata hivyo; karibia 85% ya Waswid wanazungumza English vizuri kabisa. Ukipata Scholarship, lugha ya kufundishia kwa Masters ni English.

Suala la Ubaguzi naomba nilisizungumzie sana; binafsi sijawahi kukutana na changamoto hii. Sweden na Nchi nyingi za Scandinavian wanajitahidi sana kuthamini utu wa kila MTU. Ila siku zote, mweusi ni mweusi na Mzungu ni Mzungu tu. Japo hutaona Ubaguzi kwa kusikia wala kwa macho, ila kiasili mweupe ni mweupe na mweusi ni mweusi tu.

Generally, nchi nyingi za Ulaya kwa sasa Ubaguzi siyo agenda kubwa. Sanasana labda Ubaguzi utausikia kwa Wazee na Watoto. Ila vijana wamestaarabika. Mwisho kabisa, kwa mtizamo wangu, nadhani Sweden ni miongoni mwa nchi zenye kiwango cha juu cha ustaarabu Duniani.

Gharama unayotakiwa kulipa ni admission fee peke yake. Scholarship haulipi gharama yoyote. Gharama ya admission kama sijakosea ni 990 au 900 SEK hivi. Ambayo ukiibadili kwa TZS ni kama 210,000- 230,000 hivi.

Asante saana.

Ni changamoto gani ulikutana nazo wakati unaomba hadi kufanikiwa? Zitanisaidia nami.

Haujanijibu wanahitaji nini wakati wa maombi ukiachana na gharama.
 
Mambo ya wenzetu yamenyooka hayana kupindisha. Nyeupe ni nyeupe na nyeusi ni nyeusi with no excuses! Hivyo mambo yalienda smoothly kwa kuwa nilikuwa nikifanya kila kinachohitajika kwa wakati wake kwa kufuata maelekezo.

Changamoto kidogo sana ilikuwa kuambatanisha Passport maana wakati naomba niliweka National ID kwa sababu nilikuwa sijapata Passport. Waliponiuliza nikawaambia nitawatumia ndani ya muda mfupi na nikataja lini itakuwa tayari. Mungu ni mwema nikafanikiwa kuipata na kuituma kama nilivyoahidi.

Requirements zipo nimeambatanisha kwenye link kwenye posts zilizotangulia. Ila kwa ufupi, requirement kubwa ni uwe na experience ya kazi at least 2 -3 years. Na uwe na Leadership experience pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu nashkuru kwa majibu mazuri na je vipi kuhusu wale wabeba box kunaingilika huko sweden ? tupe nondo mzee maana wengine kuingia huko kwa kusoma inaweza kua mtihani
Mkuu sina ufahamu wa kutosha juu ya hili. Mie nina ufahamu zaidi kuhusu Masters. Hata hivyo, katika pita pita zangu sijawahi kusikia Scholarship za bachelor kwa Sweden. Vilevile, elimu ya bachelor kwa vyuo vingi ninavyo vifahamu hutolewa kwa lugha yao ya Kiswid. Hii pia inaweza kuwa mojawapo ya limiting factor.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TOEFL na IELTS sanasana ni kwa nchi ambazo their first language is English kama vile UK, US, CANADA, Australia n.k

Kwahiyo kwa nchi za Ulaya kama vile Scandinavian (Sweden, Finland, Norway, Denmark) na nchi nyingine za Ulaya kama Austria, France, Germany na Netherlands ambako lugha yao ya kwanza siyo English, hizo mambo za IELTS na TOEFL kwa uzoefu wangu, kwa kiasi kikubwa sijaona wakiomba uwe umefanya hiyo mitihani.

Hivyo, kwa jibu fupi, ili usome Sweden kwa sisi Wabongo ambao tunatumia English kuanzia Sekondari hadi Chuo Kikuu, tunahitajika kuwa tumefaulu English O-level. Hicho ndicho kigezo pekee ninachokifahamu.

Katika swali lako la pili; nchi zilizoendelea(Ulaya) wanathamini sana Utamadumi wao; hivyo lugha ya mawasiliano ni lugha yao. Kwa Sweden wanatumia Kiswidi(Swedish). Hata hivyo; karibia 85% ya Waswid wanazungumza English vizuri kabisa. Ukipata Scholarship, lugha ya kufundishia kwa Masters ni English.

Suala la Ubaguzi naomba nilisizungumzie sana; binafsi sijawahi kukutana na changamoto hii. Sweden na Nchi nyingi za Scandinavian wanajitahidi sana kuthamini utu wa kila MTU. Ila siku zote, mweusi ni mweusi na Mzungu ni Mzungu tu. Japo hutaona Ubaguzi kwa kusikia wala kwa macho, ila kiasili mweupe ni mweupe na mweusi ni mweusi tu.

Generally, nchi nyingi za Ulaya kwa sasa Ubaguzi siyo agenda kubwa. Sanasana labda Ubaguzi utausikia kwa Wazee na Watoto. Ila vijana wamestaarabika. Mwisho kabisa, kwa mtizamo wangu, nadhani Sweden ni miongoni mwa nchi zenye kiwango cha juu cha ustaarabu Duniani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Shukrani kwa info iliyo shiba!!

Je ni chuo gani kizuri cha maswala ya uhandisi unakijua pande hizo?

Je ukishapa scholaship ela unapewaje?

Nauli ya kufika chuo inakuaje?

Je unakua unaliwa kwa mwezi au unapewa yote at once?
 
mkuu nashkuru kwa majibu mazuri na je vipi kuhusu wale wabeba box kunaingilika huko sweden ? tupe nondo mzee maana wengine kuingia huko kwa kusoma inaweza kua mtihani

Sent using Jamii Forums mobile app
Pengine naweza nisiwe na jibu sahihi sana juu ya hili swali. Ila kwa maoni yangu, kila kitu kwenye hii Dunia inawezekana iwapo utaweka nia na uthubutu. Huwa napata wakati mgumu kuelewa ni kwa namna gani wazamiaji wanaweza ku_survive Sweden kwa siku za mwanzo. Tuchukulie kwa mfano wewe ni mzamiaji umeingia na huna uhusiano na mtu yeyote, Je unapataje kazi?

Kazi za mabox zipo ila namna ya kuzipata ndo napata wakati mgumu kuelewa.Hii ni kwa sababu ili ufanye kazi Sweden hata kama ni kazi ya kumsaidia mtu nyumbani kwake lazima uwe na kitu wanaita Personal number, kuna kuna masharti ya kupata hiyo personal number maana ni namba inayokutambulisha wewe ni nani unakaa wapi na uthibitishe uwepo wako halali. Personal number inakuwezesha pia kupata National ID.KIla unakoenda lazima uoneshe hiyo personal number, sasa wazamiaji wanapataje madili na kuzamia na kufanikiwa? Kwakweli sina jibu la uhakika na sina uelewa wa kutosha juu ya hilo.

Wazamiaji pekee naofahamu wanafanikiwa ni wanaotoka Ertrea, hawa wanafanikiwa kwa kuwa nchi yao inajulikana inachangamoto zao zinajulikana. Pengine ili uzamie labda upate mke Mswidi akulee na hivyo akuwezeshe kupata kitambulisho hicho chenye personal number. Changamoto nyingine ya uzamiaji wa Sweden ni lugha, yaani wanatumia lugha yao kwa 99.99% kwa kila kitu. Na lugha inakuwezesha kupata kazi kwa urahisi. Sasa wazamiaji wanafanikiwa vipi kwakweli sina uzoefu wa hilo na pengine niseme sina ufahamu wa kutosha juu ya hilo.
 
Mambo ya wenzetu yamenyooka hayana kupindisha. Nyeupe ni nyeupe na nyeusi ni nyeusi with no excuses! Hivyo mambo yalienda smoothly kwa kuwa nilikuwa nikifanya kila kinachohitajika kwa wakati wake kwa kufuata maelekezo.

Changamoto kidogo sana ilikuwa kuambatanisha Passport maana wakati naomba niliweka National ID kwa sababu nilikuwa sijapata Passport. Waliponiuliza nikawaambia nitawatumia ndani ya muda mfupi na nikataja lini itakuwa tayari. Mungu ni mwema nikafanikiwa kuipata na kuituma kama nilivyoahidi.

Requirements zipo nimeambatanisha kwenye link kwenye posts zilizotangulia. Ila kwa ufupi, requirement kubwa ni uwe na experience ya kazi at least 2 -3 years. Na uwe na Leadership experience pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huwezi ukadanganya kama hauna leadership experience...sijawahi kuwa kiongozi.
 
Shukrani kwa info iliyo shiba!!

Je ni chuo gani kizuri cha maswala ya uhandisi unakijua pande hizo?
Mkuu, Ulaya kwa ujumla na nchi nyingi zilizoendelea, elimu yao siyo ya magumashi wala kubabaisha. Yaani kila chuo kinakidhi viwango na elimu inayotolewa ni kiwango kinachokubalika, hivyo chuo chochote ukipata itakuwa ni sahihi. Vyuo vipo vingi siwezi kuvitaja. Naomba utembelee link niliyoweka kwenye post za mwanzo imeanisha Programmes zote na chuo husika. Utajichagulia mwenyewe. Kikubwa elewa kuwa kila chuo ni kizuri.

Je ukishapa scholaship ela unapewaje?
Unaingiziwa kwenye account yako.

Nauli ya kufika chuo inakuaje?

Nauli unajitegemea mpaka kufika. Ukishafika unarudishiwa gharama zako za nauli.
Je unakua unaliwa kwa mwezi au unapewa yote at once?

Unapewa pesa ya kujikimu kila mwezi. Siyo at once, upewe yote utoroke?? Pesa haina undugu wa kudumu na kiumbe Mwanadamu..
 
Back
Top Bottom