Naomba unielekeze kupika BIRIANI
Mahitaji
1 kilo mchele wa basmati
1 kilo nyama iwe ya kuku au ng'ombe au mbuzi kata katika umbo dogo la kutosha kula kisha ichemshe na tangawizi na kitunguu swaumu, unga wa binzari (turmeric powder) pili pili manga na chumvi ili kuweka ladha nzuri. Ikisha iva itoe iweke pembeni na mchuzi wake uweke pembeni utautumia baadae.
1 kilo ya vitunguu kata slice ( mviringo)
1 kilo nyanya nyekudu zilizoiva, osha vizuri kisha katakata saizi ndogo ndogo sana
1/2 lita ya mafuta ya kupikia
1/2 kilo ya samli au mafuta yeyote ya kupikia
2 maggi chicken soup cubes
3 kijiko kidogo cha chai unga wa pilipili mwekundu
1/2 kijiko kidogo cha chai unga wa binzari
3 kijiko kidogo cha chai unga wa girigilani (giligilani)
2 kijiko kikubwa cha chakula mchanganyiko wa tangawizi na kitunguu swaumu vilivyosagwa
korosho iliyo kaangwa usizisage zibaki nzima robo kikombe
majani ya girigilani kichanga kimoja
mbegu za nzima ya hiriki kiasi
Pili pili manga nzima kiasi
Chumvi kiasi
Jinsi ya kuanda
Weka mafuta katika sufuria yako iliyo juu ya moto tayari, kisha kaanga nyama yako iliyokwisha chemshwa mpaka iwe na rangi ya kahawia (golden brown)
Kisha itoe nyama hiyo na ichuje mafuta ili mafuta yanayobaki weka kitunguu na endelea kukaanga kwa dakika 7-10 kisha weka unga wa binzali, unga wa pili pili mwekundu, unga wa girigilani, mbegu za hiriki na nusu ya mbegu za pili pili manga.
Changanya vizuri mpaka utapata mchanganyiko mzuri mkavu miminia humo maji uliyotunza baada ya kuchemshia ile nyama yako na kuiweka pembeni ipoe. kisha weka nyanya fresh ndani ya sufuria yako pika mpaka maji yakauke na mafuta yaanze kuoneka kwa juu ndani ya sufuria.
Kisha weka nyama yako ndani ya sufuria pole pole halafu punguza moto acha ijipike kwa muda mpaka mchuzi wako na nyama vikamate ladha pia usisahau kuweka chumvi kulingana na ladha unayopenda.
Chukua sufuria nyingine weka mafuta ya samli na vitunguu ilivyoslice kisha kaanga na majani ya girigilani, korosho funika kwa dakika 10 i, kisha weka mchele wako mkavu uliokwisha oshwa vizuri na uchanganye vizuri ongeza vikombe 5 vya maji na chumvi kidogo mchele ukishaanza kuchemka funika sufuria lako na punguza moto maji yakisha kauka kiasi weka mchanganyiko wa ile nyama yako nusu tu juu ya wali wa basmati acha wali uive kabisa kisha itakua tayari kula na pakua chakula chako kikiwa cha moto