ephen_
JF-Expert Member
- Oct 28, 2022
- 14,949
- 54,485
Tamu sana☺️MAHITAJI
*Boga 1
*Tui La Nazi 2 Vikombe
*Sukari 1 kikombe
*Hiliki 1/2 kijiko cha chai
UTAYARISHAJI NA UPIKAJI:
1.Unamenya maboga kiasi ukipendacho.
2.Unayakata kata vipande vidogo vidogo.
3.Unayachemsha na tui la pili mpaka yawive lakini yasije kuvurugika.
4.Maji yakishaanza kukauka unatia sukari kiasi ukipendacho na hiliki.
5.Kisha unamimina tui la nazi.
6.Unaiwacha ichemkie na kabla kukauka tui unaepuwa na tayari kuliwa.