Niulize kuhusu mapishi ya futari mbalimbali

Futar ya boga inapikwaje?

MAHITAJI

*Boga 1
*Tui La Nazi 2 Vikombe
*Sukari 1 kikombe
*Hiliki 1/2 kijiko cha chai



UTAYARISHAJI NA UPIKAJI:

1.Unamenya maboga kiasi ukipendacho.

2.Unayakata kata vipande vidogo vidogo.

3.Unayachemsha na tui la pili mpaka yawive lakini yasije kuvurugika.

4.Maji yakishaanza kukauka unatia sukari kiasi ukipendacho na hiliki.

5.Kisha unamimina tui la nazi.

6.Unaiwacha ichemkie na kabla kukauka tui unaepuwa na tayari kuliwa.
 
Nijuze futari ya kufuturu...pasi na gharama....
 
Hakuna futari nayoipenda kama hii ila zikiwa na maharagwe pembeni, ila kwenye mapishi ndio yalikuwa yananishinda, hongera kwako.
Yum yum yum
Nalog off
 
Futar ya boga inapikwaje?


Vipimo
Boga la kiasi - nusu yake
Tui zito la nazi 1 ½ gilasi
Sukari ½ kikombe
Hiliki ½ kijiko cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
  1. Menya boga kisha katakata vipande vya kiasi.
  2. Weka katika sufuri tia maji kiasi ya kuchemshia na kuwiva bila ya kubakia maji mengi.
  3. Changanya tui na sukari na hiliki kisha mimina juu ya boga wacha katika moto dakika chache tu bila ya kufunika.
  4. Epua mimina katika chombo likiwa tayari.
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

nimekopy hapa JINSI YA KUPIKA BOGA LA NAZI - Muislamu
 
Nijuze kupika uji wa pilipili
 
My dear, tambi hizi zinaitwa pasta.
Spaghetti ni zile ndefu kama vijiti na mara nyingi zinapikwa za chumvi na mchuzi kama macaroni.
Zote zinaitwa Tambi tu bana. Acha kukomplicate mambo
 
Natamani sana kupika ili biriani, ila nimekutana na vitu humu ndani hata sijawahi visikia sehemu, hiyo giligilani ndio kitu gani?
 
Kwa darasa hili Kachori naweza kupika bila wasi wowote ule, kwasababu Mama alikuwa anapika KATLESI akawa ananielekeza kwa vitendo.

Maandalizi yake, na mapishi yake yanafanana kwa kiasi fulani, tofauti KATLESI madonge yake unachovya kwenye Mayai badala ya Unga
 
Natamani sana kupika ili biriani, ila nimekutana na vitu humu ndani hata sijawahi visikia sehemu, hiyo giligilani ndio kitu gani?
Mbegu za dania au kotmiri
 
Almost sawa tofauti ni mahitaji (ingedients)
 
Futar ya boga inapikwaje?
Kata boga menya kisha lipange sufuriani. Kuna na uchuje matui 2 ya nazi la kwanza zito na la pili jepesi lile jepesi weka kwenye boga na chumvi
(pinch),sukari (kiasi upendacho) na iliki kisha injika jiko vikishatokota na tui kupungua unaweka lile zito linachemkia mpk kubaki rojo linalokutoshe unaepua tayari kwa kuliwa usiyakoroge hata kidogo
 
My dear, tambi hizi zinaitwa pasta.
Spaghetti ni zile ndefu kama vijiti na mara nyingi zinapikwa za chumvi na mchuzi kama macaroni.
pasta na spaghetti ni tofauti hizo unazosema ni spaghetti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…