Nabii gani au mtume wa Tanzania ambaye ni wa kweli unayemtambua?
Tunapima roho kwa kutumia njia 2.
1.Kwa kumuuliza Mungu na Mungu kwa njia ya ROHO MTAKATIFU hutoa majibu
2. Kwa kupima uwiano wa neno na maisha au huduma ya mtu.
Kama una vitu hivyo viwili utawatambua tu.
Manabii wengi hapa Tanzania na kwingineko si wa kweli kwa kipimo cha neno.
Mfano
Nabii yeyote anayetoza pesa ili awatabirie au kuwawekea watu mikono huyo hajatumwa na MUNGU.
Yesu alisema mumepewa bure toeni bure
Sasa mtu akikutoza hata mia Tano kama gharama ya kumuona, kununua kifaa cha kiroho au kuonana naye huyo si nabii wa kweli.
Pia kipimo kingine ni matokeo ya unabii wao.
Mtu akisema jambo na lisitimie huyo hakutumwa na Mungu.
Njia ya tatu ni kutazama maisha ya huyo mtumishi anapokuwa nje ya kanisa.
Mtu ana kesi za kutia mimba wake za watu, kesi za kitapeli waumini.
Mtu ana ghorofa lakini hawezi kuishi hata na mtoto wa dada yake amsomeshe.
Mtu ana private jet, account ina bilioni 3 lakini anamwambia muumini alete elfu 10 ambariki apate mtaji au kazi badala ya kutoa yeye huo mtaji.
Matendo kama hayo ni ishara huyo nabii , mchungaji, Mtume, Mwinjilisti au mwalimu hana Mungu.