Niulize swali lolote kuhusu uchumi au biashara

Mimi mwenyewe nimelicopy huko linkedin umalijibu vizuri sana.
 
Nimefungua biashara ya spares za pikipiki kijiji fulan mbaya zaidi kuna jirani yangu yeye ni fundi mwenyeji pia ni mmiliki wa hilo duka Je nitumie mbinu gani kuwin wateja ikiwa kwa sasa wateja wengi wanaenda kwa jamaa kwa sababu ni mzaliwa wa pale na pia ni kabila lao na pia wanasema ni fundi mzuri kuliko fundi wangu.ASANTE
 

Bwana Billie pole sana.
Ingawa hili swali ni la marketing and branding ila nitalijibu.
Swala lako ni gumu, watu hupitia competition ila hii yako imekaa kiugumu sana🤣😅
Tunaweza kujaribu, kulifix hili kwa kuinvest zaidi kwa wateja kuliko faida. Hapa itabidi ufanye vitu vya kuvutia wateja ili waje na uhakikishe akija mara moja basi atarudi tena na atamwambia mwenzake aje kwako.

Fanya vitu vitakavyofanya watu wajue pale kuna duka la spare za pikipiki, hapa utakuwa unafanya marketing.
Pili hakikisha mteja akija basi anaridhika na hatokaa arudi kule kwa mkabila mwenzake.
Nashindwa kukupa mifano ya moja kwa moja kwa kuwa mimi si mjuzi sana wa maswala ya pikipiki na ufundi wake. Labda kwa kujaribu; Vipi kama utaamua kutoa huduma ya ufundi bure? Yaani mtu akija kununua spare kwako basi utamuwekea bure? Kama haiwezekani basi punguza bei ya ufundi.
Naamini huyo mshindani wake kinambeba kujuana na watu, pamoja na kukaa kwa muda mrefu so anao loyal customers. Una silaha moja ya kumshinda ambayo ni kutoa great services kuliko yeye hapo hata hao wanyaturu wenzake watakuja kwako wewe muha.😅
 
Mbona kama CHATGBT answers?
 
Asante sana nimechukua point kuwa niwekeze zaidi kwa customers kuliko faida i mean naweza punguza bei ya vifaa ili competitor wangu atubu ukizingatia napata spare kwa supplier ambae ananiuzia bei chee
 
Asante sana nimechukua point kuwa niwekeze zaidi kwa customers kuliko faida i mean naweza punguza bei ya vifaa ili competitor wangu atubu ukizingatia napata spare kwa supplier ambae ananiuzia bei chee
Safi, and goodluck sir!
 
Nini faida ambayo wanaipata nchi kama Kenya ambao fedha yao inathamani kuliko ya Tanzania lakini most of the products price Zina range mule mule. Mfano utakuta labda bei ya soda in Kenyan shillings ni sawa sawa na bei ya soda in TZ shilling?
Ngoja nijaribu kujibu Kwa uelewa wangu wa stand.
Nchi kuwa na fedha yenye thamani kubwa kuliko nyingine mara nyingi husababishwa na kiasi kikubwa Cha uuzwaji wa bidhaa nje wa nchi husika. Na mara nyingi biashara hii hufanywa na wawekezaji kutoka nje na wachache Sana wa ndani, Kwa mkanda huu raia wa kawaida na serikali yake hawana Chao kwenye mnyororo huu wa thamani ya fedha ya nchi husika. Kuna wakati fedha ya Zimbabwe ilikua na thamani Sana kutokana na biashara kubwa ya mahindi yaliyokuwa yakizalishwa na walowezi wa kizungu, baada ya Mugabe kuwafukuza wazungu kwenye umiriki wa ardhi kilichofuta ni kushuka thamani Kwa fedha.
 
Kwa hio haina haja ya kusoma uchumi kama haikufanyi uweze kutumia hizo kanuni uwe tajiri. Kama nyie wachumi hamuwezi kujifanyia utajiri mnawezaje kuiletea nchi utajiri ?
Kwa nini wachumi huwa mnapenda kueleza nadharia za kukuza uchumi wakati nyie binafsi mmeshindwa kuzi apply nadharia za uchumi. Je wachumi hamuoni kuwa mnastahili kulaimiwa kwa kushindwa kujinasua na kuinasua nchi ktk umasikini ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…